Kitendo cha kuja kuomba ushauri jinsi ya kummudu mkeo kwa jambo ambalo una yakini kabisa kuwa keshalifanya ni dhahiri kuwa humo ndoani huna kauli.
Kama kweli ungekuwa unasimama kama mume kwenye ndoa yako ilipaswa ujue kila mzunguko wa mkeo, kitendo cha kukutana nae na usijue anakoelekea ukabaki na dhana tu, hiyo ni wazi kuwa anakuchukulia kama binti mwenzie. Mwanamke anaemuheshimu mumewe hasa asingekuwa na ujasiri wa kwenda kuukatikia baada ya kukutana na wewe. Lazima angegeuza na kurudi nyumbani. Kitendo cha kuendelea na safari yake alijua fika kuwa huna madhara.
Subiri siku akuletee mume mwenzio ndani kwenu kabisa, nahisi hapo utakuwa na ithibati tosha.