Hivi mkeo unamuachia Tsh. ngapi unapotaka kwenda kazini?

Inategemea sana na kipato ulicho nacho, maana kila mbuz hula urefu wa kamba.
 
Shida ya kuoa mke tegemezi hii, kwani yeye haendi kazini..? Mimi sijui huu utaratibu wa kuweka pesa za matumizi mezani always kuna pesa sehemu kwa ajili ya matumizi msingi. Ikiisha anachukua kwenye akaunti au nitachukua mimi.
Hakuna mwanamke mtegemezi ,kama wote mnafanya kazi basi itabidi uajiri Hg.

Kama anafanya kazi kwa wahindi mshahara laki na nusu ni bora akae nyumbani niwe namlipa kwa kazi anazofanya home.
 
Ukiskia mke kupenda ndio hivyo...Wala hawanaga matata huyo kama hujaoa oa kabisa
Tumepanga harusi tuifanyie mwisho wa mwaka huu, tena iwe simple sana na ikiwezekana tusitumie zaid ya laki 2. Hakuna michango.
 
Eeh yaani mgeni kaja,mtu anajinunisha plus kulalamika hana pesa,full kisirani yaani wanawake sie Mungu anatuona.

Yaani kuna anko wangu alioa mwanamke yule alikuwa mchoyo,anamaind kula,ukienda kwake ushibe kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
fala kweli huyo mwanamke af sass mkiamaindishaga misosi mnapata faida gani?
 
sisi wazee wa mikeka tunaomba tuwe wa mwisho kutoa maoni.
 
ulimpa ya mboga mkuu

hukusema naya vocha😂😂🤣🤣🤣🤣


wallahy wanawake sisi tunaraha🤣🤣.

hapo bdo hujaombwa na ya salon
 
[emoji3064][emoji3064][emoji3064]
kumbe na baba na mama mkwe wanawekwa kwenye hesabu!! Basi hiki ndo kinaweza kuwa chanzo cha vijana wengi kutooa! Nilikuwa najua kuwa ntakuwa natoa 5,000 kwa siku, kazi kwisha! Ningevuta chombo hata kesho kutwa!!
Usiogope wewe oa tu 5000 ndio bajeti ya familia nyingi hapa bongo ,cha msingi jitahidi ununue mahitaji kama mkaa ,mafuta ya kula,unga,mchele,mazagazaga ya gengeni mambo yana enda vizuri ishi kulingana na uwezo wako usisikilize watu ,nyumba zina siri nyingi kuna wengine hata hawaachi kitu nyumbani ila barabarani wameulamba
 
Nimekupenda Bure kwa Busara zako. Kipato chako kidogo unakipangilia vizuri. Nimekusoma unajali Sana familia. Mungu akuongoze upate kipato kikubwa zaidi na zaidi. You will make a great father figure. Salute
 
Oa mwanamke mwenye uwezo wa kujilisha.
Vijana wanataka wenye chura ambao mara nyingi ni wapaka rangi. Wenye wake wanaojiweza wanasoma comments tu na kushangaa kijana anavyoacha 500k wakati ameshanunua mazaga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…