Hivi mliojenga hapa mjini, mliwezaje? Mna miujiza ama ni wezi?

G4N

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
4,283
Reaction score
9,925
Kila kitu hapa mjini kinahitaji hela, unawezaje kusevu hela mpaka ufike hatua ya kujenga?

Na ukichukuwa mkopo benki ndiyo hatari zaidi. Kama ni mkopo wa kutegemea mshahara utakuta unakuwa mteja wa kausha damu, na kama ni biashara utaona inakufa mbele ya macho yako.

Mjini mambo yote yanahitaji fedha. Unawezaje kujenga ???

Bado kuna michango ya harusi, kitchen party, birthday party, misiba, na mitoko ya weekends, bila kusahau kusaidia ndugu na jamaa wa vijijini.

Naomba mbinu mlizotumia. Na muwe wakweli.
 

Sasa wewe ukisikia kuna mtu ana nyumba 80 si unaweza kusema huyu ni mdogo wake Jesus.
 
Kwanza lazima upunguze ndugu na marafiki , ili ujijuwe mwenyewe. Pili ujiulize ni kitu ngani kichopo ndani yako unacho weza kuuza kwa watu wanao kuzunguka. Ukisha fanya hivyo unajenga ndani mwaka mmoja. Pia punguza starehe
 
Rudi kijijini Mjini hupawezi!
 
Cc. Matunga PESA...kwetu pazuri.
 
Mbinu zinazotumika ni mchanganyiko sana, mbinu inayoongoza ni wizi( haijalishi aina ya wizi, ili mradi ulipata kiharamu), bonus ( usijali aina ya bonus, cha msingi ni bonus baada ya kusota), kudunduliza ( hapa utakuta nyumba moja imejengwa na mafundi kumi), mkopo ( toka benki, ofisini,jamaa, vikundi nk), kutunukiwa( zawadi toka ofisini, mshikaji, zali, bahati nasibu), urithi, kuokota nyumba.
 
Kwanza lazima upunguze ndugu na marafiki , ili ujijuwe mwenyewe. Pili ujiulize ni kitu ngani kichopo ndani yako unacho weza kuuza kwa watu wanao kuzunguka. Ukisha fanya hivyo unajenga ndani mwaka mmoja. Pia punguza starehe
Kula vizuri na vinono mfn kuku,nyama,kuvaa vizuri tupe ufafanuzi..
 
Mkuu hakuna miujiza komaa tu utatoboa
 
Wewe ndiye umeutendea haki uzi wangu. Watu wengine badala ya kutoa mbinu walizoombwa kwenye uzi, wanatoa tambo na vijembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…