Hivi mnaamini haya magari ya kutembelea ya mchina yanayokuja Africa?

Mkuu zile golden dragon za mwendokasi gearbox ni German origin na engine ni American Cummins, body ndio maranda ya mbao za kichina na tubati twepesi twa hapo alaf {kidding}.
Beberu effects hii na hakuna ukweli ,wao reality imeshawapiga na kila kitu wanachotumia ni made in China na hata Tesla zinazotengenezwa Shanghai considered higher quality kuliko za California
 
Nimeipitia hio Jaecoo 7. Sio gari ya kipuuzi. Engine na gearbox sio za kinyonge. Na bei UK ni kuanzia £29,000 hela hii unanunua BMW,Benz,VW nzuri kabisa. Kwa Tz ni kama 110m kabla ya ushuru. Mpaka uiendeshe Tz sio chini ya 200m. Hadi hapo sio ya kinyonge.
 
Zinawaka moto kwa sababu moto upo, ukiondoa moto zitakua salama.
 
Sema watu wengi hawajajua kuhusu mchina na mkakati wake. Mchina ni mtu wa biashara.

1. Mchina anakuuzia kitu sawa na bei unayotoa. Bei ndio itaakisi ubora, teknolojia na thamani ya fedha ya kitu. Mwaka jana niliagiza Laboratory Microscope china, walinipa invoices kama tano kwa kifaa kile kile, watengenezaji tofauti. Kila hii inazidi ingine ubora na bei zinatofautiana kadiri ya ubora. Hukosi kitu china ila unapata kulingana na bei yako. 😊

2. Mchina hatengenezi kitu ufe nacho, ufunge ndoa nacho. Anakuuzia kitu ukitumie, kikulipe, kikupe thamani ya fedha, kichoke kwa muda flani, ukanunue kingine. Greda ya Cattapillar mpya ni 140 ni 1.3B, hii ukinunua unatumia miaka mpaka 30. mchina ana greda yake ya Sany, Shantui, LiuGond anauza 350M, unatumia miaka mitano unapima screpa. Ila inakuwa imekurudishia pesa na faida. 😊

3. Anatengeneza kitu mbadala wa kilichopo sokoni kutoka kotoka mataifa mengine kwa bei ya kumudu. Pikipiki DT Yamaha, inauzwa 19M, Mchina akaja na Sinoray 250 kwa milioni tatu mpya. Unatumia zako miaka mitatu, unanunua nyingine na spea unamuungisha sana.

Turudi kwenye mada: Mchina sasa hivi anatengeneza magari mazuri na ya bei naafuu na ya kisasa, unanunua kwa bei rafiki na kulingana na thamani ya fedha kwa muda wa kadiri/mfupi. Ni gari unanunua, unatumia inachoka kwa muda flani, unaenda nunua tena. Mchina anamananisha biashara, nunua, tumia urudi tena kununua.
 
Mwanzo zilivyoanza kuingia zilikuwa zinawaka moto balaa. Drum brakes zilikuwa zinachemka hadi matairi yanaungua. Naona new gen zimerelebisha hili tatizo.

Mchina ni mjuzi sana wa "customer feedback and complaints", anaboresha vitu vinavyolalamikiwa. Mfano; Howo tractors, mwanzoni alilalamikiwa sana cabin kutokuwa na comfortability, sasa hivi anatengeneza cabin ina kila starehe na dereva anahisi kama yupo kwenye Scania tuu. 😊
 
Mkuu hata gari za Europe au Japan hawakusudii ukae nalo mpaka lifanane na wewe. Kuna msemo wao vitu fulani ni life time kubadili kumbe wao life time ni miaka 5-6 kutoka mpya ushaachana na hio gari ume upgrade kwenye toleo jipya. Je wabongo tunaweza?
Kama unaweza kubadili gari mpya kila baada ya miaka 3-5 Mchina anakufaa sana. Na hapa nazungumzia mpya.
 
ntajie basi la mchina namba C lililopo barabarani?
 

Mpya zero KM kwa mchina inawezekana mkuu hata kwa mtu wa kipato cha kawaida. Nimeona hapo juu unasema Jetour ni "expensive and popular" kuzid baadhi ya toleo za G-Wagon. Hebu fafanua mkuu. Wagon toleo gani? Je, ni mpya au used ya kufananisha na JT?
 
Mpya zero KM kwa mchina inawezekana mkuu hata kwa mtu wa kipato cha kawaida. Nimeona hapo juu unasema Jetour ni "expensive and popular" kuzid baadhi ya toleo za G-Wagon. Hebu fafanua mkuu. Wagon toleo gani? Je, ni mpya au used ya kufananisha na JT?
Kuna hizi changan , zilitolewa milio kama yote🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…