Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

Nimeishi mikoa takribani 21 ya TZ BARA, ukiacha Kagera, Rukwa, Ruvuma, Katavi na Mtwara. Kila eneo kuna raha zake na karaha zake:-

DAR - msimu wa mvua hakufai, ni mji wa starehe na utafutaji pesa..kila biashara inatoka!
ARUSHA/MOSHI - mji wa starehe haswaa, na gharama za maisha zipo juu, hali ya hewa safi
MWANZA - pilika nyingi, starehe na biashara kadhaa
KIGOMA - hali nzuri ya hewa, vyakula kibao bei nusu, hakunaga njaa!
IRINGA - mji wa vyakula, hali ya hewa bariiiidi
DODOMA/SINGIDA - mvua chache kwa mwaka, baridi na upepo mkali kiangazi, maisha simpo!
nk...nk.....

Hata hivyo, binadamu tumeumbwa kuyazoea mazingira. Kwa mpambanaji wa kweli mbali na maradhi, kila mji/mkoa unaweza kuishi na mambo yakaenda.
 
Huo ni uongo mkubwa, Mimi sio mwenyeji wa Dodoma,Hali ya Dodoma ni nusu jangwa sikatai,ardhi yake Ina rutuba sana,mshindi na mazao hawatumii mbolea za viwandani.Kuhusu ujenzi mafundi Kwa kweli ni ghari kulinganisha na kwetu Mbeya!Nyumba nyingi zimejengwa kwa kufuata ramani zilizokuwepo zamani ikiitwa CDA,Hayo mengine ni yeye kutokubaliana kuishi Dodoma.Pana fursa nyingi sana,Mfano ufugaji,kilimo,hakuna zao halikubali Dodoma ni Wewe tuu kujipanga.Nina miaka kumi sitamani kurudi Mbeya.Maana ardhi Mbeya ni finyu sana.
 
Dodoma ina wingu una weza zani mvua ina nyesha kila wakati kumbe linawapa moyo tu..usha kutana na nyoka wa ngapi hadi leo
Hivi toka lini mvua ndio imekuwa main factor? mikoa mingi yenye kupata mvua nyingi kwa mwaka tena nyingi sana lakini haina fusra. Mimi nahisi kunachuki nyingi sana kutoka kwa wakazi wa Dar ile kuchukuliwa hadhi ya kisiasa au cake kugawanywa tu imekuwa kero kwao. Nchi hii watu wamepata shida sana ilikuwa ukitaka chochote lazima uende Dar sasa leo watu wanayapata maeneo yao na kikubwa mji wa Serikali ukikamilika 100% ndio basi Dar ni biashara tu.
 
😂😂Mwanzoni nilivyokuja nilisema nini hiki. Lakini kukaa Kaa nikaona kumbe ni mindset tu. Umesema upo kikazi halafu unauliza wanajengaje bila ramani? Dodoma ipi unajenga bila ramani.?
Kuweka Frame za mbele tu walitaka turudi jiji eti kibali Cha mchoro tukapate.😂
Nakuelewa changamoto uliyopata kutoka Arusha ghafla tu uhamie Dodoma ni majonzi ya muda kiukweli.
 
Dabalo umenikumbusha mbali sana,hivi bwawa lipo bado

Ova
Mkuu kama miti enzi za primary tulipandishwa sana na hapo unakabidhiwa mti au kipande cha bustani ukihudumie lakini nilipita baada ya miaka mingi, bado hali ipo vile vile

Nadhani ujangwa ni uoto wa asili na ili kuuondoa bhasi utahitaji nguvu ya zyada sana

By the way dodoma ya leo hii haina ubovu huo ukiilinganisha na ile ya zaidi ya miaka 15 iliyopita wakati ndo naingia. Ni bhasi tu binadamu tuna chaguo zetu binafsi
 
Uko sahihi mkuu hakuna kujenga bila kuwapa Ramani,Zamani ramani zilikuwa mpaka ukachague CDA!,Sasa hivi jiji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…