DOKEZO Hivi Msumi ipo Dar es Salaam kweli?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Historia haidanganyi....unawajua wakazi wa mwanzoni wa Msumi, ndio wale wale wa Mbagala !!!!
Kabisa
Mwanzoni walikuwa wamakonde lakini kwa sasa ni mchanganyiko mpaka kina Bwashee...Ngosha...Kamwene....Wapemba....hadi Waha kutoka mwisho wa reli.....bila kuwasahau kina Mwa..mwa.... na Washomiree
 
Halafu huku chini wanadai mbunge anatia aibu CCM halafu wakati huo huo wanamsifia ati mganga wake ni mzuri.
 
Kwa watu wanaojua nini wanafanya hawawezi ongea mambo ya kijinga kama discussion zilizomo humu ndani.

Vijana wengi wa kileo huwa wanafuata umeme na maji na barabara. Then wanaenda kuweka makazi kwenye 20×20 . Huu ni ujinga kwa watu wanaojielewa.

Watu wengi waliowahi maeneo msumi wamejenga kwenye maeneo yenye ukubwa wa sqm 2500. Manake nini, ardhi ya DSM inapanda thamani kila siku. SLOGAN ni hamia sehemu mji ndo ukufuate.

Usifuate mji. Wajanja wamenunua maeneo wamejenga hardware viwanda vya tofali nk. We kaanzishe kiwanda cha tofali sinza.

Kwa hizi akili za kufuata lami na maji ya bomba sijui kwenye suala la ardhi tutawaachia nini watoto wetu.

Kumbuka tabata ilikuwa pori na wengine waliogopa kununua kwani waliamini yalikuwa makazi ya wanyama wakali kama simba. Kunawazee wakikumbuka ujinga waliofanya wanalia machozi.


Uzi huu utunzwe vizuri kunawatu baada ya miaka 10 tu watalia machozi. Nami ngoja nikatafute eneo msumi litanifaa baadae
 
Uko sahihi mkuu kwa kuwatia moyo watu wa Msumi
 
Ndio Yule Boya muuza Mayai kajenga huko 🤣🤣
 
Wakazi wa Msumi tujuane tafadhali!
Nimeishi huko mwaka wa 6 Sasa sijawahi jutia,..!!
Hivi mlitegemea serikali iweke maji kwenye ngedere,ijenge Barabara pasi watu kuwepo?
Punguzeni kukatisha Tamaa watu,Kuna jambo ukiliongelea watu tunajiuliza uwezo wako wa kufikiri.
Nimezaliwa kimara,hapakuwa na maji Wala Barabara baada ya muda tukapata.
Vivyo hivyo,sinza k/Koo,tabata,ubungo nk.
Hatuwezi kulala na kuamka kukuta Kila eneo Lina maji na Barabara bila kusahau umeme,MAENDELEO HATA YA NYUMBANI KWAKO HAYAJI KWA SIKU MOJA!
 
Sawa,wajenge kimpangilio basi
Maeneo yakawe kwenye ramani
Sawa ,vp miundo mbinu iko mwake

Ova
 
Hakuna mpangilio wa kimakazi
Huko na hiyo inacsababihwa
Na watu wenyewe

Ova
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ntajitahidi niende nkajionee, maana napasikia tyuu.
Ndy uende na msakuzi huko sjui kwa lipelanya kwa rubaba huko 😄
Sema kuna mashuwa wanaishi
Sema njia mbovu....
Serikali sijui halmashauri ya ubungo iwaonee huruma wenye magari huko

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…