DOKEZO Hivi Msumi ipo Dar es Salaam kweli?

DOKEZO Hivi Msumi ipo Dar es Salaam kweli?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Msumi ni Kilometer chache sana kutoka stendi ya mabasi ya Magufuli.

Sasa cha ajabu ni kwamba Msumi ipo kama vile hata wakuu wa Mikoa waliopita hapo Dar na wasasa si ajabu hawajui iko upande gani wa mji, achilia mbali DC.

Mbunge wa Ubungo (labda atapeleka pua) kwa ajili ya kampeni, Sina hakika na Mkurugenzi na blah blah wengine, kutoa umeme.
  • Msumi hakuna barabara.
  • Msumi hakuna zahanati zingatia ni eneo lenye kaya zaidi ya laki moja, Ref.Google Map.
  • Msumi hakuna kituo cha Polisi
  • Msumi hakuna maji ya bomba lakini kuna ofisi za CCM kila baada ya kilometer chache.
Kma si ushirikina wa Wamakonde ni nini?

Msumi hakuna madaraja baada ya kuzolewa na mvua, zingatia madaraja yote yalijengwa kwa nguvu za wananchi.

Tukisema Msumi hakuna Zimamoto tutakuwa tumeungana na washirikina manake mji mzima zimamoto ni moja tu pale faya kwa ajili ya Kariakoo na Muhimbili, hili hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kulizungumzia manake akili zao ziko kunako matumbo yao.

Haya tuendelee Msumi Shule ya Msingi ni moja na haitoshi zingatia idadi ya kaya, nilisikitika mvua inanyesha wamesongana kibarazani kisa wanasomeaga chini ya mti.

Kuna majengo ya madarasa yapo upande wa kulia kama unaelekea msumi maeneo ya uwanjani sijui ni ya sekondari au ya msingi wenyeji mtatujuza.

Msumi hakuna kituo cha daladala ingawa daladala zipo kwa uchache zingatia hakuna barabara ndio kisa na wenye mabasi hawaitaki njia hiyo na abiria ni wengi sana sana kaya laki moja, mara waseme darajani mara waseme center lakini kote ni ushirikina tu.

Msumi hakuna miundo mbinu ya kukusanya taka.i.e Dampo kwa sasa hawataona athari.

Ngoja kidogo, kaya laki moja na kila siku watu wanazidi kuhamia, watu wa msumi hebu wekeni kero zenu hapa manake hampo jijini wala mamkoa.

Msumi Chui ametoroka msituni anaonekana mtaani, zingatia Msitu ameshapewa mwekezaji.
hivi serikali ilipima viwanja huko?
 
Misumi ,msakuzi,mpiji na makabe kote huko hakuna maji,hospitali Kuna kizahanati tu na barabara ndiyo balaaa yaani makorongo Kwa kwenda mbele lakini yule mbuge wao Kila kuchangia anasifu rais kwa kazi nzuri kiasi kwamba akiwa karibu unaweza kuzaba Kofi.
 
Halaf unakuta akina Intelligent businessman wanapata guts za kukutongoza wakat mtu ulishaanza kupambana na kodi toka mwaka 2001!! We intell wewe achaga utukutu wako mdogo angu 😂. Ww 2001 bado unatumia vibagadu kujifunza kutembea dede maana hakuna baby walker enz hizo.
Humu shida vijana wanadangajika na I’d feki😁😁😁😁
 
  • Msumi hakuna barabara.
  • Msumi hakuna zahanati zingatia ni eneo lenye kaya zaidi ya laki moja, Ref.Google Map.
  • Msumi hakuna kituo cha Polisi
  • Msumi hakuna maji ya bomba lakini kuna ofisi za CCM kila baada ya kilometer chache.
Kma si ushirikina wa Wamakonde ni nini?

Msumi hakuna madaraja baada ya kuzolewa na mvua, zingatia madaraja yote yalijengwa kwa nguvu za wananchi.

Mzee baba, wabongo si tumezoea kujenga kiholela kwa kuvamia maeneo ambayo hata masterplan haijatoka...

Hizi ndio kadhia zake na inabidi kuzikubali tu kwa sasa, kwa slogan yetu imekuwa JENGA kwanza, maendelo yatakuja baadaye...
 
Hii sahau mzee, bado sana hata kwny huo mradi haipo!!
Hovyo sanaa hawa watu, wangejua tuna teseka na magari mabovu yale kiasi gani aisee
Nchi ya hovyo sana hii, eti Dar es salaam hii **** maeneo ni vumbi tupu na yana watu wengi ni aibu ndani ya jiji kubwa kama hili kuwa na sehemu kama mpigi magohe au msumi hakuna lami kabisa achia wingi wa watu maeneo hayo dah!
 
Kuna mradi wq DMDP phase two watajenga barabara ya msumi kilometa 9.08 . Ujenzi unaanza mwezi wa saba. Kipindi wanatangaza zabuni ili mkandarasi apatikane. Tembelea page ya mkuu wa mkoa you tube autakuta kafafanua barabara ambazo zitapitiwa lami
Tunaomba hiyo link tuone kama tumekumbukwa au niaje.
 
Hovyo sanaa hawa watu, wangejua tuna teseka na magari mabovu yale kiasi gani aisee
Nchi ya hovyo sana hii, eti Dar es salaam hii **** maeneo ni vumbi tupu na yana watu wengi ni aibu ndani ya jiji kubwa kama hili kuwa na sehemu kama mpigi magohe au msumi hakuna lami kabisa achia wingi wa watu maeneo hayo dah!
Ni huzuni, hakuna anayejali.
 
Back
Top Bottom