Hivi mtu anakuwa katika hali gani ya akili hadi anakubali kuolewa mke wa tatu, wa nne nk?

Ya kwamba umshangae mtu anaye taka kuolewa uke wenza ila hutomshangaa mwanamke kuliwa hovyo hovyo mwisho wa siku anazaa watoto wasio julikana baba zao wako wapi?
 
Hata wewe unaonekana unakubali kuwa mke wa pili kwa hiyo huna tofauti na huyo anayekubali kuwa watu na nne. Ungekuwa bora sana kwenye mada yako usimamie kwenye mke mmoja tu.

Hebu lete sababu ya kuona ni afadhali kuwa mke wa pili na kukataa kuwa wa tatu?
 
Ndio maana Mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam.
Ilitoa tafsiri ya neno kubaka na kusema Mwanamke habaki maana kinacho bakwa ni kinacho ingiliwa na sio kuingilia.

Kwa tafsiri hiyo hiyo haitowezekana, habadani kwa Mwanamke kufanya afanyayo Mwanamume.

Pia ni ngumu sisi Majanamume kuona kwa mtazamo wa ndoa, maisha na mahusiano kwa mtazamo wa kike.
 
Jambo lingine baya kuhusu polygamy kama ikizingatiwa vizuri ni kwamba inapunguza sana uwezekano wa wanaume wengine wasio na hadhi kubwa kicheo, umaarufu au pesa katika jamii kupata wenza wazuri.
Hakuna Mwanamke anashusha vigezo vyake, hata Sasa wanawake wanapenda wanaume wenye vitu vyao.
 
Mleta mada na wanaokusapoti,mko kiimani zaidi,kutoka kwa watu wa magharibi,eti afadhali niwe mke wa pili,why sasa wa pili!!!,,mi nilidhani kwa msimamo wako,utataka uwe wa pekee tu kwa mmeo.
Ngoja niwaambie kwanza kisayansi na kimaumbile,mwanamke katu abadani awezi olewa na mwanaume zaidi ya mmoja,pili population wise wanawake ni wengi kuliko wanaume ( mfano huu hata mfugaji wa kuku anaelewa,jogoo mmoja majike kumi au zaidi),, nadhani hizo ndo point kuu kubwa, kwamba kwanini mtu anaeowa mke zaidi ya mmoja haipaswi na wala haifai kumshangaa kuoa hivyo na kumshangaa mwanamke aliye kwenye ndoa ya namna hiyo.,haifai pia kumshangaa kumuona eti hamnazo.
Niwaulize hivi mwanamke kuwa wa pili au watatu,wanne,na mdangaji au mchepuko wa fulani ni lipi bora???,, Kwa kuwa haya yanatokea kwa wanawake wengi wenye mitazamo kama yenu,eti mtu anakataa kuolewa kama mke wa tatu,lkn anaona bora awe mchepuko wa fulani,hivi nani kawaroga, yaani unaruka mkojo unakanyaga...............!!!!!?? Kweli !!! ,,Mwisho wa siku majanga mengi wajichumia buuure kabisa. Na baadhi ya wanaume pamoja na kuwa na uwezo mzuri kiuchumi anaishia na mke mmoja na michepuko kadhaa,sasa hivi hujui kuwa unatawanya uchumi wako bila sababu, mwisho wa siku unafirisika hivi hivi!!, wakati ungeowa kihalali uchumi wako ungekuwa sana tu.🫵🫵
 
Mh! kaa pembeni wewe wacha kiherehere sijakufata wewe nimemfata Bantu!, siwezi kupigana na kimtu ambacho bado kinanuka mikojo kuwa na adabu mbele ya wakubwa!.
KENZY Jitu fulani hivi linajiamini, eti kimtu. Nani kakwambia nakufuata wewe mi namfuata Bantu na hapo ndipo utajua nanuka mkojo gani.
Hili ni kojo sio mkojo mshua.
Utakapokuta naikung'utia kwa juu ndipo utakaa pembeni uyatazame mamikunjo yako mbavuni humo ujute kushindana na vijana shababi.
Ushazeeka kaa pembeni utafia kwenye vinena unapambana na vijana shauri zako.
We sasa hivi bakia na hao wenzio age go, mveshane manepi vizuri.
 
Hakuna Mwanamke anashusha vigezo vyake, hata Sasa wanawake wanapenda wanaume wenye vitu vyao.
Polygamy inazidisha ukubwa wa hili tatizo hasa enzi hizi ambapo kuna income quality kubwa iliyopitiliza wachache wakijilimbikizia mali.
 
Polygamy inazidisha ukubwa wa hili tatizo hasa enzi hizi ambapo kuna income quality kubwa iliyopitiliza wachache wakijilimbikizia mali.
Michepuko
Mipango ya Kando
Vimada

Undhani hawa pia wanasababishwa na polygamy,
Kumbuka Mwanamke ni Hypergamy hivyo humfuata
Mwanaume mwenye kitu mkononi.

Yoda mzee
Hatuwezi kuelezea muono wa kike kwenye mapenzi,
Maisha na Mahusiano.

Tuwaachie Wanawake wenyewe tu
 
Mh!
 
Polygamy haizuii kufanya genes zitawanyike as long as watu walio karibu ki genes hawataoana. Nobody is saying the whole world should be polygamous, hii ni choice kwa wale wanaotaka.

Utawanyanyapaa watu wanaooa na kuamua kutozaa watoto pia kwa sababu watafanya genes zao ziishe kuongezeka kabisa kupitia kwao?

Ukiongelea mfumodume hata ndoa tu inampa mwanamme nguvu. Tuoige marufuku ndoa?

Kuna wanasayansi jamii wameangalia na kuona polygamy inawagmfaidisha wanawake pia. Na kama wanawake wamechagua wenyewe, wewe ni nani uwapangie jinsi ya kuolewa?

Mimi sipigii kampeni polygamy, lakini naona kama kuna kampeni ya kuwadogosha na kuwapangia watu walioamua kuwa katuka polygamy.

Waachieni, hili ni jambo la uamuzi wa mtu binafsi.
 
Jambo lingine baya kuhusu polygamy kama ikizingatiwa vizuri ni kwamba inapunguza sana uwezekano wa wanaume wengine wasio na hadhi kubwa kicheo, umaarufu au pesa katika jamii kupata wenza wazuri.
Hapo huoni kuwa ukikataza polygamy unawazuia wanawake wengi wanaotaka kuolewa na wanaume wenye vyeo, umaarufu, pesa katika jamii, jambo ambalo no haki yao pia kama wao wanawake, wanaume hao na mke au wake wa wanaume wao wamekubaliana?

Hiyo ni haki yao ya kimsingi unayoivunja.

Na hao wanaume wasio na mali labda hiyo ndiyo motivation yao ya kutafuta mali.

Mtu mwingine anaweza kukuhoji, huoni kuwa mtu masikini kutaka kuoa ni kutaka kuleta matatizo ya kuendeleza umasikini tu?
 
Labda nikuulize umefiwa na mme wako around una miaka kama 40 na watoto wawili,anakuja kukuowa mwanaume kama mke wa pili je utakubali?
 
Kuwa mke wa pili tu siwezi.... mbona nitashinda napigana tu naye....akiamka tu kichwa! 🤒
Wanawake WA siku hizi mnaendekeza wivu kupitiliza ndo maana mnaongea hivi
Enzi za mababu zetu mbona hayo mambo yalikuwa freshy tu
 
Nature yenyewe inawafavour wanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja kulingana na ratio za jinsia KE na ME
Wanawake ni wengi kuliko wanaume Duniani kote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…