Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

tatizo wanadamu tunahadithiana vitu ambavyo wenyewe tumekuja dunianii tumevikuta na vingine hata hatujawahi kuviona . mfano tu ni uwepo wa pepo na kuzimu ,paradiso na motoni.
hakuna mwenye kuyajua haya . sijui ibilisi aliletwa duniani hizo zote story tu uhalisia anaujua yeye aliyeumba hii dunia
 
Mtafaruku ulianza baada ya binadamu kuumbwa na kupewa mamlaka kuliko ibilisi... jamaa aka mind kwamba wao wameumbwa kwa roho na moto inakuwaje watawaliwe na alieumbwa kwa udongo na kupuliziwa pumzi ya uhai... so jamaa akaamua kumsanua binadamu ale tunda la kutambua mema na mabaya ... so ili kuweka mstari mapema akatolewa asile tunda la uzima wa milele... ina maana Adam angesanuka akawahi mtini asingekufa na ingekuwa Mungu kaanzisha adui mwingine msumbufu uwenda kuliko ibilisi... na ili wasiwe na umoja Mungu akaweka uadui baini yao. Maana callable yao bado ingekuwa kasheshe.
Hizi ni hadithi tu, ni hekaya za kale za baadhi ya binada kujipa majibu kwa mambo magumu yaliyokosa majibu.
 
Ndio maana imekuwa ni kawaida tu kumkuta mtu ni mfia dini haswa ila ni mzinifu,muongo,muuaji,mchawi,tapeli,mwizi, mnafiki n.k.
🤣🤣🤣🤣 hapo ndio ujue ibilisi ni tatizo lilomshinda Mungu
 
Kitendo cha Mungu kumtupa Ibilisi duniani ni kitendo cha uonevu mkubwa sana kwa binadamu.

Ibilisi sio levo za binadamu ni levo ya Mungu maana yake Mungu yeye angekomaa naye Ibilisi hukohuko mbinguni mpaka kieleweke. Kutuletea Ibilisi huku duniani ni kutuonea tu maana hatuna uwezo wowote wa kupambana naye.

Kama Ibilisi aliweza kupigana vita kuu mbinguni akiwa na malaika wake sasa binadamu ataweza kweli kupambana na kiumbe kama hiki?

Kiumbe ambacho kiliweza kupambana na malaika wa Mungu na kikafanikiwa kuwashawishi baadhi ya malaika kwenye vita kuu mbinguni na wakaasi sasa wewe binadamu utaweza kweli kupambana na Ibilisi?

Kama mbinguni tu Ibilisi alisumbua sana ambako ndiyo kuna Mungu na malaika huku duniani tutamuweza kweli?

Kama Ibilisi anauwezo wa kuingilia mipango ya Mungu na kuiharibu kama ule wa bustani ya Edeni na Mungu hamfanyi chochote anaishia tu kuwapa adhabu zisizo na maana yoyote Adam na Hawa. Hiki kiumbe sisi binadamu tutakiweza kweli?

Ilifikia hatua Mungu mwenyewe aliamua kumtoa kafara mwanaye wa pekee( Yesu) ili aweze kupambana na Ibilisi ila mission ikabuma. Sisi binadamu tutaweza kweli kupambana na Ibilisi?

Hivi unajua kama Ibilisi anaongea na Mungu moja kwa moja? Maana yake Mungu na Ibilisi huwa wanaonana. Unajua mazungumzo ya Mungu na Ibilisi kuhusu Ayubu? Sasa sisi binadamu tutaweza kweli kupambana na Ibilisi anayeweza kuongea na Mungu moja kwa moja?

Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani?
Hapa binadamu tumeonewa sana.

Jukumu la kupambana na Ibilisi ni jukumu la Mungu mwenyewe na sio la binadamu hivyo Mungu amtoe Ibilisi duniani na akaishi naye mbinguni sisi huku hatumuwezi.

Ndio maana imekuwa ni kawaida tu kumkuta mtu ni mfia dini haswa ila ni mzinifu,muongo,muuaji,mchawi,tapeli,mwizi, mnafiki n.k.

Nani kakudanganya kuna binadamu anaweza kupambana na Ibilisi?
Mhhh
 
Back
Top Bottom