Historia fupi ya Iblis na uasi wake.
Iblis ni jini na hakuwa malaika licha ya kuwa alipata kipaumbele cha kuishi pamoja na malaika huko mbinguni. Iblis alinyanyuliwa na malaika akiwa ni kiumbe mchanga sana katika dunia hii mara baada ya malaika kutumwa kuja kuwaangamiza majini waliokuwa wakifanya uasi hapa duniani,ikumbukwe kuwa majini walipata kuishi katika dunia hii miaka mingi kabla ya uumbwaji wa mwanadamu ila walikengeuka na kufanya ufisadi mwingi sana. Iblis aliachwa na wazazi wake hivyo malaika wakaomba idhini kwa Mungu waondoke nae wakamlee huko mbinguni.Walikubaliwa na hatimaye iblis alikua katika mikono ya malaika , na alipata elimu kubwa tu na pia alikuwa ni kiumbe mchamungu sana.Mtume Muhammad (sala na amani ziwe juu yake) alinukuliwa akisema kuwa hapana sehemu yoyote katika ardhi hii yenye ukubwa wa kiganja cha mkono isipokuwa iblis aliinamisha paji lake la uso chini na kumsujudia Mungu.Alikuwa ni kiumbe aliyefanya sana ibada ila ndani yake alikuwa na kibri/majivuno ambayo malaika hawakuweza kuyajua ila Mungu alimjua kwasababu alimuumba kwa moto na sio Nuru kama ilivyokuwa kwa malaika.
Baada ya majini kufanya uasi na kufurushwa huku duniani ,Mungu akaamua kuumba kiumbe mwingine ambae atakuja kuwa mtawala katika ardhi hii, nae si mwingine bali ni ADAM. Uumbwaji wa adam ulitokana na udongo mweusi wa mfinyanzi tena uliovunda. Ndio asili ya mwanadamu.
Adam aliumbwa kwanza kama fremu tu ambalo lilikuwa halijapuliziwa roho, Iblis alikuwa akiliona fremu la kiumbe huyu mpya wa ajabu, kisha alikuwa akilizunguka na kupita ndani ya mwili wake na kisha kutoka kisha akajisemea kuwa hakika huyu ni kiumbe dhaifu sana na pindi atakapopuliziwa roho basi mimi ndio ntakuwa mwalimu wake.
Malaika mwanzo walikuwa na wasiwasi juu ya kiumbe huyu mpya kuwa pindi atakapoumbwa na kukabidhiwa utawala huku duniani basi atakuja kuyafanya yale waliyoyafanya majini (uasi na umwagaji damu) ila Mungu alikuwa against na maono yao na akawaambia kuwa hakika anayajua yale ambayo malaika hawayajui.Adam akakamilika kuumbwa kisha Mungu akampulizia roho na haraka adam akapata uhai. Kitu cha kwanza Mungu alichompa Adam ni ELIMU. Utambuzi wa kujua kila kitu mpk vile ambavyo malaika hawavijui. Kisha akawaita Malaika,iblis na Adam wote wahudhurie kwani kuna mtihani anataka kuwapa.Mungu alivileta vitu vingi kisha akawaambia malaika pamoja na iblis wavitaje vitu hivyo.Malaika na iblis pamoja wakashindwa kwani walikuwa hawana elimu navyo basi akaitwa Adam akaambiwa kuwa watajie majina ya hivyo vitu, Adam akataja kila kitu kwa usahihi kabisa na alifaulu ule mtihani ndipo Mungu akawaamrisha malaika pamoja na iblis kuwa wamsujudie Adam kumpa heshima. Malaika kutokana na kuwa waliumbwa kwa Nuru na wanafanya yale wanayoamrishwa, basi wote wakasujudu isipokuwa iblis yeye aligoma kusujudu.
Iblis alisimama pamoja na Adam wakati malaika wote wameinamisha mapaji yao ya uso chini, ndipo Mungu akamuuliza Iblis ni nini kilichokufanya uikatae amri yangu?
Iblis akajibu kuwa hakika yeye ni bora kuliko Adam kwani ameumbwa kwa Moto na adam ameumbwa kwa udongo hivyo asingeweza kumsujudia Adam.
Aliiasi amri ya Mola wake mbele ya kundi lote la malaika na licha ya kuasi kwake bado alikataa kurejea kwa mola wake kuomba toba na msamaha. Alishaamua kama mbwai na iwe mbwai. Hapo ndipo MUNGU alipoamua kumlaani Iblis na akafukuzwa kutoka katika kundi la malaika. Iblis aliipokea laana ile ila alikuwa na ombi moja tu kwa Mungu. Mungu akamruhusu aombe anachokitaka ndio akaomba kuwa apewe uhai mrefu mpk mwisho wa dunia hii yaani awe miongoni mwa viumbe vitakavyokufa mwisho.
Mungu alimkubalia , na baada ya ombi lake kupitishwa kwa hasira akasema kwa kuwa Adam ndio amesababisha Mungu kumlaani basi atahakikisha kuwa anavikalia mbele,nyuma,kushoto na kulia vizazi vya adam ili visiielekee njia ya Mungu, ili mwisho wa siku apate watu wengi wa kuingia nao motoni.
Mungu akamjibu palepale kuwa kwa hakika Iblis hana uwezo wa kupoyosha waja wake isipokuwa kwa yule atakaeamua kumfuata.Na kwa hakika ataijaza jahannam kwa iblis na wale wote watakaomfuata.
Yote haya yanatokea huko mbinguni hakuna kiumbe chochote kilichowahi kumuona Mungu ana kwa ana. Sio Adam,sio malaika wala sio huyo Iblis .Walikuwa wakipokea tu sauti ila hakuna aliyemuona Mungu toka ulimwengu unaumbwa mpk pale utakapoisha.
Mungu atakuja kujidhihirisha kwa waja wake watakaoingia peponi tu ndio watapata kumuona. Na hakuna zawadi kubwa mwanadamu atawahi kuipata kama nafasi ya kumuona Mola wake. Mungu atujaalie tuwe miongoni mwao ameen.