Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Historia fupi ya Iblis na uasi wake.

Iblis ni jini na hakuwa malaika licha ya kuwa alipata kipaumbele cha kuishi pamoja na malaika huko mbinguni. Iblis alinyanyuliwa na malaika akiwa ni kiumbe mchanga sana katika dunia hii mara baada ya malaika kutumwa kuja kuwaangamiza majini waliokuwa wakifanya uasi hapa duniani,ikumbukwe kuwa majini walipata kuishi katika dunia hii miaka mingi kabla ya uumbwaji wa mwanadamu ila walikengeuka na kufanya ufisadi mwingi sana. Iblis aliachwa na wazazi wake hivyo malaika wakaomba idhini kwa Mungu waondoke nae wakamlee huko mbinguni.Walikubaliwa na hatimaye iblis alikua katika mikono ya malaika , na alipata elimu kubwa tu na pia alikuwa ni kiumbe mchamungu sana.Mtume Muhammad (sala na amani ziwe juu yake) alinukuliwa akisema kuwa hapana sehemu yoyote katika ardhi hii yenye ukubwa wa kiganja cha mkono isipokuwa iblis aliinamisha paji lake la uso chini na kumsujudia Mungu.Alikuwa ni kiumbe aliyefanya sana ibada ila ndani yake alikuwa na kibri/majivuno ambayo malaika hawakuweza kuyajua ila Mungu alimjua kwasababu alimuumba kwa moto na sio Nuru kama ilivyokuwa kwa malaika.

Baada ya majini kufanya uasi na kufurushwa huku duniani ,Mungu akaamua kuumba kiumbe mwingine ambae atakuja kuwa mtawala katika ardhi hii, nae si mwingine bali ni ADAM. Uumbwaji wa adam ulitokana na udongo mweusi wa mfinyanzi tena uliovunda. Ndio asili ya mwanadamu.

Adam aliumbwa kwanza kama fremu tu ambalo lilikuwa halijapuliziwa roho, Iblis alikuwa akiliona fremu la kiumbe huyu mpya wa ajabu, kisha alikuwa akilizunguka na kupita ndani ya mwili wake na kisha kutoka kisha akajisemea kuwa hakika huyu ni kiumbe dhaifu sana na pindi atakapopuliziwa roho basi mimi ndio ntakuwa mwalimu wake.

Malaika mwanzo walikuwa na wasiwasi juu ya kiumbe huyu mpya kuwa pindi atakapoumbwa na kukabidhiwa utawala huku duniani basi atakuja kuyafanya yale waliyoyafanya majini (uasi na umwagaji damu) ila Mungu alikuwa against na maono yao na akawaambia kuwa hakika anayajua yale ambayo malaika hawayajui.Adam akakamilika kuumbwa kisha Mungu akampulizia roho na haraka adam akapata uhai. Kitu cha kwanza Mungu alichompa Adam ni ELIMU. Utambuzi wa kujua kila kitu mpk vile ambavyo malaika hawavijui. Kisha akawaita Malaika,iblis na Adam wote wahudhurie kwani kuna mtihani anataka kuwapa.Mungu alivileta vitu vingi kisha akawaambia malaika pamoja na iblis wavitaje vitu hivyo.Malaika na iblis pamoja wakashindwa kwani walikuwa hawana elimu navyo basi akaitwa Adam akaambiwa kuwa watajie majina ya hivyo vitu, Adam akataja kila kitu kwa usahihi kabisa na alifaulu ule mtihani ndipo Mungu akawaamrisha malaika pamoja na iblis kuwa wamsujudie Adam kumpa heshima. Malaika kutokana na kuwa waliumbwa kwa Nuru na wanafanya yale wanayoamrishwa, basi wote wakasujudu isipokuwa iblis yeye aligoma kusujudu.

Iblis alisimama pamoja na Adam wakati malaika wote wameinamisha mapaji yao ya uso chini, ndipo Mungu akamuuliza Iblis ni nini kilichokufanya uikatae amri yangu?

Iblis akajibu kuwa hakika yeye ni bora kuliko Adam kwani ameumbwa kwa Moto na adam ameumbwa kwa udongo hivyo asingeweza kumsujudia Adam.

Aliiasi amri ya Mola wake mbele ya kundi lote la malaika na licha ya kuasi kwake bado alikataa kurejea kwa mola wake kuomba toba na msamaha. Alishaamua kama mbwai na iwe mbwai. Hapo ndipo MUNGU alipoamua kumlaani Iblis na akafukuzwa kutoka katika kundi la malaika. Iblis aliipokea laana ile ila alikuwa na ombi moja tu kwa Mungu. Mungu akamruhusu aombe anachokitaka ndio akaomba kuwa apewe uhai mrefu mpk mwisho wa dunia hii yaani awe miongoni mwa viumbe vitakavyokufa mwisho.

Mungu alimkubalia , na baada ya ombi lake kupitishwa kwa hasira akasema kwa kuwa Adam ndio amesababisha Mungu kumlaani basi atahakikisha kuwa anavikalia mbele,nyuma,kushoto na kulia vizazi vya adam ili visiielekee njia ya Mungu, ili mwisho wa siku apate watu wengi wa kuingia nao motoni.

Mungu akamjibu palepale kuwa kwa hakika Iblis hana uwezo wa kupoyosha waja wake isipokuwa kwa yule atakaeamua kumfuata.Na kwa hakika ataijaza jahannam kwa iblis na wale wote watakaomfuata.

Yote haya yanatokea huko mbinguni hakuna kiumbe chochote kilichowahi kumuona Mungu ana kwa ana. Sio Adam,sio malaika wala sio huyo Iblis .Walikuwa wakipokea tu sauti ila hakuna aliyemuona Mungu toka ulimwengu unaumbwa mpk pale utakapoisha.

Mungu atakuja kujidhihirisha kwa waja wake watakaoingia peponi tu ndio watapata kumuona. Na hakuna zawadi kubwa mwanadamu atawahi kuipata kama nafasi ya kumuona Mola wake. Mungu atujaalie tuwe miongoni mwao ameen.
 
Chanzo cha Iblis , Adam na Hawa kutupwa duniani

Mara baada ya iblis kugoma hata kuomba msamaha na kutubu kwa Mola wake, ndipo akapokea laana. Hii ni majibu kwanini Mungu hakumsamehe Iblis. Jibu ni kuwa Iblis hakutaka kusamehewa. Yeye kuambiwa amsujudie Adam aliona kuwa ni udhalili uliopindukia mipaka na mpaka kesho bado anajiona kuwa yeye ni bora kutokana na kuumbwa kwa Moto.

Makazi ya Adam yakawa ni katika bustani ya Eden,na baadae akaumbiwa mke kutokana na ubavu wake wa kushoto, bi Hawa.

Iblis nae alikuwa akiishi huko huko juu na pia alikuwa akipata nafasi ya kuzungukia bustani hiyo ya Eden.

Masharti aliyopewa Adam na mkewe ni kuwa wale kila kotu kizuri ndani ya bustani hiyo ila wasile tunda la mti mmoja tu. Waliishi hivyo ila iblis kutokana na kujua kuwa ni ngumu kumuingia Adam na kumshawishi ,akaamua amuendee mkewe na kujifanya kuwa ni mshauri mzuri kwao, kwa kumuuliza kuwa anajua kwanini wameambiwa kuws wasile tunda la mti ule? Hawa hakufahamu chochote ndipo Iblis akamwambia kuwa mmekatazwa wewe na mumeo msile tunda lile kwasababu mkila tu mtakuwa kama malaika na mtaishi milele hamtakufa.

Kwakuwa eden kulikuwa na starehe na raha tele, hakuna nafsi ya mwanadamu ingependa kusikia kuwa ipo siku itakufa na kuziacha raha na starehe za bustani hiyo, ndipo bibie Hawa akamfata mumewe na kuanza kumshawishi kuwa wale tunda hilo ili wasife. Adam kwa udhaifu wake akamskiliza mkewe na kwa pamoja wakala tunda lile ,ghafla mavazi mazuri waliyopewa na Mungu yaliwatoka na wakajikuta kuwa wapo utupu, hivyo wakawa wanatafuta majani ya miti humo bustanini ili wajihifadhi miili yao.Kwa aibu Adam akawa amejificha huku akijuta kwanini amekula tunda lile waliloshauriwa na Iblis. Iblis kwa upande wake alifurahi mno na kuanza kumuuliza Mungu kuwa yupo wapi kiumbe uliyemfanya bora kuliko mimi ona sasa amekuasi kwa kula tunda ulilomkataza asilile?

Mungu akamuita Adam aliyekuwa amejificha kwenye miti, na kumuuliza kwanini amefanya yale aliyomkataza, ADAM hakuwa na la kujibu bali alidondoka chini na kuomba msamaha na kutubu kwa Mola wake. Kutokana na kujishusha kwao yeye na mkewe, Mungu aliwakubalia toba zao.

Ila sasa kile kipaumbele cha kuishi bustanini kikawa kimeishia pale na wakaambiwa kuwa watateremshwa duniani huko ndipo watakuta kila kitu chao, wataishi huko na muongozo wa Mungu utawafata huko na mwisho watakufa na kurejea kwa Mola wao tena. Na wakaambiwa kuwa hakika Iblis ni adui kwenu na nyinyi mfanyeni kuwa ni adui,msimsikilize kwa lolote atakalowaambia ama kuwashauri.

Wote watatu kuanzia hapo wakashushwa duniani, adam,hawa na iblis.
 
Points to note

Iblis ameumbwa kwa moto.

Malaika wameumbwa kwa nuru.
Iblis sio malaika.

Iblis ni jini kwani majini asili yao ni kutokana na Moto.

Mungu hakumsamehe Iblis kwa kuwa iblis hakutaka kusamehewa,alikuwa jeuri na kiburi.

Adam alisamehewa baada ya kuomba msamaha na kutubu dhambi pale bustanini.

Kusudi la kuletwa huku duniani ni kuwa Mungu amefanya maisha haya kuwa ni mtihani kwetu ili aangalie ni nani mwenye vitendo vyema.

Maisha ya binadamu bila ya kuwepo Iblis yangekuwa hayana changamoto, kumbuka kuwa hapa duniani ni sawa na chumba cha mtihani.Mtihani wenyewe ni ambao Mungu kashatupa majibu ya kuufaulu ni jukumu letu sisi kuyanakili majibu hayo ili tusifeli.

Iblis ni kiumbe mdogo sana kulinganisha na malaika, Mungu hana ushirika na iblis ktk kuamua mambo yake.Akitaka jambo husema kuwa na lina kuwa.
 
Mambo yalianza kuharibika pale bustanini ambapo badala ya Mungu kutoa msamaha kwa adam na ev. Yeye akawamiminia laana.

Cha kwanza aliweka uadui kati ya mwanadamu na shetani

Pili akamwambia binadamu atakula kwa jasho atazaa kwa uchungu na hakika atakufa.

angesamehe kama mwanae anavyo tushauri tusamehe saba mara sabini Tusimge fika huku.
Akili mtu wangu [emoji16][emoji16]

Mungu na so called dini ni mchongo .. hivi vitu hakuna
 
alafu siku ya kiama unapigwa moto na uyo ibilisi,wengine hatumjui hata anafananaje.kwa kweli hao kina adam angemalizana nao uko eden sio kutuuzia kesi yao ambao hatukuepo
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Mungu nimchongo hayupo
 
Anguko la mwanadamu halikuletwa na mway Snadamu kwa mujibu wa Bibles.biblia inasema wazi kua nyokaaaa alikuwa mwerevu kuliko wanyama wrote..(mwanzo3:1.....Nyoka alikua anaongea kumbe.ni wapi shetani alimdanganya hawa kula tunda?shetani story yake sijui ilianzia wapi ila anguko la mwanadamu nikudanganywa na Nyoka sio shetani
 
Aliyetufundisha kuhusu yesu na shetani ndio huyo huyo aliyefundisha jua linazunguka dunia na binadamu tuliamini hivyo for thousands of years mpaka scientist walipokuja prove sio kweli ni dunia ndio inazunguka jua, mambo ya imani ni magumu kidogo
 
Mkuu mwenye makosa ni Adamu na Mkewe! Kwa sababu waliikata Amri ya Mungu na kuamua kumsikiliza Shetani! Kumbuka hapo walikuwa hawana shida yo yote,walikuwa wanaponda raha za peponi,walikuwa hawatafuti chakula,nguo au cho chote yaani walikuwa wanakula bure na kulala bure LAKINI wakaamua kumskiliza Shetani na wala Shetani hakutumia nguvu yo yote kuwalazimisha wamwasi Mungu.
 
Ibilisi ni kama ngano za alfu lela ulela tuu, hata babu yangu alikuwa nazo nyingi tuu na moja naikumbuka ilikuwa kuna kilima kimoja ukikipita lazima uiname mara tatu usipofanya hivyo unaweza leta mikosi kwenye ukoo
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Kwamba wangemalizana wenyewe!
wanatuletea likitu hatulioni lina miguvu lina ushawishi na lina mali zote za huu ulimwengu.
Kweli sisi ni nani tuliweze?
Ila kweli ni uonevu
 
Sasa kumbuka hao ni malaika ambao daily wanashinda na Mungu lakini bado waliungana na shetani

Vipi Mungu ashangazwe na sisi binadamu kushawishika na shetani katika mazingira ambayo kuna njaa, shida, magonjwa, vita nk hata huyo Mungu hatujawahi kumuona?

Kuna point nimeielewa apo.
 
Kitendo cha Mungu kumtupa Ibilisi duniani ni kitendo cha uonevu mkubwa sana kwa binadamu.

Ibilisi sio levo za binadamu ni levo ya Mungu maana yake Mungu yeye angekomaa naye Ibilisi hukohuko mbinguni mpaka kieleweke. Kutuletea Ibilisi huku duniani ni kutuonea tu maana hatuna uwezo wowote wa kupambana naye.

Kama Ibilisi aliweza kupigana vita kuu mbinguni akiwa na malaika wake sasa binadamu ataweza kweli kupambana na kiumbe kama hiki?

Kiumbe ambacho kiliweza kupambana na malaika wa Mungu na kikafanikiwa kuwashawishi baadhi ya malaika kwenye vita kuu mbinguni na wakaasi sasa wewe binadamu utaweza kweli kupambana na Ibilisi?

Kama mbinguni tu Ibilisi alisumbua sana ambako ndiyo kuna Mungu na malaika huku duniani tutamuweza kweli?

Kama Ibilisi anauwezo wa kuingilia mipango ya Mungu na kuiharibu kama ule wa bustani ya Edeni na Mungu hamfanyi chochote anaishia tu kuwapa adhabu zisizo na maana yoyote Adam na Hawa. Hiki kiumbe sisi binadamu tutakiweza kweli?

Ilifikia hatua Mungu mwenyewe aliamua kumtoa kafara mwanaye wa pekee( Yesu) ili aweze kupambana na Ibilisi ila mission ikabuma. Sisi binadamu tutaweza kweli kupambana na Ibilisi?

Hivi unajua kama Ibilisi anaongea na Mungu moja kwa moja? Maana yake Mungu na Ibilisi huwa wanaonana. Unajua mazungumzo ya Mungu na Ibilisi kuhusu Ayubu? Sasa sisi binadamu tutaweza kweli kupambana na Ibilisi anayeweza kuongea na Mungu moja kwa moja?

Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani?
Hapa binadamu tumeonewa sana.

Jukumu la kupambana na Ibilisi ni jukumu la Mungu mwenyewe na sio la binadamu hivyo Mungu amtoe Ibilisi duniani na akaishi naye mbinguni sisi huku hatumuwezi.

Ndio maana imekuwa ni kawaida tu kumkuta mtu ni mfia dini haswa ila ni mzinifu,muongo,muuaji,mchawi,tapeli,mwizi, mnafiki n.k.

Nani kakudanganya kuna binadamu anaweza kupambana na Ibilisi?
Mwapotea kwasababu hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
 
Chanzo cha Iblis , Adam na Hawa kutupwa duniani

Mara baada ya iblis kugoma hata kuomba msamaha na kutubu kwa Mola wake, ndipo akapokea laana. Hii ni majibu kwanini Mungu hakumsamehe Iblis. Jibu ni kuwa Iblis hakutaka kusamehewa. Yeye kuambiwa amsujudie Adam aliona kuwa ni udhalili uliopindukia mipaka na mpaka kesho bado anajiona kuwa yeye ni bora kutokana na kuumbwa kwa Moto.

Makazi ya Adam yakawa ni katika bustani ya Eden,na baadae akaumbiwa mke kutokana na ubavu wake wa kushoto, bi Hawa.

Iblis nae alikuwa akiishi huko huko juu na pia alikuwa akipata nafasi ya kuzungukia bustani hiyo ya Eden.

Masharti aliyopewa Adam na mkewe ni kuwa wale kila kotu kizuri ndani ya bustani hiyo ila wasile tunda la mti mmoja tu. Waliishi hivyo ila iblis kutokana na kujua kuwa ni ngumu kumuingia Adam na kumshawishi ,akaamua amuendee mkewe na kujifanya kuwa ni mshauri mzuri kwao, kwa kumuuliza kuwa anajua kwanini wameambiwa kuws wasile tunda la mti ule? Hawa hakufahamu chochote ndipo Iblis akamwambia kuwa mmekatazwa wewe na mumeo msile tunda lile kwasababu mkila tu mtakuwa kama malaika na mtaishi milele hamtakufa.

Kwakuwa eden kulikuwa na starehe na raha tele, hakuna nafsi ya mwanadamu ingependa kusikia kuwa ipo siku itakufa na kuziacha raha na starehe za bustani hiyo, ndipo bibie Hawa akamfata mumewe na kuanza kumshawishi kuwa wale tunda hilo ili wasife. Adam kwa udhaifu wake akamskiliza mkewe na kwa pamoja wakala tunda lile ,ghafla mavazi mazuri waliyopewa na Mungu yaliwatoka na wakajikuta kuwa wapo utupu, hivyo wakawa wanatafuta majani ya miti humo bustanini ili wajihifadhi miili yao.Kwa aibu Adam akawa amejificha huku akijuta kwanini amekula tunda lile waliloshauriwa na Iblis. Iblis kwa upande wake alifurahi mno na kuanza kumuuliza Mungu kuwa yupo wapi kiumbe uliyemfanya bora kuliko mimi ona sasa amekuasi kwa kula tunda ulilomkataza asilile?

Mungu akamuita Adam aliyekuwa amejificha kwenye miti, na kumuuliza kwanini amefanya yale aliyomkataza, ADAM hakuwa na la kujibu bali alidondoka chini na kuomba msamaha na kutubu kwa Mola wake. Kutokana na kujishusha kwao yeye na mkewe, Mungu aliwakubalia toba zao.

Ila sasa kile kipaumbele cha kuishi bustanini kikawa kimeishia pale na wakaambiwa kuwa watateremshwa duniani huko ndipo watakuta kila kitu chao, wataishi huko na muongozo wa Mungu utawafata huko na mwisho watakufa na kurejea kwa Mola wao tena. Na wakaambiwa kuwa hakika Iblis ni adui kwenu na nyinyi mfanyeni kuwa ni adui,msimsikilize kwa lolote atakalowaambia ama kuwashauri.

Wote watatu kuanzia hapo wakashushwa duniani, adam,hawa na iblis.
Kwani binadamu anasujudiwa?
 
Kwani binadamu anasujudiwa?
Sijida ya heshima!! Mungu alitaka malaika pamoja na iblis wampe heshima Adam...Malaika licha ya kuwa wameumbwa kwa material bora zaidi ambayo ni NURU walitii ila Iblis alikataa katakata kutokana na kuona ameumbwa kwa Moto na Adam ameumbwa kwa udongo
 
Kwani nuru ni nini
 
Haya mambo ukiyafikiria sana, utakufuru tu.

Ndo maana hamna kuuliza maswali kanisani.

Dini na 'ujuha' wa kujifanya vina mahusiano ya kindakindaki.

Yaani unaamua tu kwamba hapa nameza kama vilivyo tu. Basi.

Maana la sivyo moto unaningoja.
Pengine na huo moto haupo!
 
Back
Top Bottom