Hivi Mungu amemshindwa shetani kabisa? Basi shetani tumpe maua yake

Hivi Mungu amemshindwa shetani kabisa? Basi shetani tumpe maua yake

Haiwezekani mbinguni au katika ulimwengu tusiojua wanaishi viumbe wawili wanaoogopana. Sasa tutajua nani mwenye nguvu?

Inasemekana shetani ni mbaya kama tulivyokalilishwa na Mungu lakini inakuwaje Mungu ashindwe kumuangamiza kama kweli Mungu hashindwi chochote?

Hata wachungaji/mapadre wenyewe hawataki shetani aangamizwe mana watakosa cha kutuhubiri ili kupiga hela. Kwa maana nyingine shetani kawapa ulaji wachungaji. Siku akitoweka tu mapdre/ maskofu / wachungaji watakufa njaa maana watakosa cha kutudanganya.
Eti wanasema Bado mda sijui utafika lini 😆😆
 
Zaburi 14:1a

"Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu"

BORA kua mjinga kulikua kua mpumbavu , upumbavu ni hali HATARI sana NDANI ya MTU


Ujinga ni kukosa taarifa SAHIHI, Kwaiyo ni rahisi Sana kumuelimisha mjinga lakini mpumbavu ni MUNGU mwenyewe ndie awezae KUMBADILISHA
Huyo Mungu mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea kwa vile Hayupo kujiongelea mwenyewe wala hawezi kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Hakuna uthibitisho wowote ule uliothibitisha kwamba energy haikuwepo kisha ikawepo.

Kwa hiyo kinachofahamika na kuthibitishika ni kwamba energy ilikuwepo, tumeikuta ipo na itaendelea kuwepo.

Mpaka pale kutakapokuwa na uthibitisho kwamba energy haikuwepo, ndipo itakubalika hivyo.

Ila hakuna anaye jua energy ilianzaje
Wewe na Kiranga ni kama Thomaso . Mwamba Thomaso bila uthibitisho wa macho ya nyama hawezi kukubali chochote . Kwa bahati mbaya mtu akifa macho ya nyama yanakuwa hayana msaada kwake , labda siku moja mtakuja kumuona Mungu kwa macho ya roho hata katika njozi za usiku .
 
Tumia lugha ya picha na kuongea kwa tafsida, mti wa katikati ni ule mti na tunda ni lile tunda la kumegwa, kula tunda ndio kumegwa.

Shetani baada ya kuingia bustanini kama nyoka, akajigeuza mtu, akamfundisha Eva jinsi ya kumega tunda, akamega.

P
Hee Pascal, ni kweli haya?

Sasa ngoja nikupe food for thought. Amri ya "kutomega" tunda kama unavyokuita wewe, kulitolewa na Mungu kwa Adamu kabla Eva hajaumbwa. Sasa kama ni hivyo, Mungu alikuwa akimwambia Adam "asimege" tunda na nani wakati Eva hajaumbwa bado?

Mti wa "katikati" pia ulikuwapo kabla ya Adamu hajaumbwa, na Adamu alipoumbwa, akiwa peke yake ndipo akaambiwa asile toka mti huo. Sasa basi uli refer kitu gani kama ulishakuwapo kabla ya Adamu kuumbwa?
 
Wewe na Kiranga ni kama Thomaso . Mwamba Thomaso bila uthibitisho wa macho ya nyama hawezi kukubali chochote . Kwa bahati mbaya mtu akifa macho ya nyama yanakuwa hayana msaada kwake , labda siku moja mtakuja kumuona Mungu kwa macho ya roho hata katika njozi za usiku .
Kwa nini uhitaji kuamini Mungu yupo kwa imani, Badala ya kujua Mungu yupo kwa uthibitisho kabisa?

Huyo Mungu kama yupo anacho jifichia asijulikane yupo ni nini?
 
Kwa nini uhitaji kuamini Mungu yupo kwa imani, Badala ya kujua Mungu yupo kwa uthibitisho kabisa?

Huyo Mungu kama yupo anacho jifichia asijulikane yupo ni nini?
Mungu anajidhihirisha katika vitu alivyoviumba . Ila wewe unataka umuone Mungu mwenyewe aliyeviumba hivyo vitu yaani unataka ujue Mungu anaonekanaje kwa umbo na sura !
 
Mungu anajidhihirisha katika vitu alivyoviumba .
Ulijuaje na unathibitishaje Mungu huyo aliumba vitu?

Au ni mawazo yako na hadithi ulizo simuliwa tu?
Ila wewe unataka umuone Mungu mwenyewe aliyeviumba hivyo vitu yaani unataka ujue Mungu anaonekanaje kwa umbo na sura !
Wewe kama hukuwahi kumuona huyo Mungu akiumba hivi vitu, Utasemaje na kuhitimisha kwamba Mungu huyo ndio muumbaji?

Ni nani aliwahi kumuona huyo Mungu akiumba hivi vitu?

Na alijuaje ni Mungu?
 
Ulijuaje na unathibitishaje Mungu huyo aliumba vitu?

Au ni mawazo yako na hadithi ulizo simuliwa tu?

Wewe kama hukuwahi kumuona huyo Mungu akiumba hivi vitu, Utasemaje na kuhitimisha kwamba Mungu huyo ndio muumbaji?

Ni nani aliwahi kumuona huyo Mungu akiumba hivi vitu?

Na alijuaje ni Mungu?
Walifunuliwa na kupewa taarifa na malaika wa Mungu . Mimi mwenyewe niliwahi kuletewa taarifa na malaika wa Mungu kuhusu jambo langu. Malaika wa Mungu ndio wanaotawala energy na nyota zote kwa kufuata order wanazopewa na Mungu.
 
Walifunuliwa na kupewa taarifa na malaika wa Mungu . Mimi mwenyewe niliwahi kuletewa taarifa na malaika wa Mungu kuhusu jambo langu.
Unathibitishaje ni malaika na sio hallucinations?

Bila shaka ulipata hallucinations halafu unasema ni malaika wa Mungu...😄

Ninyi watu mnachekesha sana.
 
Wabongo wengi sana hamna imani na Muumba ndio maana aya maswali yenu ya kukufuru uku Jf ni mengi mno.

Unakuta mtu anamkufuru muumba wake kwa sababu pumzi za uzima aliyonao inamhadaa anafanya vile anavyojiskia.
Acha vitisho kijana jikite kwenye mada. Kwanini Mungu asimuue shetani ili hizi drama zao ziishe?
 
Unathibitishaje ni malaika na sio hallucinations?

Bila shaka ulipata hallucinations halafu unasema ni malaika wa Mungu...😄

Ninyi watu mnachekesha sana.
Hizo hallucinations ni hisia zako ndo zinakutuma hivyo . Ila ujumbe niliopewa niliufanyia kazi na nikapata matokeo chanya katika dunia halisia . Namuamini Mungu sana mpaka leo .
 
Endeleeni kumjadili Mungu ila mimi bado nawaza hizi namba za Tesla( 3, 6, 9) kuna siri gani? Kingine nilichogundua hii dunia ina formula zake ngoja niendelee kutafakari
 
Mungu ni chanzo cha kila kitu. Nguvu ya nuru na giza tunavuna kwake. Samael maana yake ni sumu ya Mungu. Huyu ndie mjaribu kwa watu wote waelekeao binguni, ukisikia usitutie katika vishawishi anzungumziwa Samael ambaye upande wa giza wanamjua kama mume wa lilith. Hivyo nguvu ya shetani inavunwa kutoka kwa Mungu. Ambapo kila utakaachopanda ndicho utakachovuna, (karma) hivyo shetani ndiye mjaribu ambaye huja kitujaribu wana wa Mungu hivyo hana nguvu kumzidi Mungu
 
Hizo hallucinations ni hisia zako ndo zinakutuma hivyo
Pia huyo Mungu ni hisia zako ndo zinakutuma hivyo.
. Ila ujumbe niliopewa niliufanyia kazi na nikapata matokeo chanya katika dunia halisia . Namuamini Mungu sana mpaka leo .
Wewe kumuamini Mungu sio shida, kwa vile ni hisia zako tu ndizo zinakutuma hivyo.

Huyo Mungu hawezi kujidhihirisha mwenyewe yupo wala hawezi kuja hapa kujitetea yupo.

Ndio maana ninyi mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea Mungu asiyekuwepo.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Jiulize kwanini mwili ukilala usingizi , kuna MAISHA yanaendelea

MTU ni Roho yupo ndani ya mwili anayo nafsi hai, mwili kulala usingizi ni kitendo cha kuhama kutoka ulimwengu wa nyama na damu na kuingia katika ulimwengu wa Roho ambao obviously ndipo MUNGU na shetani huweza kujidhihilisha kwa mtu B'se MUNGU ni roho na shetani vivyo hivyo ni Roho kamwe hatuwezi kuwaona kwa macho ya nyama na DAMU na hata macho ya Rohoni ila kuna ishara utaziona na ukiwa na NENO la MUNGU utafahamu usauti au lugha yake kwa NENO lake lililopo moyoni

Kwa hiyo mechanism ya kushift kutoka katika ulimwengu wa mwilini na kuingia katika ulimwengu wa Roho ni dhahiri MUNGU yupo, alikuwepo na atakuwepo milele
 
Hakuna mungu wala shetani, enjoy maisha kula nyama ukifa umekufa, dunia haina huruma.
 
Back
Top Bottom