Hivi Mungu amemshindwa shetani kabisa? Basi shetani tumpe maua yake

MUNGU kaumba dunia tupu, akumba mfumo wa kuyawezesha maisha kuwepo. Uovu ni wa binadamu.
Uwezo wa kuwa muovu, Binadamu aliupata wapi?

Mungu mjuzi wa vyote, Hakujua kwamba binadamu atakuja kuwa muovu amdhibiti na kumzuia mapema?

Dunia lazima ifanye kazi kwa mfumo. Umetengeneza gari, ili litembee si ni lazima vyuma visagane?

Freewill tunayo sababu baada ya kuzaliwa nature ilitupa akili ya namna ya kukabiliana na majanga.
Kwa nini majanga hayo yawepo?

Mungu huyo kwa nini aumbe Dunia yenye majanga ilhali uwezo wa kuumba dunia isiyo na majanga alikua nao?
Baharini kuna dhoruba ila binadamu tunajenga nyumba zinazoelea na tunaifuatuata dhoruba.
Nakwambia hivi hiyo free will haipo.

Concept ya free will ni stori uchwara uchwara tu za kuhalalisha Mungu asiyekuwepo.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kwanini shetani anatakiwa kuuwawa boss? Binafsi naona uwepo wa shetani ni mpango wa MUNGU tena aliujua wakati wa uumbaji na akauruhusu.
Basi huyo MUNGU ni muovu, mkatili na mjinga sana.

Kama yeye mwenyewe aliruhusu uwepo wa huyo shetani, Halafu ninyi kutwa kucha mnasali kumuomba huyo Mungu awaepushe na huyo Shetani basi mtakuwa vichwa maji na wapumbavu sana.
 
Kwanza tumia capital letters kutaja jina la Mungu.

Mwanzo wa Mungu pia ndio mwanzo wa shetani, ambaye mwanzo alikuwa malaika, ndie alikuwa malaika mkuu 2nd in command baada ya Mungu.

Mungu ana nguvu na shetani ana nguvu, ila nguvu za Mungu ni kubwa zaidi ya nguvu za shetani kwa mambo mawili tuu, creation of life, and taking back the life, lakini vitu vingine vyote, everything God can do, the devil can do!.

Shetani alipoasi alifukuzwa tuu mbinguni lakini alibaki na nguvu zake zote. God ananguvu kuliko shetani lakini hawezi kumuangamiza shetani!.

Shetani ni mzuri sana kwa kuji disguise hivyo alipoingia bustani ya Aden kum tempt Eva, alijigeuza nyoka akapenya bustanini, kule akajigeuza mtu, ndipo akamshawishi Eva kula lile tunda, kwa kumuonyesha kwa practical kabisa jinsi tunda linavyochumwa, linavyo megwa, akammegea Eva, Eva na shetani wakala tunda.

Baada ya Eva kuuonja utamu wa tunda, akampelekea Adamu tunda, akamfundisha tunda linavyomegwa. Adam akamkatatalia kula tunda lililokatazwa na Mungu. Eva akamlazinisha, Adamu akakubali kumega tunda, na kutokana na utamu wa tunda, Adam na Eva wakaishia zao uzingizini!.

Shetani akasepa zake.

Walipoamka, wakaanza kuona noma!, ndipo Mungu akamuadhibu Eva, atazaa kwa uchungu kufidia utamu wa tunda, na hiyo dhambi ya kumega tunda, ndiyo dhambi ya asili, ili binadamu azaliwe, lazima kwanza dhambi ya asili itendwe ndipo mi.ba itunge!. Kuna binadamu mmoja tuu aliyekingiwa dhambi ya asili, ni Bikira Maria, alipata mi.ba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Hata sasa Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.

P
Bwn Pasco nimekuelewa ila kuna sehemu unatuacha. Hv hapo kwenye kumega tunda unamaanisha Adamu alimpiga miti Eva!?

Kama hivyo ndivyo basi ina maana Eva alianza kupigwa miti na nyoka

Daah dini ngumu wacha nikale zangu beer
 
Watu walianza kuchipua kama mimea au walianzaje ??
Watu hawakuanza.

Hakuna wakati ambao kulikuwa hakuna watu, kisha watu wakaanza kuwepo from nothing.

Watu walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo.

Sisi ni Energy, We cannot be created or destroyed but we transform from one form to another.
 
Uwezo wa kuwa muovu, Binadamu aliupata wapi?

Mungu mjuzi wa vyote, Hakujua kwamba binadamu atakuja kuwa muovu amdhibiti na kumzuia mapema?
Kwanini unampa hili jukumu MUNGU? Binadamu anazaliwa akiwa mwema, tunawaita malaika, anapokomaa anauchagua uovu ilihali anaweza kuuchagua wema, kwanini hii lawama apewe MUNGU?
Kwa nini majanga hayo yawepo?

Mungu huyo kwa nini aumbe Dunia yenye majanga ilhali uwezo wa kuumba dunia isiyo na majanga alikua nao?
Hivi unajua kuna viumbe ili viishi sharti ipite dhoruba? Tatizo binadamu tunataka ulimwengu uwe sehemu ya binadamu na si binadamu sehemu ya ulimwengu.

Nimekupa mfano mwepesi boss, Unaweza kuunda gari linalotembea ila hakuna msuguano wa vyuma? Yaani engine ifanye kazi ila kwenye chamber zake pasitokee milipuko na joto kali inayochakaza valve.

Hiyo dunia isiyo na upepo mkali, jua kali, matetemeko itaruhusu uwepo wa maisha ya viumbe? Au ili maisha yawepo sharti mfumo uruhusu uwepo wa hivi vitu?
Nakwambia hivi hiyo free will haipo.

Concept ya free will ni stori uchwara uchwara tu za kuhalalisha Mungu asiyekuwepo.
Suala la Freewill nimeshaona unalifananisha na chaos. Yaani unataka chaos ndo iwe free will. Si haki kwa wengine. Mfumo uliopo freewill ipo. Freewill bila ukomo ni chaos.
 
Yakobo 1: 13-15
Mtu ajaribiwapo asiseme, ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjarubu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti
 
Kwanini unampa hili jukumu MUNGU? Binadamu anazaliwa akiwa mwema, tunawaita malaika, anapokomaa anauchagua uovu ilihali anaweza kuuchagua wema, kwanini hii lawama apewe MUNGU?
Kwa sababu ninyi mnadai tuliumbwa na huyo Mungu mjuzi wa vyote na mwenye uwezo wa yote.

Kama Mungu huyo ni mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Je Hakujua na ku notice kwamba binadamu ataweza kuwa muovu amdhibiti na kumzuia mapema?
Hivi unajua kuna viumbe ili viishi sharti ipite dhoruba? Tatizo binadamu tunataka ulimwengu uwe sehemu ya binadamu na si binadamu sehemu ya ulimwengu.
Sisi ni sehemu ya ulimwengu.

Ndio maana binadamu hufa naku uacha ulimwengu.

Ulimwengu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo.
Nimekupa mfano mwepesi boss, Unaweza kuunda gari linalotembea ila hakuna msuguano wa vyuma? Yaani engine ifanye kazi ila kwenye chamber zake pasitokee milipuko na joto kali inayochakaza valve.
Kwa Mungu mnayedai ni muweza wa vyote, Hakutakiwi kuwepo chochote kinacho mshinda au kitakacho mshinda.

Sisi binadamu hatuwezi vyote ndio maana bado tunapambana kujua vitu vyote.

Ila kwa Mungu huyo muweza wa vyote, Kushindwa kuumba Dunia isiyo na matatizo wala uovu ni makusudi kabisa.

Otherwise, Huyo Mungu na yeye hawezi yote kama sisi.

Una elewa lakini?
Hiyo dunia isiyo na upepo mkali, jua kali, matetemeko itaruhusu uwepo wa maisha ya viumbe? Au ili maisha yawepo sharti mfumo uruhusu uwepo wa hivi vitu?
Kwa Mungu muweza wa vyote, Lazima angekuwa na mifumo mingi ya kuendesha dunia na hatakiwi kuwa limited na mfumo mmoja tu wa kuendesha maisha.

Maana yeye si ni Mungu muweza wa vyote?

Anaweza hata kuumba dunia tukaelea angani na kulala hewani.

Kwa nini unadhani mfumo huu huu mmoja ndio Mungu alikuwa lazima autumie?
Suala la Freewill nimeshaona unalifananisha na chaos. Yaani unataka chaos ndo iwe free will. Si haki kwa wengine. Mfumo uliopo freewill ipo. Freewill bila ukomo ni chaos.
Nakwambia tena hivi, Free will Haipo.
 
Kwa sababu ninyi mnadai tuliumbwa na huyo Mungu mjuzi wa vyote na mwenye uwezo wa yote.

Kama Mungu huyo ni mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Je Hakujua na ku notice kwamba binadamu ataweza kuwa muovu amdhibiti na kumzuia mapema?
Kwanini amzuie na amdhibiti? Kwani ni kazi ya MUNGU kuzuia ufisadi? Wizi? Si mambo ya binadamu hayo?
Sisi ni sehemu ya ulimwengu.

Ndio maana binadamu hufa naku uacha ulimwengu.

Ulimwengu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo.

Kwa Mungu mnayedai ni muweza wa vyote, Hakutakiwi kuwepo chochote kinacho mshinda au kitakacho mshinda.
Sasa tatizo lipo wapi? Unataka kuishi milele kwa raha ndo uuone ukuu wa MUNGU? Ukuu wa MUNGU unapimwa kwa mfumo perfect kwa viumbe wote si mfumo perfect kwa mwanadamu, Kama binadamu ni sehemu ya ulimwengu heshimu na kaa sehemu yako ukihama mfumo unakutema. Huo ni mfumo perfect kabisa unaothibitisha ukuu wa MUNGU.
Sisi binadamu hatuwezi vyote ndio maana bado tunapambana kujua vitu vyote.

Ila kwa Mungu huyo muweza wa vyote, Kushindwa kuumba Dunia isiyo na matatizo wala uovu ni makusudi kabisa.
Elewa maana ya mfumo. Kwa ninavyoiona dunia ni lazima iwe kama ilivyo ili iwepo na iwe fair kwa viumbe vyake, kuanzia binadamu mpaka bakteria.
Otherwise, Huyo Mungu na yeye hawezi yote kama sisi.

Una elewa lakini?
Kuweza yote maana yake ni nini? Kwamba ili awe muweza yote ni lazima wewe upate yote mazuri?

Mkuu, Ulimwengu ni mfumo, unaofanya maisha yaendelee kuwepo,

Mfano wewe unaweza kuweka chakula kwenye sinki la choo kichafu cha uma na ukakila ila hufanyi hivyo sababu unajua ukifanya hivyo kwa muda mfumo hautakuruhusu kuendelea na maisha bila kupata magonjwa.

Same case, kila kitu kilichopo kipo ili mfumo ufanye kazi, sasa wewe kwanini unataka kisiwepo ili kuthibitisha aliyeviweka ni muweza wa yote?
Kwa Mungu muweza wa vyote, Lazima angekuwa na mifumo mingi ya kuendesha dunia na hatakiwi kuwa limited na mfumo mmoja tu wa kuendesha maisha.

Maana yeye si ni Mungu muweza wa vyote?
Tunarudi pale pale, huu mfumo ni perfect kwa viumbe vyote. Kwanini unataka uwe perfect kwako ndo awe muweza wa vyote?
Anaweza hata kuumba dunia tukaelea angani na kulala hewani.

Kwa nini unadhani mfumo huu huu mmoja ndio Mungu alikuwa lazima autumie?
Ukikaa angani radi, msugano, miale ya jua n.k iondolewe ili awe muweza wa vyote au ibaki? Yaani naona kama unataka ulimwengu uwe sehemu yako ili kuthibitisha ukuu wa MUNGU, kwanini? Wewe ni sehemu ya ulimwengu.
Nakwambia tena hivi, Free will Haipo.
Kwa unavyotaka wewe haiwezekani, ni chaos.
 
Kwanini amzuie na amdhibiti? Kwani ni kazi ya MUNGU kuzuia ufisadi? Wizi? Si mambo ya binadamu hayo?
Kama ni mambo ya kibinadamu, wewe ulijuaje na unathibitishaje kuna mambo ya Mungu?

Huoni kwamba unafosi mawazo yako uchwara yasiyo na mantiki wala uthibitisho wowote ule?
Sasa tatizo lipo wapi? Unataka kuishi milele kwa raha ndo uuone ukuu wa MUNGU? Ukuu wa MUNGU unapimwa kwa mfumo perfect kwa viumbe wote si mfumo perfect kwa mwanadamu, Kama binadamu ni sehemu ya ulimwengu heshimu na kaa sehemu yako ukihama mfumo unakutema. Huo ni mfumo perfect kabisa unaothibitisha ukuu wa MUNGU.
Ukuu wa Mungu ni nini?

Kwa nini sio ukuu wa ulimwengu?
Elewa maana ya mfumo. Kwa ninavyoiona dunia ni lazima iwe kama ilivyo ili iwepo na iwe fair kwa viumbe vyake, kuanzia binadamu mpaka bakteria.

Kuweza yote maana yake ni nini? Kwamba ili awe muweza yote ni lazima wewe upate yote mazuri?

Mkuu, Ulimwengu ni mfumo, unaofanya maisha yaendelee kuwepo,

Mfano wewe unaweza kuweka chakula kwenye sinki la choo kichafu cha uma na ukakila ila hufanyi hivyo sababu unajua ukifanya hivyo kwa muda mfumo hautakuruhusu kuendelea na maisha bila kupata magonjwa.

Same case, kila kitu kilichopo kipo ili mfumo ufanye kazi, sasa wewe kwanini unataka kisiwepo ili kuthibitisha aliyeviweka ni muweza wa yote?

Tunarudi pale pale, huu mfumo ni perfect kwa viumbe vyote. Kwanini unataka uwe perfect kwako ndo awe muweza wa vyote?

Ukikaa angani radi, msugano, miale ya jua n.k iondolewe ili awe muweza wa vyote au ibaki? Yaani naona kama unataka ulimwengu uwe sehemu yako ili kuthibitisha ukuu wa MUNGU, kwanini? Wewe ni sehemu ya ulimwengu.
Hakuna uhusiano wa huyo Mungu na ulimwengu.

Huyo Mungu ni dhana uchwara tu kuhalalisha mambo usiyo yaelewa.
Kwa unavyotaka wewe haiwezekani, ni chaos.
Hata wewe unavyo fosi huyo Mungu awe ndio muumbaji wa ulimwengu ni Chaos...

Hakuna ulazima wa uhusiano wa huyo Mungu na ulimwengu.
 
Neno Catholic ( Katoliki ) lina maanisha ulimwengu na wakatoliki wanaamini Mungu ndiye anauendesha ulimwengu.
Kuamini kitu fulani kina endesha ulimwengu ni jambo rahisi sana.

Ila kuthibitisha kitu hicho ndicho haswa kinacho endesha ulimwengu ni kazi ngumu sana.

Huyo Mungu ni dhana uchwara tu kuhalalisha mambo ambayo binadamu hana majibu nayo.

Hakuna ukweli wowote kwamba Mungu ni muendesha ulimwengu.

Ni dhana uchwara tu waliyo pumbazwa watu vizazi kwa vizazi.
 
Energy haiwezi kutengenezwa au kuharibiwa sawa. Lakini energy yenyewe ilitoka wapi ? Au Jua lilitokea kutoka wapi ?
 
Back
Top Bottom