Hivi Musa alikuwa Myahudi au Mwarabu?

Hivi Musa alikuwa Myahudi au Mwarabu?

Watu wa jumamosi walikufuru wakageuzwa manyani.
Siku ya Ijumaa ina surat nzima ndani ya Qur'an inaitwa surat Juma'ah
Biblia ni kitabu cha uzushi kisicho na mwenyewe.
Hebu nipe aya inayosema watu wa jumaamosi walikufuru wakageuzwa manyani,na nipe aya inayokwambia ijumaa ni siku takatifu au imewekwa rasmi kwa ajili ya ibada tu.Ukikosa hama huko
 
Hebu nipe aya inayosema watu wa jumaamosi walikufuru wakageuzwa manyani,na nipe aya inayokwambia ijumaa ni siku takatifu au imewekwa rasmi kwa ajili ya ibada tu.Ukikosa hama huko
'Na hakika mlikwisha yajua ya wale miongoni mwenu walio ivunja Sabato (siku ya mapumziko Jumamosi) na tukawaambia: kuweni manyani.
Surat Bagarah.

'Na yule ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani na amemkasirikia, na amewafanya miongoni mwao manyani.
Surat al Maa'idah.

'Ikiadhiniwa sala siku ya Ijumaa,
Surat al Jumu'ah
 
Sasa mbona unajihukumu mwenyewe!Walioivunja sabato wamelaaniwa wakawa manyani.Tena inaendelea kusema tumeiweka hiyo adhabu kuwa mawaidha kwa wacha Mungu(qur 2:65-66).Wewe kuivunja sabato ndo desturi yako.Sasa nani nyani hapo kwa akili yako?Nukuu aya inayosema baada ya kuhitilafiana kwa ajiri ya hiyo sabato(jumaamosi),Mungu akawapa ninyi siku ya ijumaa iwe ndo siku ya ibada.Usiniambie kuna sura inaitwa juma,nataka aya inayokuambia unepewa ijumaa kuwa ndiyo siku ya ibada badala ya sabato ya jumaamosi
 
Haaa...haaa...haaa !
Adhabu hiyo ni mawaidha kwa wacha Mungu. Hata sodoma na gomora ni mawaidha kwa wacha Mungu. Wasio wacha Mungu wanafunga ndoa na kuzitetea ndoa za jinsia moja !

Hayo maneno ya Ijumaa kuwa siku ya sala ni yangu !?
'Enyi mlio amini ! (Waislaam) ikiadhiniwa sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara (fungeni biashara). Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.

'Na itakapo kwisha sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.
Surat Jumu'ah 9-10.
 
Bro aya ipo katika surat.: inasema."Enyi mlioamin pindi inaponadiwa sala ya ijumaa fungen biashara zenu na muindee ibada,baada ya swala tawanyikeni katika ardhi kwemda kutafuta ridhiki" nenda kasome
!
 
Katika Uzi huu naona neno uislam linawapata tabu sana haswa waislam wakisema musa,Yesu au kuanzia adam walikuwa waislam wanadhan Muhhamad ndio kauleta uislam sabahu ndivyo wanavyofunzwa hivyo na kwasababu maandiko na mafundisho yao yamekuwa twisted ionenake uislam upo kwenye competiotion na Dini waliyoiamzisha wao kwa mashumuniya ya Ukristo..nasema wameianzisha kwasababu Yesu hajawahi kutamka yeye ni mkristo au kaleta dini inaitwa ukiristo bali ni dini ilianzishwa na kina Paulo miaka 300 baada ya Yesu kuondoka na baadae kuja muhamad ndio wakapandikiza hicho kitu ionekane kuna dini mbili

Sasa ngoja niwasaidie nawapa elimu itakayoruhusu akili yenu kufikiri.! Neno ISLAM lipo very technical linatokana na neno mzizi SALAM maana yake aman pili linatokana pia lina neno mzizi mwingine SILIM maana yake kujisalimisha....sasa kujisalimisha matakwa yako mbele ya Mungu kwa neno moja la kiarabu ndio inaitwa ISLAM na anaejisalimisha na kunyenyekea mbele ya Mungu anaitwa MUSLIM.

Sasa hebu turejee kwanini waislam wanasema mitume wote ni waislam ni kwa msingi kwa sababu mafundishi yao yote Noah,mussa,Jesus, ibrahim walifundisha kwa njia tofauti tofauti na walipewa vitabu tofauti tofauti lakin lengo lao ni moja wote walikuja kufundisha watu kujisalimisha mbele za Mungu na kumtegemea yeye ambapo kwa kitendo kiarabu kinaitwa ISLAM sio lazima wangekuwa wanasheria na taratibu za uislam wa leo kwasababu kila mtu ana zama.zake na mahitaji yake ila muhhmad amekuja kwa ajiliya kuhitimisha na hatakuja mtume mwingine baada yake ndio akaja na uislma huu wa leo na sio yeye aliyeuanzisha
 
Haaa...haaa...haaa !
Adhabu hiyo ni mawaidha kwa wacha Mungu. Hata sodoma na gomora ni mawaidha kwa wacha Mungu. Wasio wacha Mungu wanafunga ndoa na kuzitetea ndoa za jinsia moja !

Hayo maneno ya Ijumaa kuwa siku ya sala ni yangu !?
'Enyi mlio amini ! (Waislaam) ikiadhiniwa sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara (fungeni biashara). Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.

'Na itakapo kwisha sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.
Surat Jumu'ah 9-10.
Kumbe hiyo ilikuwa ni siku ya biashara.Haioneshi kuwa ni siku iliyowekwa maalum kwa ajr ya ibada tofauti na ilivyo jumaamosi.Hiyo ni siku kama zilivyo zngne,na ndio maana mnasali kila siku mara tano.Lkn jumaamosi ilivyotamkwa kwenye quran na biblia ni tofauti kabisa.Ni siku ya ibada tu na sio ya kufanya kazi.Lkn ninyi mmetia tia hila,mpaka ikawa ni siku ya kazi.Soma qr 4:154 na ufafanuzi wake kipengele C ktk qur chapa ya 8 iliyotafcriwa na Sheikh Abdullah Salej Al-Farssy
 
Haaa....haaa....haaa !
Umekwamaa, maelezo meengi, upuuzi mtupu.
Qur'an ndio muongozo wetu na si maoni yako. Vipi Yesu alisema waumini waabudu lini ?
Wayahudi wao wanaabudu lini ?
 
Ni vizuri kumjua huyo Musa kwanza ni nani.

Musa alikuwa kiongozi wa Wana wa Israel na Mwanzilishi kwa maelekezo ya Mungu wa utaratibu wa sheria za Ibada ya Wana wa Israel, Dini inayoitwa leo ya Kiyahudi, Judaism. Kiebrania anaitwa Moshe Rabbeinu maana yake Moshe Our Rabbi(Musa Mwalimu Wetu wa Dini).

Namba ya Musa kiyahudi, Moshe Rabbeinu ni 613 ambayo pia imelingana na idadi ya sheria/maagizo (mitzvot) ambazo Mungu kupitia Musa aliwafundisha wana wa Israel kuzitimiza.

Musa ni binadamu pekee ambaye alionana na Mungu uso kwa uso, Kumbukumbu Ya Torati 34:10, na kuongea nae moja kwa moja live, Hesabu 12:8.

Musa alizaliwa mwaka wa Kiyahudi wa 2368 baada ya uumbaji, tarehe 7 ya mwezi wa kumi na mbili (adar) kwa kalenda zetu unaangukia mwezi wa pili na wa tatu.

Musa alikuwa mtoto wa Mzee Amram na Mkewe Yokebedi, wana wa Israel wa kabila la Lawi. (Kutoka 6:16-20), (Kutoka 2:1-2). Musa alizaliwa wakati wakati Mama yake akiwa na umri wa miaka 130.

Baba yake alimpa jina la Chaver(rafiki) na Babu yake akampa jina la Gedori (Avigdor). Binti wa Farao baada ya kumfanya mwanae alimpa jina la Minios, yawezekana kutokana na mazingira aliyompata mtoto Musa, kumuokota mtoni,Kutoka 2:10, jina la Minios lina maana ya "toa nje", Moshe ni tafsiri ya kiebrania ya jina hilo la Minios ambalo kwa kiswahili ni Musa.

Musa alizaliwa katika kipindi kigumu sana, kipindi ambacho Farao alikuwa ametoa agizo kuwa watoto wote wa kiume wa Waebrania (watoto wa Israel) wauwawe, kipindi hiki Wana wa Israel walikuwepo utumwani Misri.Kutoka 1.22. Mama yake Musa alifanikiwa kumficha mtoto wake huyu kwa kipindi cha miezi 3, baada ya kipindi hiki akamtengenezea maficho mtoni, mahala ambapo binti wa Farao alimpata, Kutoka 2:6. Kwa ushauri wa dada yake Musa, Miriam, binti Farao alimuajiri Mama yake Musa, Yokebedi kuwa yaya wa mtoto Musa, Mama huyu sasa akiwa yaya wa mwanae na bila binti wa Farao kujua ndiye akamjenga Musa kujitambua yeye ni nani na ndugu zake ni akina nani, na kujenga upendo kwa ndugu zake Wana wa Israel waliokuwa utumwani Misri, yeye akiwa Ikulu ya Farao.

Machache yanajulikana juu ya maisha ya utoto ya Musa ndani ya Ikulu ya Farao, biblia haijaeleza sana juu ya hili, kwa historia ya kitamaduni za Kiyahudi, kuna habari kuwa pindi Musa alipokuwa kijana mdogo ndani ya Ikulu ya Farao, siku moja alikwenda na kuketi miguuni mwa Farao pindi Farao akiwa kwenye kiti chake cha kifalme pamoja na Washauri na Waganga wake na Musa akamvua Farao kofia yake ya Kifalme kimchezo tu kama Babu achezaye na mjukuu wake.

Kitendo kile kwa tasfiri ya waganga wa Kimisri waliokuwa pamoja na Farao ilikuwa ishara mbaya ya uasi wa Musa dhidi ya Farao. Hili kuthibitisha kiu ya utawala ya Musa mbele ya Farao kabla ya kumuangamiza, wakamuwekea Musa mbele yake bakuli kubwa ya mkaa unaowaka na bakuli kubwa ya dhahabu safi ya Farao. Kama Musa akichukua dhahabu ya angepaswa auawawe maana ingethibitika sio mwaminifu kwa Farao na ana uchu na Ufalme wa Farao. Lakini kwa msaada wa Malaika na kwa mshangao wa wote, Musa alichagua kuula mkaa wa moto mdomoni mwake badala ya kuchukua dhahabu ya Kifalme, kitendo hiki kilimuepusha na kifo siku hiyo lakini kilimpa kilema cha mdomo, toka siku hiyo Musa hakuweza tena kuongea vizuri, Kutoka 4:10.

Kufupisha, Musa alichaguliwa na Mungu kuwaongoza Israe kuelekea nchi ya ahadi, Kutoka 3-4, aliwaongoza wana wa Israel kwa miaka takribani 40 kueleka nchi ya ahadi, Kanaani, na Mungu alimpa Musa torati kwa niaba ya Wana Israel, Kumbukumbu ya Torati 12:24.Torati ambayo Musa aliwapata wana wa Isarel, torati ambayo kwa ujumla wake ina vitabu vitano, Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu ya Torati.

Maagizo mengine ya mdomo, oral tradition, yanapatikana pia kwenye historia na tamaduni za wana Isarel, talmud. Musa hakuingia nchi ya ahadi, Kumbukumbu ya Torati 32:48-52.

Japo Mungu alimuonyesha Musa nchi hiyo ya ahadi ya Wana Israel akiwa mbali. Kumbukumbu ya Torati 34:4 " BWANA akamwambia hii ndio nchi niliyowaapia Ibrahiu, na Isaka na Yakobo nikisema, nitawapa wazao wako. Basi nimekuonyesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko" . Ni nchi hii ambayo leo Wana wa Israel, watu wa Musa, wanapigana na Waarabu kuihusu.

Musa alifariki juu ya mlima Nebo mwaka 2488 akiwa na umri wa miaka 120, Kumbukumbu ya Torati 34:7, kuepuka Wana wa Israel kuliabudu kaburi lake, Musa hakuonekana tena baada ya kwenda mlimani ambapo ndipo alipokufa na kuzikwa na Mungu mwenyewe bila wanadamu, mwili wake haukuwahi kuonekana. Kumbukumbu ya Torati 34:5-6.Yoshua Mwana wa Nuni alichukua uongozi wa Wana Israel baada ya Musa, kama Mungu alivyomuagiza Musa, Kumbukumbu ya Torati 34:9.

Maneno ya mwisho ya Musa (Moshe Rabbeinu) yalikuwa haya: Kumbukumbu ya Torati 33:29
"U heri, Israel. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na Bwana! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahala pao pa juu."

Huyu ndiye Moshe Rabbeinu, shujaa wa wakati wote wa Israel, Mtumishi Mwaminifu wa Yehova, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
 
Alikuwa mtu mweusi ndo maana alioa pia mke mweusi kwa yule mzee aliyekua akimchungia kondoo wake
 
Alikuwa mtu mweusi ndo maana alioa pia mke mweusi kwa yule mzee aliyekua akimchungia kondoo wake
 
Alikuwa mtu mweusi ndo maana alioa pia mke mweusi kwa yule mzee aliyekua akimchungia kondoo wake
 
wanakupotezea muda.. waulize Musa alizaliwa kipindi gani na uislamu umeanza lini? ni kama mashariki na kusini.. usipoteze muda wako kubishana na wanywa kahawa na stori zao.
Wewe kama huna elimu ya mile kilichoulizwa ni vema ukae kimya sio utoa maneno ya kejeli,nyambavu.....
 
Haaa....haaa....haaa !
Umekwamaa, maelezo meengi, upuuzi mtupu.
Qur'an ndio muongozo wetu na si maoni yako. Vipi Yesu alisema waumini waabudu lini ?
Wayahudi wao wanaabudu lini ?
Yesu alikuwa akiitakasa sabato,yaani ilikuwa desturi yake kuitakasa sabato(luka 4:16).Sabato sio ya wayahudi kwa taarifa yako.Ilifanyika kwa ajili ya mwanaadamu(marko 2:27).Sasa wewe ni nani?Nikupe taarifa nyingine.Sabato ni ya BWANA,MUNGU,na si ya wayahudi(kutoka 20:10).
*Unasema quran ndo muongozo.Pengine hujui.Mtume wako anasema Musa na Haruni walipewa kitabu kipambanuzi kwa wacha Mungu(qur 21:48),je,na wewe ni mcha Mungu?Basi kitabu alichopewa Musa na Haruni ndo muongozo kwako na c alichopewa Muhammad.
*Mungu wako anamwambia mtume wako,hatakiwi kuhukumu ilhali torati ipo(qr 5:43).Sasa wewe hilo la kusema qurani ndo muongozo kwa wacha Mungu umelitoa wapi?Unabishana na mungu wako?Wewe na mungu wako nani mkweli?Tuambie sasa
 
Hizi porojo umeziokota kijiwe gani !?
Nimekuuliza Yesu kasema muabudu lini na vipi ?
Wayahudi na dini yao ya Uyahudi wanaabudu lini ?
Wakiristu nani kawaambie waabudu jumapili ?
Waabudu jumamosi ni 'manyani' tena yana laana ! Aliye na laana ya Mungu ni nani wa kumuongoa ?
 
Back
Top Bottom