Sasa hao Wayahudi mbona hawamuabu Yesu na wanamwita mwanaharamu !
Wakiristo na wayahudi wanakutania wapi ?!
Tofauti ya Ukristo na Uyahudi ni juu ya Kristo aka Masiha Mpakwa Mafuta wa Bwana, shina la Daudi.
Wayahudi bado wanamsubiri Kristo aje ili wamfuate wakati Wakristo wanaamini Kristo aliishakuja na jina lake ni YESU. Ndio tofauti kubwa na ya msingi.
Katika Ukristo inaelezwa Kristo Yesu atakapokuja mara ya pili Wayahudi watamkubali na kuwavuta kuwa wake.
Yohana 7:
25 Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue?
26 Na kumbe! Anena waziwazi, wala
hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo?
27 Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako.
31 Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?
41 Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo.
Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya?
42 Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?
43 Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake.
47 Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika?
48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?
49 Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa.
50 Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao),
51 Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo?
52 Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.
Mathayo 28:
Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ile ya Jumapili, Mari amu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikwenda kuliangalia kaburi. 2 Ghafla pakatokea tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu Malaika wa Bwana alikuja kutoka mbinguni akalisogeza lile jiwe, akalikalia. 3 Malaika huyo alifanana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. 4 Wale walinzi wa kaburi walipomwona walitetemeka kwa hofu, wakawa kama wamekufa.
11 Wakati wale wanawake walipokuwa wanakwenda, baadhi ya wale askari waliokuwa wanalinda kaburi, wakaenda mjini kuwaeleza makuhani wakuu yote yaliyotokea.12 Baada ya kufanya mkutano na wazee na kushauriana, waliwapa wale askari kiasi fulani cha fedha na 13 kuwaambia, “Semeni, ‘Wanafunzi wake walikuja wakamwiba usiku sisi tukiwa tumelala.’ 14 Kama habari hizi zikimfikia gavana, sisi tutamridhisha na hamtapata shida yoyote.” 15 Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha wakafanya kama walivyoagizwa.
Na habari hii imeenea kwa Wayahudi mpaka leo.
Zekaria12:
9 Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu.
10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake.