Hivi mwanajeshi wa Marekani ana hadhi sawa na mwanajeshi wa Tanzania? Kuanzia kipato/ mshahara, mafunzo?

Hivi mwanajeshi wa Marekani ana hadhi sawa na mwanajeshi wa Tanzania? Kuanzia kipato/ mshahara, mafunzo?

Wenzetu hupigana Vita za kiuchumi .Mfano Vita ya kuitandika Iraq iligharimiwa na makampuni ya mafuta ya marekani yalitoko Kuwait.

Ni.kuwa Saddam Hussen alivamia Kuwait kule makampuni makubwa ya mafuta ya marekani ndio yalikuwa yameshika biashara ya mafuta ya Kuwait

Wakaiambia serikali ya marekani pelekeni jeshi mkamtwange Saddam Hussein Pesa za gharama za Vita tutalipa sisi.Bunge na serikali ikaidhinisha.

Ndio maana waweza shangaa iweje Iraq ivamie Kuwait halafu Marekani kimuume.Mbona sisi tulivamia Uganda na mmarekani hakuja kututwanga?

Jeshi la Marekani Ni chombo Cha kiuchumi.cha ulinzi wa biashara za Marekani popote Duniani.La kwetu ni la kizallendo linaishi kwa bajeti ya Kodi za walala hoi machinga,mama ntilie,Bajaj,bodaboda,machinga nk
Kwahiyo tulibadilishe VP!? Shida ni watawala au ni aina ya watu walioko jeshini fikra zao bado mgando???
 
Aaaah mkuu unataka uchukue tonge langu!? Ila jamaa yuko vizuri mfukoni sio siri nilijaribu kumdodosa Jana akasema kwao mtu akijiunga jeshini serkali inamuhakikishia maisha,,yan hana wasiwasi kwamba atajenga Lin,familia itakula nini,,akanambia wao wanaambiwa wafikirie marekani kuitawala dunia tu wala sio maisha
Haha hapana mkuu sio lengo langu hilo hata kidogo, Nilitaka kujua tu coz jamaa amejiexpose sana nawakati bado yupo kwenye service tena nchi ya watu. By the way labda mamlaka inajua uwepo wake so sishangai kuwa opened kiasi hicho..
Kwa aliyokueleza ni kweli wenzetu wanajaliwa sana kuanzia maladhi, makazi na kiinua mgongo.
Sisi huku hatulipwi mishahara bali posho tu
 
Wala hainigusi,,binafsi nilipenda kuwa askari hasa Jwtz lkn mzee akanikatalia kwamba ntadumaa kiakili na kiuchumi ikabidi nimsikilize
Hahaha aisee umenifanya nicheke sana😂😂
And do you think your daddy was right?
 
Kimafunzo tofauti hua ipo ila si kubwa, na mala nyingi hua ni kwenye aina ya vifaa tu

mfano General wa JWTZ hatofautiani sana na General wa USA

Tofauti ipo kwenye maslahi, wao wako juu kuliko hawa wa kwetu

NB: haya ni maoni yangu niko tayari kurekebishwa.
 
Haha hapana mkuu sio lengo langu hilo hata kidogo, Nilitaka kujua tu coz jamaa amejiexpose sana nawakati bado yupo kwenye service tena nchi ya watu. By the way labda mamlaka inajua uwepo wake so sishangai kuwa opened kiasi hicho..
Kwa aliyokueleza ni kweli wenzetu wanajaliwa sana kuanzia maladhi, makazi na kiinua mgongo.
Sisi huku hatulipwi mishahara bali posho tu
Anatoa misaada kwa kibali kabisa kuna shule imemwagiwa kompyuta 70, vitabu kibao, kajenga matundu 10 ya vyoo
 
Jeshi letu niseme wazi hatujakitumia vizuri .Marekani wanalipwa vizuri sababu jeshi hutumika kuvamia nchinkiuchumi ili wapore Mali ziende Marekani.

Mfano majeshi yetu yalienda kupigana nchi zote za kusini mwa Afrika jeshimlingevamia migodi ya almasi na dhahabu Afrika kusini,Zimbabwe,Namibia,no na visima vya mafuta Angola na kuvamia Kongo kupora raslimali kule na kuzileta Tanzania ,Tanzania ingekuwa nchi tajiri kuikaribia Marekani.

Tatizo jeshi letu halitumiki kupora Kama la Marekani wanapigana tu Kama wehu hawakwapui
Yaani pamoja na migodi yote tuliyonayo hapa tz tena mikubwa na wingi wa madini tofauti tofauti bado umasikini upo wa kiwango cha sgr. Hata wangeturuhusu kuchukua bure yasinge tufikisha popete.

Air force, navy sea, special forces, swat, huwezi linganisha na wanajeshi wetu hawa tunaogombania siti kwenye daladala,

Achilia mbali ujuzi combat wanazo vaa watanzania unakuta zimepauka mpaka rangi haionekani vizuri, kwa mbali unaweza kudhan mgambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😅😃😃😂😁
Mtu Anajifanya Anajua Kiingereza Na England Hajafika
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Kwahiyo tulibadilishe VP!? Shida ni watawala au ni aina ya watu walioko jeshini fikra zao bado mgando???
Jeshi linatakiwa libadilike liwe la kiuchumi zaidi.Nchi ikisema JWTZ njooni .Wape invoice chap chap lipeni kiasi hiki wanaume tuingie kazini sio ohhh tutalipwa baada ya Vita .Unapiga hesabu gharama zote na faida juu .Kuanzia miposho ya uhakika kwa pesa za kigeni ya wapiganaji.Unawaambia vijana wa kazi ingieni.kazini .Pesa IPO. ya uhakika

Nyerere Mimi Kuna vitu nilikuwa simuelewi Idd Amin alipovamia Tanzania akisaidiwa na Ghadaffi wa Libya sababu Ni muislamu mwenzie .Akampa vifaa na wanajeshi kibao waarabu wa Libya.

JWTZ wakatembeza kichapo na wakafanikiwa kuwateka Askari wote wa Libya waliokuwa wakipigana Uganda kusaidia Uganda .JWTZ ilipowateka Uganda ikaenda kuwaweka kuwaficha mkoa mmoja wa nyanda za juu kusini sehemu ambayo si rahisi kijua kuwa walikuwa kule.Wakawa wanahudumiwa vizuri mno .Wengine Hadi waliomba wawe wakristo sababu wakiona jinsi nyerere Mkristo akivyowatendea vizuri

Vita ilipoisha Libya ikaomba suluhu na Nyerere kuwa yaishe walikosea baada ya ujumbe wa Ghadaffi kumpelekea ripoti nzuri ya jinsi mateka wa Uganda walivyohudumiwa vizuri na Mkristo Nyerere Roho ikamuuma kuwa itaonekana uislamu mbaya kwa watanzania akasema akaomba alipe gharama zote Tanzania ilitumia kwenye Vita ili Nyerere amrudishie mateka wa Libya waliotekwa uganda

Nyerere alichojibu akasema yeye hauzi watu yeye Mkristo akamwambia Ghadafi achukue watu wake mateka bure .Wakasafirishwa kwenda Libya Tanzania Wala JWTZ haikupata hata shilingi Mia.

matokeo uchumi ulidorora nchi ikawa na Hali ngumu ya ajabu Nyerere kakomaa tu oo wananchi tumetoka vitani fungeni mikanda!!!! Nchi ikawa hovyo kiuchumi Hadi yeye mwenyewe akaamua kuondoka kwa aibu akisingizia ohhh nangatuka neno ambalo hata kwenye kiswahili halimo kumbe anatoroka hajui nchi atairudishaje Hali Yake nzuri kiuchumi baada ya kutoka vitani.

Huyo Ghadafi Kama mimi.ningekuwa Raisi ningempa invoice na faida juu anilipe gharama ya Vita na pia serikali ya Uganda mpya tuliowasaidia kuingia vitani ningewapa invoice Wailipe JWTZ gharama zote za Vita na faida juu

JWTZ isikubali kupigana Vita yoyote isiyo na maslahi ya kiuchumi kwa jeshi au nchi.Vita za kibwege waachane nazo
 
Hebu tuache masihara tuongee fact,licha ya kuzidiwa ki technology lakini hata uimara wa wanajeshi wetu ni wa mashaka sana (physic) ni nadra kukuta mwanajeshi wa Tanzania hana kitambi yaani suala la mazoezi ya kuweka fit mwili ni shida,huwa nawaona wakiwa kwenye mchaka mchaka aisee utawahurumia maana huwa wanajikata makundi mawili la wenye afadhali wanakuwa mbele wale wenzangu na mimi utawaona nyuma wengine wanatembea majasho yanawatoka wako hoi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani pamoja na migodi yote tuliyonayo hapa tz tena mikubwa na wingi wa madini tofauti tofauti bado umasikini upo wa kiwango cha sgr. Hata wangeturuhusu kuchukua bure yasinge tufikisha popete.

Tatizo liko serikalini Hayo makampuni makubwa ya madini yanayochimba yako masoko ya hisa kule kwao.Hata sisi watanzania twaweza miliki.hisa za hayo.makampuni yanayochimba madini nchini serikali haitaki watanzania kununua hisa masoko ya hisa nje ya nchi

Kupata Watanzania wengi matajiri sio rahisi tusiporuhusu watu kununua hisa na kuuza kwenye masoko makubwa ya hisa Duniani yaliyoko Ulaya, Marekani na Japan. Huko ndiko matajiri wa dunia huzalishwa kwenye hayo masoko

Pia Kuwezesha nchi kuwa na pesa nyingi za kigeni badala tu ya kutegemea mauzo ya mazao ya korosho sijui dengu na mazao mengine ya mashambani yanayotegemea Hali ya hewa

Kwenye hayo masoko ndiko kwenye mikampuni mikubwa Duniani inayoongoza kupata faida ambayo huuza hisa na kununua yakiwemo makampuni haya tunayoita ya mabeberu yaliyoko Tanzania tunayosema oohh mnatumyonya .Ukinunua hisa kule kwao hunyonywi ni haki bin haki Tena unalipwa kwa pesa za kigeni gawio la faida

Bila Tanzania kuwa active kwa Watanzania kushiriki biashara ya hisa ya kimataifa umaskini utaendelea

Soko la ndani la hisa Ni dogo na maskini ndio maana unakuta hata kampuni Kama Vodacom hisa zimedoda sokoni.

Soko maskini halizalishi matajiri.Ndio maana impact ya soko la hisa la Tanzania haionekani kwa Mwananchi wa kawaida kubadili maisha yake akinunua hisa!!!

Kuna masoko zamani madogo lofa yalikuwa yakiitwa soko mjinga.Ukipata meza Hapo ya kuuza ujue utaondoka kapa Kama Ni nyanya zitakuozea kwenye meza
 
Wale wako juu sector zote,mshahara,mafunzo

Si kweli wanajeshi wa US wanalipwa salary ya kawaida kabisaaa kulinganisha na field nyingine huko US,tena wako chini kabisa kulinganisha na field nyingine kama Accountants, Lawyers, Salesman, Doctors, IT etc

An entry-level Army private analipwa $20,172 kwa mwaka.

Top Air Force generals analipwa $189,600 kwa mwaka.

dodge
 
Sio kweli mkuu, hapa nyumbani wanajeshi wanaheshima kubwa tu na mishahara yao ni mizuri.

Ikumbukwe tu kuwa kila Taifa linajikuna kutokana na uwezo wa rasilimali zake. Hatuwezi fanana wote. Ila kwa viwango vya hapa nyumbani, wanajeshi wetu wanalipwa vizuri.
Halafu inawezekana ni mstaafu kwani mstaafu wa kwetu hawezi kutoa misaada wilayani!
 
Tanzania wanasiasa wakisha wahonga mavyeo na mapesa maaskari wenye vyeo vikubwa, ninyi takataka wa chini hakuna mwenye muda na ninyi.

Mtaambulia vimishahara vya laki 5, kupanda bure daladala na kusokomezwa kwenye makarandiga ya msaada wa USA.
 
Best comment in 2020 so far

Back
Top Bottom