Omnilabeltech
JF-Expert Member
- Jul 26, 2026
- 533
- 845
Tuseme mwanaume anadate na mwanamke anayempenda lakini hana uwezo mkubwa wa kifedha. Ghafla anatokea mwanamke mwingine mwenye pesa, biashara na uwezo wa kubadilisha maisha yake.
Je, huyo mwanaume atamkataa huyo mwenye pesa kwa sababu tayari ana mtu anayempenda, au ataanza kufikiria fursa aliyoipata?
Mara nyingi tunawasikia wanaume wakilalamika kwamba wanawake wanawaacha wakikutana na wanaume wenye pesa. Lakini je, mwanaume akipewa nafasi kama hiyo, huwa anafanya nini?
Swali langu: Je, wanaume wengi wanaweza kukataa utajiri unaokuja kupitia mwanamke mwingine na kubaki na mwanamke wanayempenda, au tunawalaumu wanawake kwa jambo ambalo hata wanaume wanaweza kulifanya?
Wanaume, semeni ukweli bila kujitetea!