Hivi Mwanaume anaweza akachomoka mbele ya mwanamke wenye fedha kuliko mpenzi wake au tunalaumu wanawake tu

Amani ya moyo ambayo Mke wangu ananipa haina bei. Over!
 
Kuna tofauti ya mwanaume na vivulana.
Hiyo hutokea kwa vivulana vivivu ambavyo hulelewa na mijimama kwa kufungiwa ndani.
 
Ni wanaume wachache sana watavutiwa na mwanamke kwa kiwango cha kumuacha mwanamke anayempenda sababu ya pesa. Wengi wataibia ibia tu ila hatataka kurisk kwa kiwango cha mwanamke wake kujua unless ana homon za kulelewa ambazo ni za kike.
 
Ndiyo nimeshakataa mara kadhaa, nina bahati ya kupendwa na wanawake kama mara mbili hivi nimewakataa wanawake wenye hela (tena hela nyingi sana).

Huwa nahisi wana magonjwa fulani fulani labda anataka kuniambukiza

Niliwahi kupata chance pia ya kuoa mzungu bado nilikataa sababu niliamini atanizidi kiuchumi na nitashindwa kumdhibiti (akili za kitoto zamani nilikuwa ninawaza kumdhibiti mwanamke ni kitu kizuri).

Ila kuanzia sasa na kuendelea nikipata bahati za namna hiyo siwezi kuzichezea tena no matter what lakini siwezi kumuacha mke niliye tayari sababu tu nimepata mwenye hela
 
Wewe ni mariooo unaitafuta justification ya kulelewa. Hakuna mwanaume wa hivyo
 
Mwanaume anafunga ndoa na mke wa malengo yake..... madam hii inaweza kua Term Mwanaume imetumika kimakosa
 
Kufikia kuuliza swali kama hili ina maana tayari una conclusion kichwani mwako.

Tutakachochangia sisi ni kukufanya usherehekee madhaifu yako.

Kijana yeyote 'aliyechezwa' jando, kamwe hawezi kuuliza swali la kinyonge kama hili.

Vijana dhaifu niseme hivyo, ama sijui ni mporomiko wa maadili ya kijamii ndiyo inapelekea vijana wa kiume kuwa na mawazo kama hayo.

Hapa sitaki kupoteza hata cha kukushauri, maana tayari ushapinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…