shabiki
JF-Expert Member
- Jan 17, 2013
- 965
- 896
There is no good news like bad news![emoji16]Kwenye maisha ukisimulia watu jinsi jana usiku ulivyolala kwa kunywa uji na kipande cha andazi,watu watakusikiliza kwa makini sana na watakuonea huruma
Kwenye maisha hayo hayo ukisimulia jinsi jana usiku ulivyokula mbuzi choma huku ukishushia na belaire yako baridiiiiii,watu watakuona unajisifu na kujigamba.
AMKA wasimulie jinsi jana ulivyokua zako ukiendesha baiskeli ukapata pancha ukakokota hadi nyumbani,watakusikitikia kisha watakupa pole sana.
AMKA wasimulie jinsi jana kuna dereva daladala kakupiga pasi SUBARU yako,utasikia wanasema unawatambia au unawasimulia chai.
Unashindwa kuelewa binadamu kabiisa hasa hawa wa nchi ya magufuli,wanataka kusikia na kuona nini,au matatizo na shida tu ndio story wanazotaka kusikia? unawaza huelewi sazingine mtu unatamani usimulie kitu unaogopa maana lazima watakuingiza kwenye kundi la wapenda sifa na wazee wa majigambo kina kiduku lilo.
Unajua inawezekana kabisa maisha ya kiduku lilo anayotusimulia humu yakawa ni ya kweli kabisa (kuna jitu lishaguna huko) ndio shida yetu wabongo.