Hivi, nani anatakiwa kuchinja nyama?


Jibu la KIROHO. Ubarikiwe sana. waacheni wanaotaka kupakaa damu wapakae sie tule nyama. Ila kabla ya kuila, itakase kwa DAMU YA YESU
 

Mkuu tunakuelewa vizuri kero yako, lakini wakati mwingine ni vema tukubali kuendelea na utamaduni ulio zoeleka, mbona tunakubaliana nao wanapo funga mahoteli/migahawa ya chakula wakati wa mfungo wa Ramadhani bila ya kujali, kwamba si raia wote ni Waislaam - mwezi mzima unajikuta nawe unafunga wakati wewe ni mkristo!

Sina shaka baadhi ya Waislaam wenye itikadi kali za kidini wakikumbuka hilo labda watajifunza namna ya kuvumilia/kuheshimu dini za watu wengine specifically WAKRISTO.
 
Sasa kama mahusiano yalikuwa mazuri kiasi cha kuita jirani yako akuchinjie kuku au mbuzi ili mle pamoja imekuwaje huu udini wa kubaguana,kuchomeana nyumba za ibada na kashfa? Nani kayaleta hayo ghafla namna hii? Ndugu wanapogombana haraka sana wanamtafuta mchochezi wao na kumu eliminate.Waislam na Wakristo ni ndugu toka zamani wakiishi kwa kushirikiana (hata kuchinja kuku)hivyo ni vema sasa hivi wakamjua ni nani anayewagombanisha?kwa sababu mwanao yu mahututi na mwenye usafiri jirani yako mmegombana kwa udini jee yule aliyechochea udini huo mtamuona?
 
shida hapa nikua ukristo haufundishi njia sahii za uchinjaji bali wayahudi na waisilamu wanafundishwa
 
Hakuna sehemu kwe kolani kwamba mkristu akichinja basi mslam asile.

Mwana mpotevu kwe baibo hakuchinjiwa ng'ombe na mslam.
 
Hakuna sehemu kwe kolani kwamba mkristu akichinja basi mslam asile.

Mwana mpotevu kwe baibo hakuchinjiwa ng'ombe na mslam.
kwao ni haramu kula mnyama aliyechinjwa na mkristo...cha kushangaza wakristo wenyewe hawana tatizo kula mnyama aliyechinjwa kwa kuelekezwa kibla...kuna kitu cha kujifunza hapa...
 
uislamu ni dini yenye utaratibu kwa kila jambo. Hivyo kwa dini ambazo hazina utaratibu, mtatusamehe. Simply hatuli nyama zilizo chinjwa na wasio kua waislamu kwa sababu kwetu nyama hizo ni vibudu kwa kua zimechinjwa bila kuomba idhini ya muumba.
 
Tunakula nyati, anachinjwa? Ili uweze kumchinja inabidi umpige risasi ndipo uwahi kumchinja na wakati mwingine unamkuta amekufa. Nguruwe inabidi umpoteze fahamu ili uweze kumchinja. Chakula kikiandaliwa na mwislamu kuna taratibu inabidi zifuatwe za uchinjaji na mtu yeyote anakula. Mkristo anapochinja kuna utaratibu anaufuata na mtu yeyote anaruhusiwa kula, ila mkristo kabla ya kula kitu anatakiwa abariki chakula pale najisi yeyote inatoka hata kwa mwislam akibariki anakuwa hana tatizo, ila tatizo ni mafundisho ya viongozi wa dini wanashindwa kutoa elimu ya kutosha kwa waumini wao na baadhi yao ni tatizo wanahubiri chuki na bora viongozi wetu wa dini wakawa na elimu za dini na zakijamii kuliko kuwa na kiongozi shule ndogo anaongoza watu wenye uelewa mkubwa halafu anafanya mambo ya kuwagawa wa Tz.
 
Kama shida ya Waislamu ni kuchinja tu basi tutawapelekea na KITIMOTO wawe wanatuchinjia.
 

Wacha utani wewe!!

Unaweza kumuwahi nyati kabla hafa umchinje!!! hujitaki!!??
 
kuchinja mnyama ambaye ni halali ktk uislam ni sehemu ya ibada, hivyo jambo hili huwezi kulitenganisha na dini yao. kwa wakristo tendo la kuchinja pia nao ni ibada huwezi kulitenganisha na dini pia. marastafari kuchinja hakutakiwi kabisa kwa mujibu wa imani yao. sasa ktk makundi haya matatu. MUISLAM akichinja mkristo na baadhi ya rastafarian watakula, ila MKRISTO akichinja muislam hatakula . hivyo jamii yetu imeishi kwa kuvumiliana , kuheshimiana kwa miaka mingi. bila kuweka choyo ndani yake. jamii yetu imempa kisu MUISLAM ili achinje tule wote.[ haikatazwi wewe kuchinja japo si muislam, ila kama muislam akiwa ni miongoni mwa walaji wako mjulishe] kiserikali kwenye hafla zote . kwenye machinjio kisu kapewa muislam.
 
Samahani kidogo wadau, hivi KITIMOTO anachinjwa au anauawa?
Anachinjwa Mkuu au nyundo akianguka na kulegea kisu kinamalizia! Na kule kwetu huwa kazi hiyo tunawapa ndugu zetu ktk Adam kwa sababu wanapenda kuchicha, na ili Tusiwakwaze, na ni kama nguruwe wa shughuli tuwe pamoja! Manake huwa swali lao la kwanza kabla ya kula, "Kachinja nani?"
 
uislamu ni dini yenye utaratibu kwa kila jambo. Hivyo kwa dini ambazo hazina utaratibu, mtatusamehe. Simply hatuli nyama zilizo chinjwa na wasio kua waislamu kwa sababu kwetu nyama hizo ni vibudu kwa kua zimechinjwa bila kuomba idhini ya muumba.
Wacha zako hizo za kuleta!Toa ushahidi wa ayat ndani ya Qurani inayo zuia Mkristo asichinje!Si useme tu kuwa mna uchu wa nyama kwa sana!
 

Na je, mapokeo yanasemaje kuhusu kuchinja binadamu? Sala ni ile ile?
 
Wanyama wengi wanachinjwa kwa Machine siku hizi .... Labda kama ni swala la ajira hapa kwetu / ujasilia mali .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…