Hii ishu ina migogo baadhi ya maeneo na watu wanataka kuanza kugoma kununua nyama. Niliwahi kutana nayo na kwenye maoni ya katiba mpya. Kisheria na kijamii nani wanaruhusiwa kuchinja mifugo machinjioni? Tumezoea mashehe ndo wanachinja, je wachungaji/wainjilisti na mapadre/makatekista wanaruhusiwa kuchinja? Kama ndio kwa nini haikuwekwa zamu? Kama hapana kwa nini iwe hivyo? Kuna ndugu zangu wauza nyama na wengine ni walokole wamenifuata na kuniuliza kuhusu hilo, ukichukulia nina kaelimu ka kukariri wakajua najua kila kitu. Naomba wanasheria, wanajamii, mabwana mifugo na wengine wenye ujuzi wa hili jambo mnijuze ili nisitoe ufafanuzi wa kimgogoro.