Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

Yeah unachokisema ni kweli, hakuna kbaya juu ya hilo mkuu, lkn kwa kuwa mama ni mlezi wa familia anategemewa ajue nn preferable foods kwa 'wanae' then from there it's all about her kuamua kipi kipikwe siku husika, hiyo huenda ikapunguza kero wanazozieleza kina baba hapa.
Exactly, and we expect that by default!
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.
Mimi ningejibu
Bebi leo tunakula hasara😀😀
 
Mkuu kumbe tuko wengi .
Hill swali huwa naulizwa kila jioni,na mimi jibu langu huwa nyie pikeni mnachotaka mi ntakula matunda tu.
Lakini bado ataomba umshauri.

Dah pole sana mkuu kumbe my wife wako nae ni kama huyu hapa.
Hawa watu ni ukoo mmoja sema baba tofauti tu 😂😂😂!
Swali linanivurugaga mood kweli hilo.
 
Sidhani kama linachosha

Yaani kusema tu kwamba Leo unatamani kula ugali au wali inakukera?
Mara moja kwa mwezi haichoshi, ila j3,j4,j5, alhamisi, ijumaa, j1, j2 aah hapana bana...Idara ya mapishi meneja ni yeye! Tusichoshane...
 
Hawa watu ni ukoo mmoja sema baba tofauti tu 😂😂😂!
Swali linanivurugaga mood kweli hilo.
Na siku usipokuwepo hana MTU Wa kumuliza apike nini,hebu fuatilia wapigie simu watoto kuwatakia usiku mwema,na kama uko mbali labda kikazi,kisha waulize mmekula nini usiku huu jibu litakuwa moja wali maharage.

Hata ukae mwezi nzima huko menu itakuwa hiyohiyo hasa dinner ,ndo msosi wamama wameukariri.
 
Na siku usipokuwepo hana MTU Wa kumuliza apike nini,hebu fuatilia wapigie simu watoto kuwatakia usiku mwema,na kama uko mbali labda kikazi,kisha waulize mmekula nini usiku huu jibu litakuwa moja wali maharage.

Hata ukae mwezi nzima huko menu itakuwa hiyohiyo hasa dinner ,ndo msosi wamama wameukariri.
Watoto watapigwa wali ndondo kama jela 😂 hadi utaporudi
 
Dah nalichukia sana Hilo swali, me akiniuliza namtajia chakula ambacho ni ngumu kuweza kukiandaa Muda Huo
Hatakubali hata hivyo, utaskia nani aanze kumenya vitunguu swaumu sahizi 😂😂😂!!! Sasa unajiuliza si angechemsha supu ya mawe tu.
 
Mara moja kwa mwezi haichoshi, ila j3,j4,j5, alhamisi, ijumaa, j1, j2 aah hapana bana...Idara ya mapishi meneja ni yeye! Tusichoshane...
Yaani wewe unashindwa tu kumuelewa huyo dada.
Mimi nimemuelewa vizuri Sana..
Furaha yake ni kukupikia unachotaka kula kwa siku hiyo.
Yawezekana kabisa anajua unapenda pilau,kambale sijui tambi..lakini je labda pengine siku hiyo unatamani ule pilau na si tambi.
 
Pole sana hao viumbe tuwe tuna wasamehe mambo mengine duh ndo walivyo.

Hapa wakwangu ndo ananiuliza eti Mume unakula sasa hivi? wakati anajua tukimaliza taarifa ya habari ya Azam ndo tunakula...ni meshindwa hata kumjibu loh
Ana utani na serikali ya mjengoni huyo! Yani saa 2 ndio anauliza kama unakula. Mzee jiandae kulishwa chai na mkate kama wafuasi wa Yesu 😂😂😂
 
Ndiyo bado kapo jamani. Ila majority kwa vile mnapenda kukaa bar na kuning'iniza miguu juu kama paka: inabidi tu tule wenyewe na watoto maana hamkawii kurudi siku ya pili (after saa 6 usiku)
Kula na wanao tu maana huku nje mishkaki choma na bia ilivyo mitamu. Haielezeki!!!
 
Watoto watapigwa wali ndondo kama jela 😂 hadi utaporudi
Pia kautafiti nilikafanya,wamama Wa nyumbani huwa wanajilipa na ile Kodi ya meza unayoacha asubuhi,kwa hyo anaibana ili apige cha juu.

Anakuuliza kukufanyia timing ili usimbane ametumiaje hyo hela,has a kama wewe ni mzee mnoko,utasikia sisi tunakuwazia wewe sisi tuko sawa we utajibu simple 2 pikeni mnachotaka nyie,basi their favorite food ni chakula cha serikali wali ndondo bei rahisi,anachukua Mchele vikombe viwili na maharage kikombe kimoko toka kwenye ile stock ulinunua pale nzega wakati unatoka kwenye semina mwanza.
Ndo ushapigwa hivyo,hakunaga huduma ya bure mkuu hata kama ulilipa mahari kwao.
 
Kula na wanao tu maana huku nje mishkaki choma na bia ilivyo mitamu. Haielezeki!!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
Mimi mume wangu katika hili lazima tukubaliane mapema kabisa .. lazima ale nyumbani, tena tunamsubiri muda wa kula awepo..
Kama atatoka baada ya kula ni sawa ila muda wa kula ajiandae tu kurudi nyumbani .
 
Hahaha kuishi na Hawa viumbe yataka kuwaelewa kweli kweli na kuwachukulia nadhani hakuna ubaya juu ya Hilo swali ingawaje Kuna saa linaboa hasa pale unapotaka kuona ubunifu wake.mi siyo Hilo tu kila asubuhi ananiuliza Leo nivae Nguo gani,nagundua nikimwambia vaa hiki na kile anafurahi na kujiamini Sana hata Kama nikimchagulia famba😂
 
Back
Top Bottom