Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

kwakweli hata mimi hilo suala linanikera sana, yaani ndani mna samaki, kuku, pweza, harage sukari, unga, mchele na mboga zote ndani ya friji, na ukimjibu pika chochote atakuambia chochote ndo chakula gani. Na pia unaweza mwambia pika mchicha, unarudi kazi unakuta matembele.
 

Mimi nina ratiba ya misosi:-

1.J3 -Ugali
2.J4 -Tambi
3.J5 -Wali
4.ALH-Chips
5.IJM -Ndizi/Nyama
6.JMO-Ugali
7.J2- Pilau
 
Kweli mkuu hizi ratiba nikiwa tu dar ambapo yupo wife na Hg ila porini ni chochote kitachokatiza twende.

Nikiwa Dar najua kabisa leo ni msosi gani na wao wanajua cha kupika.
Dah kweli kabisa, ukiwa na mama lazma ule kwa ratiba maalum
 
Hahahah kweli sema sometime miyeyusho sana hilo swali 😝

Nilichojifunza wanawake kufanya jambo bila kumuuliza MZEE wanaona kama alitafanyika vyema kwahiyo anauliza kupata mawazo yako,kwa kifupi kama hawaamini mawazo yao! kweli swali la mizinguo kila kitu kipo lakini hajui cha kupika wakati kile ambacho kipo ndani kinaliwa ndio maana kimenunuliwa.
 
Hahahahah ndio hivyo man, hawajiamini hawa watu. Anataka approval yako sema ndio wake wazuri sana maana huwa wanaomba ushauri kwenye mambo mengi zaidi. Sio wale wakurupukaji
 
Ndio maana tunaitwa wanaume, tatizo lenu mnataka kujiona sawa na wake zenu, mwanaume ni strong mara zaidi, so ukiona we unamfananisha na wanaume its a point of weakness, ipo siku unaweza mwambia mbona hujifunzi useremala??? Acha fikra dhaifu. Hakuna kazi ngumu kama kumtreat mtu vizuri japo ni rahisi pia.
 
Swali Hilo halinipi shida maana inaonesha anakujali mpaka anakuita beby. Kuna wakati mwanamke anapika chakula halafu mwanaume anafika na kuonesha kutopendezewa na kilichopikwA. Hivo kuepusha hayo Ni Bora unaulizwa maana ukila unachojiskia hata amani inakuwepo
 
Mtu anayepiga hata mkewe utamjua tu.
 
Inaonekana wewe mkeo unamuona kama hazimo ee, inaonekana wewe ni mtu anayeweka vitu moyoni na kuja kuongelea sehemu weak? Au nia yako ni nn? Badilisha mtizamo huo, kuwa a real man,penda familia yako, penda mkeo acha roho mbaya.
 
Mimi nina ratiba ya misosi:-

1.J3 -Ugali
2.J4 -Tambi
3.J5 -Wali
4.ALH-Chips
5.IJM -Ndizi/Nyama
6.JMO-Ugali
7.J2- Pilau
Kwahiyo j5 wali na j2 pilau hii inanikumbusha bweni
Mi sinaga ratiba siko bweni mkuu mi huwa na tabia kumpatia mke fedha kutosha wiki2
Mezani nakuta mapochopocho kiongozi

Huyo Ni Mimi lakini
 
Kwahiyo j5 wali na j2 pilau hii inanikumbusha bweni
Mi sinaga ratiba siko bweni mkuu mi huwa na tabia kumpatia mke fedha kutosha wiki2
Mezani nakuta mapochopocho kiongozi

Huyo Ni Mimi lakini

Mimi lazima nijue ratiba za kula maana kama siku ni wali basi mchana napiga light food tu ,ila kama usiku ugali mchana nakula msosi heavy!!
 
Kwenye thread za watafiti kumbe na wewe umo? Vipi majibu yangu yalikufurahisha? Ukiona kuna thread unasoma halafu huwezi kuchangia, jua kuwa unasoma thread ambayo hustahili kuisoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…