Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

Mshaanza kukomoana, si muachane tu ndugu.
Hamna kukomoana wala mwanamke gani ambaye hajui majukumu yake! Fuatilia hata page za mapishi huko instagram uone wenzio wana idea gani mpya na wewe upike.

Tatizo ni kukosa ubunifu yani we chakula unajua wali marage na nyama tu! Kuna namna kibao za kuupika wali ukaonekana kama new dish.
 
Kiukweli mimi napenda kuulizwa.maana NI mchaguaji mzuri wa chakula
Ugali wa sembe sili,kabichi sili.
napenda wali Nazi na samaki wa Nazi na bamia ziwe za kutoshaaaa.
akibadili kuku,au maini na firigisi ya kukaanga
Hayo yote japo anayajua ila still atakomaa kukuuliza maswali ya kindezi😅
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.

Swali la collective responsibility hili. Hawa uzao wa Hawa mwalimu wao ni Yule Yule.
 
Mi nikiwaza chakula cha mchana we uwaze cha usiku. Maisha kusaidiana. Kwani kusema unachojisikia kula kuna shida gani. Mimi ningekaa na wewe ungekula chakula cha aina moja mpaka ujue kusema unachotaka kula
Kimsingi si nakuwa sili hapo home tu! Kuna haja gani sasa ya kuishi kama nipo jela.

Vyakula nanunua ila tu kwenye ratiba yenu niondoeni maana ntakula huko huko nakotoka nikija nalala tu hayo maswali utaulizana na wanao.

Tuone kama hutabadilika😅 na siku wageni wakija wala sili nao ubaki na aibu yako.
 
Sasa hizo namna wakati anakuuliza si ndiyo umjibu?
Ni usumbufu tafta vitabu vya mapishi ujifunze!!! Hio kazi alitakiwa kuifanya mama yako toka upo kwenu.

Nikikwambia nataka chicken fried rice utaweza pika? Au yataanza mambo ya mie hata sijui hio inapikwaje?
 
Wanaonaga tunaboreka tukiwa ghetto tumetulia. Wanajaribu kusisimua kwa kuleta mazungumzo. Ila ndio yako nje kabisa ya muktadha
Wakiwaza nyumba ndogo itakavyokusisimua, wanachanganyikiwa bila kikomo.
 
Attachments

  • VID-20211125-WA0105.mp4
    2.4 MB
Kwahiyo hawa wasiopenda kuulizwa migawahani wanakula watakacholetewa Life is Easy tusicomplicate mambo madogo.
Ushasema mgahawani mkuu! You are provided with choices ni wewe kuchagua tu nataka hiki its easy kuchagua katika list of options.

Sasa mke yeye nae afanye kama mgahawani akupe list of dishes uchague moja mbona rahisi. Tatizo yeye hata option 1 hana anasubiria wewe umpe input. Hio ndio kero yenyewe sasa.

Mfano mkeo awe na Menu list halafu anakwambia unapenda nini katika hivyo leo basi unampa moja anaandaa hapo ni sawa. Ila sio wewe uanze kufikiria mapishi tena inaboa.

Imagine mi napenda ugali na nyamachoma au mishkaki ataanza kuchoma nyama jikoni?
 
Yaani wewe unashindwa tu kumuelewa huyo dada.
Mimi nimemuelewa vizuri Sana..
Furaha yake ni kukupikia unachotaka kula kwa siku hiyo.
Yawezekana kabisa anajua unapenda pilau,kambale sijui tambi..lakini je labda pengine siku hiyo unatamani ule pilau na si tambi.
Mie nakula chochote uzuri sie tumefunzwa kula chochote kinachopikwa in the day toka utotoni!

Katika vitu ambavyo niligundua sipendi ni dagaa kauzu, kabichi, mchicha, magimbi na ndizi! Yani ukipika chakula nje ya hivyo ntakula tu sina tatizo.
 
Kweli watu tunatofautiana. Mbona ni swali zuri sana, lenye maana kubwa ndani yake.
1. Anakupenda, anakuheshimu na anaheshimu maamuzi yako. Ni kama anavyoweza kukuuliza avae nini wakati ana nguo kabati zima.
2. Anaridhika sana na wewe na yeye anajaribu kukuimpress kuhakikisha unaridhika pia. Hizi jitihada za kutaka kukuridhisha bila shaka huwa anazifanya mpaka kitandani.
Mkuu unajua mnachanganya sehemu ndogo sana!

1.Kuna swali linaloibuka out of comparison ama choices.
Akiuliza nipike nini kati ya A au B kwako ni rahisi kumchagulia. Nivae nini katika hii ama hii! Haya maswali ni mepesi sababu ni multiple choice qns.

2.Kuna swali linalotokana na kuwa clueless kabisa! Yani hana idea kabisa sasa hili ndio huwa kero. Ni sawa na swali la kwenye mtihani uambiwe explain ama discuss huwa haya yanakera.
 
Kweli maisha yanatofautiana sana,maana nina miaka 17 ya uchumba sugu ila sijawahi kuulizwa swali hilo,ngoja nitafute hela maana ndio sababu ya kutoulizwa na % kubwa nahisi hatuulizwi kabisa,maana najua siku nikikuta ugali nyama ni kama suprise,tumezoea mwendo wa harage ugali na tembele tu
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.

dah kaka huyo mkeo sio pacha wa mke wangu kweli.. maana nakereka sana na maswali ya jikon kama hayo.. nilimwambiaga sijawah kumsiki mzee anaulizwa swali la jikon na mshua .. wewe unaniizaje tunakula nini.. au kuniambia vitu flan vimeisha.. au tunahitaj sijui hotpots mpya.. hayo ni maswala yalio chini ya himaya yako.. sijihitaj kujua hata idadi ya glas tulizonazo
 
Kweli maisha yanatofautiana sana,maana nina miaka 17 ya uchumba sugu ila sijawahi kuulizwa swali hilo,ngoja nitafute hela maana ndio sababu ya kutoulizwa na % kubwa nahisi hatuulizwi kabisa,maana najua siku nikikuta ugali nyama ni kama suprise,tumezoea mwendo wa harage ugali na tembele tu
😅😅😅😅😂😂😂 utaulizwa tu badili jimbo
 
dah kaka huyo mkeo sio pacha wa mke wangu kweli.. maana nakereka sana na maswali ya jikon kama hayo.. nilimwambiaga sijawah kumsiki mzee anaulizwa swali la jikon na mshua .. wewe unaniizaje tunakula nini.. au kuniambia vitu flan vimeisha.. au tunahitaj sijui hotpots mpya.. hayo ni maswala yalio chini ya himaya yako.. sijihitaj kujua hata idadi ya glas tulizonazo
Kwamba yeye ndo anunue Hotpot???[emoji3][emoji3][emoji3] Mwanamke atakuuliza tunakula nini kama hujampaa helaa.. wewe mpe lakin 2 kila mwisho wa mwezi uonee..
 
Mie nakula chochote uzuri sie tumefunzwa kula chochote kinachopikwa in the day toka utotoni!

Katika vitu ambavyo niligundua sipendi ni dagaa kauzu, kabichi, mchicha, magimbi na ndizi! Yani ukipika chakula nje ya hivyo ntakula tu sina tatizo.
Umeufufua uzi[emoji1787]
Acha hiyo ya kula chochote,
Wengine tunapenda waume zetu watuchagulie cha kupika kwa siku hiyo[emoji39]
 
Mie nakula chochote uzuri sie tumefunzwa kula chochote kinachopikwa in the day toka utotoni!

Katika vitu ambavyo niligundua sipendi ni dagaa kauzu, kabichi, mchicha, magimbi na ndizi! Yani ukipika chakula nje ya hivyo ntakula tu sina tatizo.
Aisee Mkuu mbona mboga zote huli [emoji23].!
Mimi kitu ambacho swezi kula Ni Makande, ugali nalazimisha sana
 
Raha bwana ufike kwa table ukutane na kitu hata hukujua kitapikwa, sio kuulizana baby nikupikie nini leo...uzuri wengine hatuchagui vyakula, na hata kama hatuvipendi tulishafundisha kukubali na kuridhika na kilichopo mezani, halafu hatuna umwinyi wa "hiki ni chakula cha baba"!
 
Na sisi tunajisikia raha kupika kile tutakachovhaguliwa kwa siku hiyo.
 
Back
Top Bottom