Hivi nchi jirani na rafiki wa kweli wa Tanzania ni ipi?

USA wana Canada, Nigeria wana Ghana, Australia wana New zeeland.

Namaanisha yule jirani ambaye hata ukienda kumtembelea unahisi uko nyumbani tu haubaguliwi. Mila zinaendana.

Kwa Tanzania ni nani? Kenya? Uganda? Rwanda? Burundi? Malawi? Msumbiji?
Mombasa
 
Nchi jirani ni huko kwa wasukuma.
 
We mzanzibari Zanzibar no mkoa uliochangamka itoe hapo
Kama "Zanzibar ni mkoa uliochangamka" kama unavyosema wewe, basi mikoa yote ingechangamka vile, Tanzania ingekuwa ya ajabu sana duniani.

Mkoa unaoendesha li'nchi' kubwa sana na kulifanya hilo li nchi kama mtumishi wake!

Huo si mkoa uliochangamka tu, bali kuna jambo la ziada nyuma yake. Hebu jaribu kuanglia vizuri zaidi ukitambue hicho kitu kilichoko nyuma ya huo mkoa 'janja'.
 
USA wana Canada, Nigeria wana Ghana, Australia wana New zeeland.

Namaanisha yule jirani ambaye hata ukienda kumtembelea unahisi uko nyumbani tu haubaguliwi. Mila zinaendana.

Kwa Tanzania ni nani? Kenya? Uganda? Rwanda? Burundi? Malawi? Msumbiji?
Nchi zote hizi mimi nimezitembelea na kwa maoni yangu Burundi ni nchi bora sana kwa majirani zetu, sikuona kero yoyote ambayo ilinisumbua
 
Ninakubaliana nawe.

Lakini hata katika mslahi, ukitaka kuwapanga hao majirani zetu kwa kipimo hicho cha "maslahi", bado utaona kwamba hakuna tunachoambulia.
Sisi tunabaki kuwa ni "shamba la bibi tu", kwenda mbele.

Wengi wao hao majirani, kama Kenya na Rwanda wako tayari kuzoa kila kilichopo hapa kwa manufaa yao , laikini sis tunafanya nini? Tunaachia tu!

Ndiyo maana hata huyo Magu uliyemnukuu hapo alilitambua hilo kama lilivyo.
 
KENYA na MSUMBIJI, hizo nchi ukienda Mtanzania haina noma kabisa yaan unaishi kama kwenu tu.
 
Ungesema kwa sauti kubwa, au kwa kupiga makelele kabisa ili walioweka pamba masikioni huko kunakotolewa maamuzi wakusikie.

Kila kukicha tunahangaika na Kenya, sijui huko Kenya kuna jambo gani hasa linalowapoteza akili zote hawa wanaojiita viongozi wa nchi hii!
 
KENYA na MSUMBIJI, hizo nchi ukienda Mtanzania haina noma kabisa yaan unaishi kama kwenu tu.
Haujui tu jinsi gani watanzania(wachimbaji wa madini) walivyofurushwa hapo msumbiji Kama magaidi huku wakikataliwa kuchukua kitu chochote kile walichokua wanamiliki.
 
Haujui tu jinsi gani watanzania(wachimbaji wa madini) walivyofurushwa hapo msumbiji Kama magaidi huku wakikataliwa kuchukua kitu chochote kile walichokua wanamiliki.
Haijui huyo ndio maana anaongea kwa mihemko.
 
USA wana Canada, Nigeria wana Ghana, Australia wana New zeeland.

Namaanisha yule jirani ambaye hata ukienda kumtembelea unahisi uko nyumbani tu haubaguliwi. Mila zinaendana.

Kwa Tanzania ni nani? Kenya? Uganda? Rwanda? Burundi? Malawi? Msumbiji?
Rwanda.
 
Haujui tu jinsi gani watanzania(wachimbaji wa madini) walivyofurushwa hapo msumbiji Kama magaidi huku wakikataliwa kuchukua kitu chochote kile walichokua wanamiliki.
Kidogo,.

Hiyo ilikuwa mwaka 2017 mwezi wa 3.

Mzozo ulianzia huko migodini ukaishia mijini hadi mitaani mgeni ukikamatwa hatakama una documento yako safi imekula kwako.

Baada ya kama wiki hivi aalijitokeza msaidizi wa ubalozi(alivyojiita) kuongea na watanzania sasa yeye akasema watanzania wote ndani ya siku tano warudi kwao mwenye nyumba,kiwanja abebe kama hakibebeki uza ndani ya siku hizo.

Watu walitupa vitu vyao kibao bila ya kutaka.
 
Rwanda,Burundi na Uganda. Nchi hizo ukiingia hakuna tofauti na kwenda mkoa wowote ndani ya Tanzania. Congo DRC wakati fulani niliamini kuwa tuna karibiana hadi waliponitoa tongo tongo kwenye mpaka wake na nchi ya Rwanda.

Nikiwa Gisenyi upande wa Rwanda nikataka kukatiza kihalali kabisa kuingia Goma maana ni mji uliounganika na Gisenyi ya Rwanda. 🤾‍♂️🤾‍♀️🕺
Mmama mmoja mlinzi wa mpaka mwenye manyota akachukua pasi yangu ya kusafiria na kuuliza kwa hasira, ... weej hii paspol ya nji gaani? Nikajibu: Tanzania! ... Akasema: Tanzanie wana-passe ku visa. .... kimoyo moyo: Hizi hasira za nini?😳

Nikageuza hapo hapo kurudi Rwanda!. 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…