Hivi nchi jirani na rafiki wa kweli wa Tanzania ni ipi?

Na hao ni watu tuliopambana kufa na kupona katika mapambano yao ya uhuru?

Hapana.

Mimi siwalaumu wananchi wa nchi hiyo, huo ni ubovu wa uongozi katika nchi zote mbili, Tanzania na Msumbiji kwa kukosa kuendeleza mahusiano na udugu kati ya nchi zetu.

Mara nyingi tunakimbilia kulaumu wananchi wa kawaida, lakini kumbe uzembe unatokana na viongozi.

Msumbiji, kati ya nchi zote zinazotuzunguka, pengine pamoja na Uganda, ilipashwa tuwe na uhusiano wa kindugu kabisa kuliko mambo ya ushirikiano pekee.
 
Vitu vingi vya Bongo vinashabihiana na Wakenya, kama lugha vyakula na mababila
 
USA wana Canada, Nigeria wana Ghana, Australia wana New zeeland.

Namaanisha yule jirani ambaye hata ukienda kumtembelea unahisi uko nyumbani tu haubaguliwi. Mila zinaendana.

Kwa Tanzania ni nani? Kenya? Uganda? Rwanda? Burundi? Malawi? Msumbiji?
Burundi ndio jirani mwema kwetu.
 
Kenya. Kuanzia lugha, + uwiano ws makabila. Halafu EAC ya tangu enzi ya mkoloni
 
Watanzania tunapendana sana na BURUNDI. Mtashangaa sio Kenya. Kenya iko kibiashara. Kindugu ni Burundi.
Issue sio kupendana au undugu.

Undugu na Burundi utakusaidia nini ????

Wakanada wamejaa Marekani wanapata ajira, Wamarekani wao wanafaidi soko kubwa la Canada. Ni chumi mbili kubwa zinazosukumana.

Dunia hii ni ya ushindani. Kuamini katika udugu wa kinyonyaji ndio sababu Afrika iliachwa nyuma.

Walikuja wageni hapa wana explore dunia, tukawachukulia poa kama ndugu, tumevaa magome ya miti tuko happy go lucky tunacheza cheza ngoma kutwa, hatujui kusoma kwa hiyo hatujui historia ya ushindani na unyama wa binadamu; wakatutandika viboko, funga kamba, swaga kama mbuzi pandisha kwenye meli, peleka utumwani Uarabuni na Marekani, naive people, shenz type. Halafu wakachuma mali wakasepa. We have never recovered from such ignoramus naivette.
 
Usijitoe akili wakati unajua mliokota dodo chini ya mnazi
 
Matajiri walevi hawanaga marafiki wa kweli
Ukilewa atakuibia pesa
Ukilewa anakuchukulia mwanamke wako
Ukilewa Bill inaongezwa mara dufu ili afaidike
 
Wewe hapa unataka kudanganya watu, na kutaka kujifanya mjuaji, kumbe huna ujualo.

Ushirika wa Canada na USA, mbona hujaulinganisha na ule wa USA na Mexico?

Kwani wewe unadhani Mexico hakuna biashara? USA anapokwenda kupigana vita vyake nchi mbalimbali, ulishasikia akimwita Mexico aende akashiriki vita hivyo?

Watu wengine mbona hupenda sana kujitoa fahamu, halafu wakishafanya hivyo, na wao wanadhani wanao uwezo wa kunyofoa akili za wengine.
 
Aliyekwambia ninani? jaribu kuenda msumbiji saivi halafu njoo utoe feedaback
Najua nachokwambia, ishu iliyopo sasa ni huo UGAIDI ila Mtz ukifika Msumbiji kwanza kabisa ni free visa maisha yako yote. Uwe na Passport tu basi. Unaishi kwa amani kabisa
 
Zimbabwe, Msumbiji, uganda,Burundi,comoro ndiyo ndugu wa karibu kwetu.
 
south africa na tanzania.mpaka leo watafunya vurugu ila kwa mtanzania hakuna.nimeona hata wakenya wanajifanya watanzania na wasomali kule south
πŸ˜„πŸ˜„ Sijui hata unaongea Nini, Jana tu kulikua na maandamano hapo SA baada ya police kuua mtanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…