Hivi nchi yetu ilishawahi kunufaika na Chama chochote cha Upinzani?

Dogo acha kukurupuka, hivi unajua ni nani alikuwa anavujisha hizo skendo?
 
Ndio hasara tulizopata toka vianzishwe.
 
Dogo acha kukurupuka,hivi unajua ni nani alikuwa anavujisha hizo skendo?
Dogo ni wewe unayefanya assumptions, na kama kuna aliyekuwa anazivujisha kwanini hakuzipeleka kwa wabunge wa CCM akawapa upinzani, kwasababu anajua CCM wanalinda ufisadi wao kwahiyo ni chama cha kifisadi, hivyo kama aliwapa wapinzani alijua wapinzani wataokoa jahazi na wakaokoa kweli kutoka kwenye genge la mafisadi wa CCM.
 
Ndio hasara tulizopata toka vianzishwe.
Wewe na hiyo CCM yako miaka 50 na zaidi sasa bado tunapigana na madawati na rasilimali zote tulizonazo, bado vituo vya afya havitoshi, ni sawa nchi ipo ipo tu haina dira, halafu lawama wapewe upinzani, hivi ni akili au matope?
 
Mbona Kafulila aliyezikomalia Skendo ya Escrow sasa hivi yupo Ccm. Dk slaa aliyeibua Skendo nzito za ufisadi yupo wapi?
 
Nimelaumu au nimeuliza? Walishatupa manufaa gani wapinzani? Tumia akili dogo.
 
Wanajamvi, vya siasa vinavyoitwa vya upinzani kama mwandishi alivyoainisha vimeshaleta maendeleo makubwa sana katika nchi hii.

Nasema hivyo kwa dhana ya maana ya maendeleo. Kwamba maendeleo ni ongezeko la uwezo wa watu kuweza kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili. Uwezo huu uko kichwani! Kwa hiyo, vitu ni matokeo ya ongezeko hilo.

Vya na vya siasa vya upinzani ndivyo vimewafungua ubongo watanzania kujadili mambo ya kisiasa katika nchi ya Tanzania.

Vyama vya siasa vya upinzani ndivyo ambavyo vimekuwa vinaimulika serikali katika madudu yote, na serikali ilipoyatekeleza na kuyaacha madudu yale hatua za maendeleo ya vitu zimeonekana.

Kimsingi vyama ya siasa vya upinzani ndiyo thinking power ya Tanzania kwa sasa. Sera zinazotekelezwa mpaka sasa za chama ya wala ni COPY AND PASTE za vyama vya upinzani.
 
Mbona Kafulila aliyezikomalia Skendo ya Escrow sasa hivi yupo Ccm. Dk slaa aliyeibua Skendo nzito za ufisadi yupo wapi?
Wakati wanaziibua walikuwa upinzani, wamerudi CCM kama walivyo CCM uwa wanalinda ufisadi nao wameamua kulinda ufisadi huko. Wamechoka maana wantumia nguvu nyingi kuibua madudu ya serikali ya CCM na CCM wanatumia nguvu nyingi na dola kuyaficha wameamua nao wakale tu huko huko kwa mafisadi. Kumbe unakiri kuwa waliyaibua maskendo eh? Safi sana basi ndiyo mazuri ya Upinzani hayo maana waliyaibua wakiwa upinzani
 
Nimelaumu au nimeuliza? Walishatupa manufaa gani wapinzani? Tumia akili dogo.
Manufaa waliyotupa umeyataja mwenyewe hapo juu kuwa Kafulila na Slaa wakiwa upinzani waliibua skendo, au hayo si manufaa we dogo? Mbona una akili kibaba
 
Nimesema waliziibua? Au walichomekewa wazikomalie? Dogo uko sawa?
 
Watakati mh, mkapa yupo madarakani aliliambia bunge kwa kipato cha Tanzania tunaweza kusomesha watoto wetu buleee bila kulipa ada, baadae mkapa akafuta ada shule za msingi, mbowe aliliambia bunge tunaitaji bara bara 6 za kuingia na kutoka ndani ya jiji,ndio zinajengwa sasa,

Kiufupi bila upinzani mambo meeengi usingeyajua , wapinzani wanafukunyua hukoooooo wanayqleta bungeni hii inasaidia hata wengine wawe waoga kutupiga kwa kuhofia ikifika kwa wapinzani kitanuka ile mbaya

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Nimelaumu au nimeuliza? Walishatupa manufaa gani wapinzani? Tumia akili dogo.
Yani wewe na wenzako mnaoisifia serikali ya CCM hamna tofauti na mtu watu waliyemkabidhi shamba la hekari 1000, lenye kila kitu kuanzia matrekta, mfumo wa umwagiliaji alime alisimamie halafu mwisho wa siku analeta gunia mbili za mahindi na watu wanasema kapambana kweli nafaa
 
Manufaa waliyotupa umeyataja mwenyewe hapo juu kuwa Kafulila na Slaa wakiwa upinzani waliibua skendo, au hayo si manufaa we dogo? Mbona una akili kibaba
Kuna wazalendo wapenda nchi hii waliwapa ili waziibue. Kwa hiyo ni Ccm iliwatumia tu akina Dk Slaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…