Hivi ndio vyuo vya kata vya Tanzania

Hivi ndio vyuo vya kata vya Tanzania

Aliyetoa mada bado hana uelewa vzuri,,hajui kwamba competence yako ktk kaz after kuhitm ndiyo inayomdetermine m2 ??.
 
Wakuu naomba kuweka wazi kwamba hapa tanzania kuna vyuo vya kata hii ni kutokana na ukweli kwamba vinachukua wanafunzi wabovu ,hamna wahadhiri wa kutosha n.k vyuo vyenyewe ni hivi hapa 1.SAUT 2.Arusha university 3.tia 4.cbe 5.teofilo kisanji 5.MUCCoBS ,ahsanteni

Kaka ukiviita vyuo vya kata utaleta ugomvi hapa jukwaani viite: JANJA JANJA UNIVERSITIES. Ndilo jina ambalo halijawa na kashfa. Sekondari tu zinatofautiana sembuse chuo kikuu jamani! Hata kule niliko soma diploma kuna tofauti kati ya chuo na chuo jamani.
 
Ila kuna ukweli JAMANI, kweli mtu asome teofoli,SAUT ajifananishe na aliyesoma HILL?
 
Wakuu naomba kuweka wazi kwamba hapa tanzania kuna vyuo vya kata hii ni kutokana na ukweli kwamba vinachukua wanafunzi wabovu ,hamna wahadhiri wa kutosha n.k vyuo vyenyewe ni hivi hapa 1.SAUT 2.Arusha university 3.tia 4.cbe 5.teofilo kisanji 5.MUCCoBS ,ahsanteni
Wewe unasoma/umesoma chuo gani kizuri, tutajie na sisi tukasome?
 
Naomba mwenye namba za UHAMIAJI please, hapa kuna mhamiaji haramu!
 
Nakuunga mkono,sijawahi kuona mtu kapata point 3,4,5,6 akaenda cbe.
1.kwa hiyo asiye na point 3,4,5, ama 6 ndio hana vigezo na vyuo vinavyomstahili ni vile vinavyochukua wale wasio na vigezo kama alivyotaja mleta mada?
2.kwa hiyo toka CBE ianzushwe na katika matawi yake yote umeshafanya uchunguzi ukabaini hujawahi kuona?ama umejaa assumption za kitoto kuwa hao hawaendi huko?
3.kwa hiyo hao uliowataja ndio wanafunzi wanaostahili kwa vigezo kusoma vyuo vikuu?nitataka uniambie kwa nini wengi wao kati ya hao huwa hawaongozi chuoni ama huko o level wengine walikuwa na matokeo ya kawaida tena wengine mpaka two na hata three?ukiwa na akili unapaswa kujua kuwa mtihani haujawahi kuwa kipimo sahihi cha uwezo wa mtu kiakili ndio maana matokeo hutofautiana sana kwa baadhi ya watu ukifatilia trend yake,tunataka kuona hao unaowasema wana akili wanafanya mambo mapya kwa kugundua vitu na SI KUWA NA UWEZO WA KUKARIRI MADESA TU.
 

HIVI NA WEWE UMESOMA WAPI?kama umesoma UD nataka nijue,lakini tayari nimeona uwezo wako mdogo sana kama unajipambanunua kuwa wanafunzi wa UD ndio bora,jina la chuo halisaidii.

mapungufu yako katika majibu yako kwa aliyetaka kutajiwa wagunduzi toka udsm ni
1.umejibu nje ya hoja maana badala ya kutaja ama kuonyesha hao watu umeenda kuleta orodha ya vyuo kama inavyoonekana
2.inaonekana hata kingereza hujui kabisa,hapa mada inavitaja vyuo vya kata kuwa vinachukua watu wasio na sifa lakini wewe umeleta orodha ya vyuo ulivyofikiri ni bora kwa afrika,naomba usome imeandikwa orodha ile ni ya nini,na kwa sababu nahisi kiingereza ndio hukuelewa ngoja nikusaidie,orodha uliyotuwekea inaonyesha vyuo katika mpangilio wa umaarufu na si ubora, na hapo hapo wakatahadharisha kuwa pamoja na vyuo vya afrika kusini kutokuwa na ubora lakini ndivyo vinavyoongoza katika orodha hii,sasa jiulize kama na wewe ni msomi wa udsm alafu unataka wote tukubali kuwa kila aliyepita udsm ana uwezo kushinda vyuo vingine huku wewe pekee ukionyesha uwezo mdogo sana hata katika kuchangia mada hii,mimi mathalani sikusoma udsm na haikuwa ndoto yangu kusoma udsm,lakini wapo watu waliopita hapo wengine ni primary mate wangu na wengine ni secondary mate wangu lakini kama ukifatilia matokeo kama kigezo hawawezi kuja hapa kujigamba kuwa walikuwa zaidi yangu. nakusubiri kwa hoja na utoe majibu kwa haya
 
We ni product ya vyuo vya kata

kweli wewe hamna kitu kichwani,maana sioni hoja unazotoa,huyo uliyemjibu ameeleza kitu kizuri tu kuwa competence ndio kigezo cha kuweza kumtambua mtu na uwezo wake na hili kwa anaejua asingetoa majibu ya ajabu kama wewe ulivyofanya,kama mwanafunzi wa kata anatambua kuwa competence ndio kigezo angalau unaweza kutumia alafu wewe hujui basi kwangu mimi huyu ndio anayeelewa pamoja na kutoka chuo cha kata kama mnavyosema
 
kweli wewe hamna kitu kichwani,maana sioni hoja unazotoa,huyo uliyemjibu ameeleza kitu kizuri tu kuwa competence ndio kigezo cha kuweza kumtambua mtu na uwezo wake na hili kwa anaejua asingetoa majibu ya ajabu kama wewe ulivyofanya,kama mwanafunzi wa kata anatambua kuwa competence ndio kigezo angalau unaweza kutumia alafu wewe hujui basi kwangu mimi huyu ndio anayeelewa pamoja na kutoka chuo cha kata kama mnavyosema

Wewe ni product ya chuo cha kata
 
HIVI NA WEWE UMESOMA WAPI?kama umesoma UD nataka nijue,lakini tayari nimeona uwezo wako mdogo sana kama unajipambanunua kuwa wanafunzi wa UD ndio bora,jina la chuo halisaidii.

mapungufu yako katika majibu yako kwa aliyetaka kutajiwa wagunduzi toka udsm ni
1.umejibu nje ya hoja maana badala ya kutaja ama kuonyesha hao watu umeenda kuleta orodha ya vyuo kama inavyoonekana
2.inaonekana hata kingereza hujui kabisa,hapa mada inavitaja vyuo vya kata kuwa vinachukua watu wasio na sifa lakini wewe umeleta orodha ya vyuo ulivyofikiri ni bora kwa afrika,naomba usome imeandikwa orodha ile ni ya nini,na kwa sababu nahisi kiingereza ndio hukuelewa ngoja nikusaidie,orodha uliyotuwekea inaonyesha vyuo katika mpangilio wa umaarufu na si ubora, na hapo hapo wakatahadharisha kuwa pamoja na vyuo vya afrika kusini kutokuwa na ubora lakini ndivyo vinavyoongoza katika orodha hii,sasa jiulize kama na wewe ni msomi wa udsm alafu unataka wote tukubali kuwa kila aliyepita udsm ana uwezo kushinda vyuo vingine huku wewe pekee ukionyesha uwezo mdogo sana hata katika kuchangia mada hii,mimi mathalani sikusoma udsm na haikuwa ndoto yangu kusoma udsm,lakini wapo watu waliopita hapo wengine ni primary mate wangu na wengine ni secondary mate wangu lakini kama ukifatilia matokeo kama kigezo hawawezi kuja hapa kujigamba kuwa walikuwa zaidi yangu. nakusubiri kwa hoja na utoe majibu kwa haya

Uandishi wako tu unaonyesha wewe ni product ya vyuo vya kata, hakuna mkato,hakuna nukta hutenganishi paragraph etc etc.....

Sijakataa nakubaliana na wewe kuwa anaweza kutokea mtu mmoja au wawili kwenye chuo cha kata akawa mzuri ila probability ni 1%. Mimi ninapofanyia kazi nimeshamueleza HR kuwa akiona mtu anaomba kazi anatoka kwenye hivyo vyuo vya kata asijihangaishe kumuita kwenye interview hata kama ana first class kwa sababu si halisi.
 
Uandishi wako tu unaonyesha wewe ni product ya vyuo vya kata, hakuna mkato,hakuna nukta hutenganishi paragraph etc etc.....
soma upya,na kama hakuna mkato,wala hakuna nukta ama paragraph,ama wewe ni virus?hivyo vyote unavyosema sijaweka mbona vipo ama umetoroka mirembe?

Sijakataa nakubaliana na wewe kuwa anaweza kutokea mtu mmoja au wawili kwenye chuo cha kata akawa mzuri ila probability ni 1%.
hizi takwimu umezifanyaia wapi?ama umetoka kunywa kiroba na kuja na majibu ya kufikirika kuwa ni asilimia moja?nataka nikwambie kuwa hakuna mwanafunzi anayedahiliwa kwa mfumo wa TCU alafu awe hana vigezo,vinginevyo huelewi vigezo vya kuingia vyuo,na pengiene hujui maana ya university,

wakati chuo kikuu kikiwa udsm pekee wanafunzi wengi walikuwa wanakosa nafasi za kusoma si kwa sababu hawana vigezo ila ni kwa sababu chuo hakina uwezo wa kubeba wanafunzi wote wenye sifa,hapo udsm wanachukua wanafunzi wenye vigezo sawa na vyuo vyote,kuna wenye 1,wenye 2 na wenye 3 kama vyuo vingine kwa matokeo ya advance, na kwa matokeo ya o level, udsm wanachukua wanafunzi waliokuwa na 1, waliokuwa na 2,waliokuwa na 3 na waliokuwa na 4 ila walipata c tatu na kufanikiwa kufaulu vizuri advance, na mwaka huu pekee kuna mwanafunzi yupo hapo mwaka wa kwanza anasoma education O LEVEL ALISOMA NA KUPATA DIVISION 4 kwa sababu alipata C tatu basi alikuwa na kigezo cha kusoma na kufanya mtihani wa advance na ilibidi asome shule ya private niliyosoma O LEVEL na mwisho alifaulu vizuri katika shule hiyo(sitaki kuitaja ila ilikuwa ni ya 17 kitaifa kwa shule za wanafunzi wachache),kwa sasa huyu mwanafunzi anasoma udsm mwaka wa kwanza na div 4 yake ya O level,na wapo wengi wa namna hii hapo.

na hata vyuo vingine pia vinafata vigezo vya university kote duniani na hivyo unavyoiita vya kata.

Mimi ninapofanyia kazi nimeshamueleza HR kuwa akiona mtu anaomba kazi anatoka kwenye hivyo vyuo vya kata asijihangaishe kumuita kwenye interview hata kama ana first class kwa sababu si halisi.
huu ni uwenda wazimu tu.
na huyo bosi wako naye atakuwa hana akili na hana uwezo wa kung'amua.

hivi hajiulizi,mwanafunzi alifaulu mwenyewe O level, akafaulu mwenyewe Advanve na akachaguliwa kwenda chuo kwa mfumo uleule wa TCU,lakini anakosa sifa eti hakusoma sehemu fulani, ni kichekesho sana,leo nikupe mfano mmoja tu,ukisoma historia utakuta kuwa profesa Mwesiga Baregu alifundisha udsm na baadae anafundisha st Augustine,kwaa hiyo unataka kuniambia hao wanafunzi waliochaguliwa kwenda ST Augustine kwa mfumo wa TCU kama wale wa UDSM na hawa wanafunzi wakafundishwa na BAREGU sawa na aliowafundisha udsm, unataka kuniambia ubora wa wanafunzi kwa ufaulu wa kuingia chuoni una dosari gani?na ubora wa Baregu kufundisha unatofautianaje mpaka wale aliowafundisha udsm wawe bora kuliko aliowafundisha st Augustine?
 
Wewe ni product ya chuo cha kata

utakavyoita hata useme nimesoma chuo cha mtaa ama kitongoji sina tatizo maadamu nina uelewa mkubwa na ninachokifanya tena kwa ustadi wa hali ya juu kabisa.

hivi hebu niambie wewe mpaka hapo ulipo umefanya nini cha maana katika jamii ama huko kazini kiasi kwamba unajivunia kusoma huko ulikosoma?umefanya nini cha maana kiasi cha chuo chako kupata sifa toka kwako kama zao lao?

nataka uniambia ni kitu gani ambacho umefanya ama umegundua ama umeboresha katika ulimwengu huu wa sayansi ili tuone kweli sisi wa vyuo vya mtaa hatuwezi kufanya ama hatujawahi kufanya.
 
Sijakataa nakubaliana na wewe kuwa anaweza kutokea mtu mmoja au wawili kwenye chuo cha kata akawa mzuri ila probability ni 1%.

Unamaanisha uzuri upi mkuu?

Mimi ninapofanyia kazi nimeshamueleza HR kuwa akiona mtu anaomba kazi anatoka kwenye hivyo vyuo vya kata asijihangaishe kumuita kwenye interview hata kama ana first class kwa sababu si halisi.

Huu ni umburura uliopitiliza, shame on you.
 
Duh mtoto wa mkoani kachaguliwa UDSM lzm apagawe tu ila ni kawaida mpwa najua bd unaamini ukisema chuo kikuu unaamanisha UD haaaahaa kazi kwl.
 
There is elements of truth in this thread, angalia GPA zinazo gawiwa vyuo vya private ni za juu na kudisco ni kwa nadra au hakuna.
unahitaji tu kueleweshwa kwa sababu hujui.

mifumo yote ya taasisi za binafisi kokote duniani ina ufanisi wa hali ya juu sana na wanasimamia kwa kikamilifu na hata uende marekani utakuta private wana ufanisi kushinda taasisi za umma.

wakati unaropoka hivi jaribu kuanzia mwanzo wa elimu mpaka juu ya elimu.

1.shule ya msingi.

ukichukua watoto wanaosoma shule za binafisi na wale wa shule za umma. utabaini haya.

kwanza marks wanazopata watoto wa shule za binafisi ni kubwa sana kwa sababu kila kitu wamefundishwa kwa ukamilifu na wakaelewa,wale wa shule za umma wanapata marks ndogo sana kwa sababu hawajafundishwa kwa ukamilifu na hakuna usimamizi na wengi wao wanakuwa ni wanafunzi wa kubahatisha maana hawaelewi.

lakini unaweza kushangaa huyo wa shule za umma akawa ana akili kushinda wa binafsi lakini kwa sababu hakufundishwa sawasawa ama hakufundishwa kabisa basi hata ukiwapa swali moja huyo wa umma anaanza kujiumauma asijue la kufanya na huyo wa binafisi anafanya kwa haraka sana na kwa usahihi. bisha kama wewe ni mbishi wa asili lakini kama unachangia kwa hoja utakubali ukweli huu

pili,hata ukiamua kuwajaribu watoto hawa juu ya uelewa wao wa jumla katika mambo mbalimbali utakuta hawa wa private wamejengwa katika misingi ya kujua mambo mengi sana ya kidunia na hawa wa umma unakuta hawaelewi nini kinaendelea na kwa kiasi kikubwa wao ni kukariri kwa kwenda mbele.

tatu,unapokuja mtihani wa darasa la saba unakuta hawa wa shule za binafisi wanapata marks za juu mno sawa na marks wanazopata kwenye mitihani ya shuleni na hawa wa umma ndio wengi wanaishia kupata marks za chini na kufaulu kwa mbinde sawa na marks walizokuwa wanazipata kwenye mitihani ya shuleni

KAMA SHULE YA MSINGI WANAFUNZI WANGEKUWA WANAPEWA MITINI YA SHULE ZAO TU kama mitihani ya kuhitimu,BASI BILA SHAKA UNGESEMA YALEYALE KUWA KWA NINI WANAFAULU WOTE AMA KWA NINI WANAPATA MARKS ZA JUU,LAKINI KWA SABABU MTIHANI NI MMOJA HAPA UTAKUWA KIMYA WALA HAUTAKUMBUKA KAMA NA HUKO WANAPATA MARKS ZA JUU KUSHINDA WA SERIKARI

2.sekondari kidato cha kwanza hadi cha nne.
huku nako hali ni ileile,wanafunzi wa private wanafundishwa vizuri kwa ustadi mkubwa chini ya usimamizi makini,wale wa shule za serikali ndio wanajitafutia wenyewe,kama kuna kitu hakupata ndio basi,hawana mwongozaji,wengi wao hata hawajiaminina darasani wamelundikana kama mahindi,


tofauti yao.

kwanza,wanafunzi wa sekondari shule binafisi wanacover karibu kila kitu kwa wakati sawia,lakini wale wa umma wengine mpaka wanaingia necta form four hawajawahi kusoma kitu,wanaishia kujaza majina tu. kwa hali hii wanafunzi wengi wa private ukikagua marks zao wanapata marks za juu sana hata mashuleni kwao lakini wale wa shule za serikali wanapata marks za chini hata huko mashuleni,kumbuka shule za serikali O LEVEL ndio zinapewa nafasi ya kwenda kuchagua wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mtihani wa darasa la saba na hivyo wanafunzi wengi wa private walikosa nafasi hizo na hivyo shule za private wanafunzi wengi ni makapi baada ya shule za serikari kuwaacha,MIMI MWENYEWE NI MHANGA,SIKICHAGULIWA KWENDA FORM ONE IKABIDI WANINUSURU NA SHULE YA PRIVATE na ni watano tu tulinusuriwa na wengine hawakwenda kokote kwa kuwa hakuna aliyepenya darasa zima,na nikawa mzuri na baadae moto wa kuotea mbali.


pili,wanafunzi wa shule za binafisi wanaongoza kwa ufaulu katika mitihani ya kitaifa huku wale wa shule za serikali wengi wakioongoza kufeli hata kama wanaakili kwa sababu hawahudumiwa ipasavyo,na kwa KUWA WANAFANYA MTIHANI MMOJA WOTE HAKUNA ANAEPIGA KELELE KUWA MBONA WA SHULE ZA PRIVATE WANAPATA MARKS ZA JUU,LAKINI KELELE ZINAZOPIGWA NI KWAMBA SHULE ZA SERIKALI NDIZO MBOVU ILA WANAFUNZI SI WABOVU,kaangalie marks za mitihani ya mashuleni kati ya watoto wa private na wale wa serikali utakutana na tofauti ileile ya watoto wa private kupata marks za kubwa bila kujali kama walikuwa na uwezo usiostahili hata kuchaguliwa serikali na wale wa shule za serikali wanapata marks ndogo licha ya kuwa ndio waliokuwa na ufaulu mkubwa darasa la saba.


mfano mdogo tu,shule niliyosoma mimi O level haikuwahi kufelisha mwanafunzi hata mmoja form two kwenda form three kwenye necta ya form two toka nilipoanza shule pale miaka ya 2000s na kuna siku mwanafunzi mmoja wa shule za serikali akaniambia haiwezekani wafaulu wote kila mwaka labda kama mnaiba mitihani,ukweli naujua kuwa shule haijawahi kuiba mtihani ila nikamuacha kwa sababu yeye alisumbuliwa na imani,na mfano mwingine,mimi nina mdogo wangu wa kike palepale niliposoma na uwezo wake ni wakawaida sana,jana ndo kanitumia matokeo kuwa ana wastani wa 77 na kapata A tano,wa kwanza ana 95 na wa mwisho ana 50, na wako 142. hapo hakuna aliyefeli wote wamefaulu.
lakini ukiniambia niweke matokeo ya shule yoyote ya serikali ni aibu,lazima wapo waliofeli ama wamepenya kwa tabu.


tatu,matokeo ya necta form four hakuna anaebisha kuwa kila mwaka shule za private ndio zinafanya vizuri wakati wanafunzi wote wanatumia syllabus ileile na mitihani ni ileile na vitabu ni vilevile na walimu wao wametoka kwenye vyuo mbalimbali ikiwemo na hivyo vyuo mnavyoviita vya kata


3.advanced level.

kama kuna elimu mbovu niliyopata kuishuhudia ni advance shule za serikali,kama kawaida yao,serikali wanajichagulia wanafunzi wote waliofaulu alafu makapi wanaachiwa tena ndugu zangu wa private,private wanafunzi wao ni wale wa div 3 za mwisho na four,wapo wanaoreseat kabisa,lakini wao ukifika na CCC(C TATU) ZA MASOMO YOYOTE HATA KAMA KWENYE KOMBI INASOMA DFC ama DDF ama CCF nk watakuchukua wanakuumba mpaka unakuja kuapata one,two ama three ya kwenda chuoni.


KWA SABABU NAMI O LEVEL NILIFAULU serikari haikuwa tena na jeuri ya kuniacha,wakanipeleka kwenye shule zao,nilipofika tu shuleni nilichanganyikiwa na mandhari peke yake kabla hata sijaingia darasani,nilipiga simu palepale nyumabani wanihamishe shule lakini ilishindikana,nilisoma kwa tabu sana na mpaka namaliza shule siwezi kusema nilienda advance kufundishwa bali ile shule ni sawa na tu na kituo cha kufanyia mtihani,sitaki hata kusikia serikali na shule zao,pale shuleni nilibahatika kukutana na wanafunzi waliopenya toka shule za serikari ambao kwa idadi walikuwa wachache sana mana wengi tulitoka private schools,wengi wao walionekana kuna vitu vingi sana hawakujua na walifaulu kwa kukariri zaidi hata kama walikuwa na akili nyingi.


nakumbuka matokeo menyewe ya shule ya mtihani wa necta form six yaliwaangusha wengi na wengine wakapata hata zero lakini yote hayo ni kwa sababu,hatukufundishwa,hatukupewa vitabu,yaani ni mwendo wa watoto wa bata wa kujitafutia kila kitu.


matokeo ya form six yakishatoka unakuta watu mpaka wanafunzi wa shule za private walioreseat wamefanya vizuri kwenye shule za binafisi na wale waliopenya na kuchaguliwa serikalini wanaanguka


4.vyuoni

katika vyuo mambo ni yale yale,kwanza ikumbukwe kuwa vyuo vya serikali vimekuwepo muda mrefu sana na vyuo vingi vya private si vya siku nyingi,lakini ni ajabu kuwa kwa muda mfupi sana private wamepiga hatua kubwa sana,si tu katika kuweka miundombinu bali hata katika ubora wa elimu maana hawataki mchezo,sema kinachosumbua watu ni kule kukariri kuwa mtu akisema chuo basi ni mlimani pekee,ama mtu akisema anaenda kusoma engineering basi ni civil engineering,lakini ukimwambia mtu eti nasoma telecom engineering kwa kiasi kikubwa watu wengi mtaani wataona unachukua kitu cha ovyo labda mpaka uanze kumwelewesha taratibu,IMANI NI KITU KIBAYA SANA WAKATI MWINGINE.


NIMETOA MFANO HUMU,shule niliyosoma O LEVEL kuna mwanafunzi kamaliza form six mwaka jana pale,matokeo yake ya o level alipata four ila akafanikiwa kuwa na C tatu katika 4 yake,ikabidi asome pale maana hakuwa na pa kwenda,shule ya private ikamfundisha akawa anapata marks nzuri tu na mpaka necta inafika alikuwa anafikisha wastani wa shule,matokeo yake ya six akafaulu vizuri na sasa yuko tena serikalini wamemchukua kwa kuwa katengenezwa,yuko hapo udsm mwaka wa kwanza,na ndio alikuwa mwanafunzi bora wa mkoa mzima mpaka serikali wakampa zawadi wakati kuna shule kubwa na za muda mrefu za serikali na mashuhuri lakini wanafunzi wake hawakufua dafu kwa huyu,pia shule yenyewe pamoja na kuchukua makapi yote kitaifa ilikuwa ya 17(TUNAPOSEMA SERIKALI HAIFAI WATU HAWAELEWI KUWA KARIBU KILA TAASISI IMEATHIRIKA NA UBOVU WA SERIKALI AMA UBOVU WA MFUMO NA HATA ELIMU HAIWEZI KUWA IMESALIMIKA NA ATHARI ZA SERIKALI KATIKA MATOKEO)


NISEME KWA KIFUPI SANA KUWA SHULE ZA PRIVATE NA VYUO VYA PRIVATE NI SAWA NA TIMU YA ARSENAL,WAO WANA KAZI YA KUTENGENEZA NA KUNOA VIPAJI VYA WANAFUNZI NA KUWAUZIA SHULE NA VYUO VYA SERIKALI AMBAVYO KWA KIASI KIKUBWA NDIO WANAONGOZA KUHARIBU WANAFUNZI ALAFU WANASINGIZIA UBORA WAO WA ELIMU UKO JUU.


Sasa je wote wana uwezo?

IVI WEWE KAMA UMEPEWA KAZI YA KUFUNDISHA 1+1=2 NA WOTE WAKAELEWA UNATAKA WAKIFANYA MTIHANI WAJIKOSESHE ILI WAONEKANE WANATENDA HAKI?this is crazy.
nimesoma O level katika shule ambayo toka ianzishwe miaka ya 1990s mpaka leo haijawahi kupata div zero,unataka wajikoseshe wapate zero?ili iweje?hivi mbona huulizi kwa nini shule za serikali zinachagua wanafunzi wote wenye uwezo alafu zinashindwa kuwafanya wafaulu wote maana hata kabla hazijawachagua wanakuwa wamethibitika kuwa na uwezo.


NI KICHEKESHO SANA KUWA WATU WENGI HAWAWEZI KUNGAMUA.


PRIVATE SCHOOL=wanachagua wanafunzi wao miongoni mwa makapi yaliyoachwa na government schools
GOVERNMENT SCHOOLS=wanachagua wanafunzi wenye uwezo tu na wanaonekana hawana uwezo wanawaachia private.


KAMA UNGEKUWA MDADISI ulipaswa pia kujiuliza kwa nini shule za serikali zenye wanafunzi wote wenye uwezo hawafaulu wote?
pia kwa nini shule za private zinafanya vizuri pamoja na kuwa wanafunzi wengi ni makapi ambao hawakustahili kupata nafasi serikalini?


Kuna vyuo kama SUA, UDSM,UDOM hata ukipata GPA YA 2.5 huyo mtu anauwezo mkubwa kwa kichwa.

acha uongo wewe kutumia majina na si vigezo na ufanisi wa vyuo,mimi mbona kuna watu nimesoma nao shule ya msingi nilikuwa nawazidi uwezo,nikasoma nao sekondari pia uwezo wao ulikuwa chini yangu na hata advance na kwa sababu huku kote mtihani ni mmoja yaani wa kitaifa hawawezi kubisha,sasa kwa kuwa wao waliamua kusoma huko na mimi nikaenda kwingine na mitihani yetu inatofautiana leo unataka kutoa hitimisho kwa kutumia mitihani tofauti???????


hauwezi kuwapima watu kwa kutumia vigezo tofauti,kungekuwa kuna mtihani mmoja wa vyuo ubishi huu nadhani usingekuwepo maana ni wa kishabiki zaidi.


ngoja nikupe mfano mdogo kwa evaluation yangu kuhusu kusifia watu kwa vyuo walivyotoka.
kuna siku nilihudhuria kongamano la kigoda cha mwalimu Nyerere pale udsm MWAKA JANA,mada ilikuwa ni dira ya taifa,huku tukiangazia azimio la arusha,watoa mada alikuwepo zitto na mdada mmoja simkumbuki,
pia alikuwepo Willy Mtunga wa kenya(jaji wa mahakama ya juu kenya,supreme court),KINGUNGE NA WENGINE WENGI.


ilipofika wakati wa floor panel kuchangia,wanafunzi wa udsm walichangia utumbo karibu wote wakionekana walikuwa na uelewa mdogo sana. binafsi nilishangaa sana kwa wale waliokuwepo watanielewa na wasiponielewa nitawaelewesha.


siku hiyo tukapata mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa documentary ya mwanaharati na mpigania uhuru DR. Walter Rodney,UZINDUZI uliofanyika kesho yake na documentary ilitengenezwa na Clairemount Chung kutoka JAMAICA.


nilikuwa mwanafunzi pekee ambaye sikutoka udsm,tulipofika mambo yaliendelea,ilipofika wakati wa kujadili ndipo wanafunzi wa udsm walitia aibu,kwa sababu wazungumzaji walikuwa wanajua mambo mengi sana na english yao haikuwa ya mchezo na mada ilikuwa nzuri sana,

ila nilishangaa kuona wanafunzi wa udsm wakikimbia bila hata kuchangia wala kuuliza swali mara tu baada ya mjadala kuanza na alibaki mwanafunzi mmoja tu,binafisi nilichangia walau kiasi na nikaongea na nguli hao wa histoaria japo mimi si mwana arts. kifupi wale jamaa walikimbia na kwa haraka haraka nilihisi kiingereza ndo kiliwakimbiza na uelewa wa wale jamaa maana haikuwa rahisi kuchangia mbele ya watu wanaojua kupitiliza tena wengine maprofesa toka sehemu mbalimbali duniani.

mjadala uliisha saa sita usiku na wanafunzi tulikuwa wawili tu,mmoja wa udsm aliyebaki japo hakuchangia wala kuhoji chochote na mimi.



Lakini kuna jamaa zangu tulisona nao Adv walikuwa poor academically, wakapata 3 ya mwisho lakini walivyo kwenda private universities wana GPA si chini ya 4 kila mmoja. Hivyo vyuo vya private vingi vinawachukulia wanafunzi wake kama wateja kwa kuwapa alama nzuri ili na kesho waje au walete ndugu zao. Fanya research utapata majibu.

maelezo haya nadhani nimeyajibia vya kutosha,ila si vibaya nikaongeza kidogo.
huko private ufundishaji wao ni tofauti sana na vyuo vya serikali na usifikiri wanapewa marks.


mfano. udsm unaingia lecture,wanafunzi mko kama mia 500 ama 400 ama 300 lecturer anafundisha kundi lote hili na wanafunzi wake hawaelewi kwa mmojammoja,hapo anatumia microphone,hakuna hata nafasi ya kusema mwalimu sijaelewa,ikipigwa lecture ngumu wanafunzi mnatoka hamjaelewa na hamkuuliza ili mueleweshwe,hapo unategemea uje kupata GPA kubwa wakati hata darasani hupati nafasi ya kuelewa kila kitu?marks zinaanzia hapa kupungua na ukitoka hapo unategemea discussion zikusaidie na ukute hao wanaokusaidia nao kuna vitu wamemiss.


vyuo vya private unakuta darasa limegawanywa kwa wanafunzi 40 ama 60 kila darasa japo kozi ni moja na labda ina wanafunzi 150.
wanafunzi wanafundishwa kwa ukaribu mpaka lecturer anapata nafasi ya kuwazungukia aone wanafanya nini,je wameelewa,pia anakuwa amewakariri uelewa kwa kila mmoja,na wasipoelewa wanauliza na mwalimu anawaelewesha na hata ofisini unaweza kumfata mwalimu akakuelewesha. rejea idadi inayotakiwa kufundishwa na mwalimu mmoja,maana hili lundo kama mahindi lina athari zake na wengi wanaingia tu kama ushahidi,


pia serikalini huwezi kumkataa lecturer ambaye humwelewi yaani ni mtindo wa kwenda nae hivyo hivyo,private kama lecturer haeleweki mkisema tu anang'olewa na kibarua kinaota nyasi na mnatafutiwa lecturer anaeeleweka.


HAWA WAKIJA KUFANYA MTIHANI KWA VYOVYOTE VILE LAZIMA WAFANYE VIZURI KULINGANA NA WALIVYOFUNDISHWA.


watu ni wabishi tu. maana sijajua kigezo gani wanatumia kusema WANAFUNZI WA PRIVATE hawana uwezo .
hivyo vyuo vya private vina wanafunzi toka hata shule zinazojulikana kama shule za watu wenye vipaji maalumu kama tabora boys,mzumbe,kibaha,ilboru,tena wengine wamesoma shule za vipaji tu kuanzia form one mpaka form six.

KAMA BADO HAUJAELEWA WEWE UTAKUWA NA AJENDA NYINGINE.
 
Duh mtoto wa mkoani kachaguliwa UDSM lzm apagawe tu ila ni kawaida mpwa najua bd unaamini ukisema chuo kikuu unaamanisha UD haaaahaa kazi kwl.
halafu hawa madogo wanaotoka mkoani wengi ni washamba sana.wanamambo ya kizamani kujua chuo kipo kimoja au viwili.du.na wanaulimbukeni sana wa kuja mjini sijui.mimi mbona nna jamaa yangu amesoma kibaha advance na o level mzumbe na alifanya vizuri sanaa na alienda dodoma hata hakuangalia kwamba asome ud sijui kwa sababu ya jina hapana yeye aliangalia interest zake kama yeye na kamaliza tayari saafi.chuo ni chuo ,ndiyo maana ajira zikitangazwa wanasema mtu yeyote ambae anavigezo kutoka katika chuo kinacho tambuliwa na selikali,hawaandiki sua ,mzumbe wala ud wala cbe.alafu mbona kuna watu wametoka cbe,ifm ndo usiseme,tia, wengi wanafanya kazi katika makampuni makubwa a haata bot na si kwa kupewa
 
Back
Top Bottom