Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu Uchumi wa Tanzania. Takwimu huwa hazidanganyi

Magu alijenga uchumi wa machinga tuπŸ˜…πŸ˜…
 
Ukweli ni kwamba, ukimwacha Mwalimu Nyerere, mpaka wakati huu, hakuna Rais aliyefanya mambo makubwa kwenye uchumi wa Tanzania kama Mkapa.

Ni kwa vile tu watanzania wengi wana vichwa vyepesi vinavyopenda kujadili na kusifia mambo mepesi, mambo mazito aliyoyafanya Mkapa, hawawezi kujua.

Record ya Mkapa, haijawahi kuvunjwa na utawala wowote Duniani. Record hiyo ni ya kushusha inflation toka 30% aliyoiacha Rais Mwinyi, mpaka 4%.

Mkapa ndiye aliyetengeneza mifumo ya uchumi, kodi na fedha.
 
Misukule ya Magufuli itasema kwa nini umamchafua mtu ambaye amelala hawezi kujitetea.

I assure you kama Mwenfazake angekuwa hai tungekuwa kama Zimbabwe au Yemen au Somalia. Tuendelee kumshukuru Mungu kwa kutuondolea yule Shetani
Kwa sisi Wakristo Biblia Takatifu inasema, "msihukumu ili msije mkahukumiwa, kwasababu kipimo kilekile mnachowapimia wengine ndiyo kipimo hichohicho mtakachopimiwa".
 
Kwa hiyo kupanua barabara ndio kukuza uchumi? Lakini mbona husemi kuwa alikuwa jizi la plea bargain?
 
Hizo takwimu ameziandika tu kutoka kwa kiazi mmoja kama yeye Sia za BODI YA TAKWIMU YA KITAIFA

huyu dada ni kiazi kama viazi mbatata vingine

USSR
Jibu hoja, ameshakupa takwimu. Matusi hayasaidii kitu
 
Watu wasio na ajira hawampendi kbsa magufuli as if tatizo la ajira n Tanzania s mngehama tu mkatafute kwenye fursa
 
Yaan mtu mwenye akili timamu kbsa huwez mchukia magu sisi tunaoagiza vitu nje tumepata afueni hasa kwenye suala la AirPort mizgo inawah sababu ya magufuli jamaa alikua very straight sema ndo huwez kumpenda huwezi ona mazur yake kwenye reli dar folen imeisha huduma za jamii zipo almost dar nzima inafika weeknd dar hakuna folen huyo n magu ukienda kila sehem dar panamasoko watu wameacha kwenda mbali kununua bidhaa daaaah afrika sjui tulirogwa wapi aisee ndo maana hatufanikiwa tunaleta lawama z wakoloni kumbe sisi kwa sisi ndo tunarudishana nyuma
 
Magu alijenga uchumi wa machinga tuπŸ˜…πŸ˜…
Hao ndio watanzania halisi wanaotakiwa kuwezeshwa ili kufikia levels za juu kabisa na kushika njia zote za uchumi wa nchi.

Sio hawa wahindi na waarabu wanaotuibia na kwenda kuficha fedha huko makwao.
 
Always Huwa una excuses kama zote kujaribu kutafuta justifications for your failures..

Covidi ilikuwepo kuanzia 2015 Hadi 2020? By the way athari za covid zimeanza kuanzia mwaka 2021 Hadi Sasa Mwendazake akiwa kaburini.
Hebu rudia tena, Mwendazake akiwa ....! Kamata hapohapo tutaendelea tukirudi.
 
Takwimu Uchwara.

Zimepikwa.
Na wala....
Hazibadilishi Mtazamo halisi.


Hao waliopungukiwa Kiuchumi walikuwa walozi, wevi,majambazi, mafisadi, wala rushwa watoa rushwa, watakashishaji fedha, mebeberu na vibaraka vyao, Tundu Lissu na wengine.....

Aisee kuna yale mleta mada aliyomezeshwaπŸ˜‚, sitarudia kuyaweka....nitachangia, siku zikiwadia, halafu niwekwe kwenye takwimu za 'baby shower'


πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ulivyoandika "duniani" tu ukanivuruga, ingawa umeongea vizuri sana.
Kuongeza tu Mkapa aliamsha uchumi ndiyo maana unaona percent ilkuwa 154% kama msemaji wa kwanza alivyosema; alitengeneza macro economy na baadaye akaonyesha way to micro. TZ Vision 2025 ambayo ilifanya mwelekeo kuwa na direction baada ya Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar kefeli.

Issue ya kukua uchumi (acha siasa); ambayo ina-reflect kwenye GDP bado tunampa Mkapa; ingawa kwa Kikwete kuliongezeka billioni 14 almost zile zile alizoziacha Mkapa 13 billioni, na kwa Magufuli 15 billion; lakini reflection ya kazi za Mkapa zinaonekana Zaidi mwaka wa kwanza na wa pili wa Kikwete. Reflection ya Kikwete ilionekana kuanzia mwaka wake wa tatu na kuendelea hadi mwka wa pili wa Magu. Watu mna beza sana Magufuli, kwenye mwaka ujao mtashangaa sana GDP itakapo reflect kwa Samia, investment kama Bwawa la Nyerere, SGR, meli, Ndege, viwanja vya ndege, nk nk itampaisha Samia,

Kwa hiyo kusema kuwa Magufuli ndiyo aliharibu uchumi wa Nchi si ukweli
 
Mojawapo ya juhudi ni pamoja na kipunguza kuajiri na kuwapanga waliopo waweze kufanya kazi kwa bididoooo
Hii imekaaje kwa ustawi wa jamii? Ni jukumu la serikali kutengeneza fursa za ajira kwa kuajiri au kuwezesha mazingira ya watu kujiajiri.
 
mimi nawaamini zaidi wataalam kuliko wanasiasa.
 
Ninapokaaa maji yalikuwa ni mda wote na kipindi chote, kumbe kukua kwa uchumi ni kama ivi sasa Maji hamna kabisa mtaani na ndoo au dumu linauzwa 500. Nakuombea kwa mwenyezi Mungu uwe maskini wa kutupwa duniani na kesho mbinguni ili uonje shubiri ya Ugumu na changamoto za maisha.

siku zote furaha ipo nami.
 
Na nyie pikeni za kwenu Mzee mtuletee 😁😁😁

Kila siku nawaambia Mwendazake alikuwa looser huelewi.Kwamba NBS na BoT na WB wamepika takwimu kama zama zenu au? 😜😜
 
Huo ni uongo wa mchana kweupe? Kwa hiyo kama yalikuwa mda wote yamekauka ghafla au? 😁😁😁😁

Ukitaka kudanganya uwe na logic
 
Kwa sisi Wakristo Biblia Takatifu inasema, "msihukumu ili msije mkahukumiwa, kwasababu kipimo kilekile mnachowapimia wengine ndiyo kipimo hichohicho mtakachopimiwa".
Hata Mimi ni Mkristu halafu Mkatoliki niliyesoma Seminari. Ila nakuambia usijifiche kwenye Biblia kutaka kumtetea Magufuli. Magufuli alikuwa hata kanisa analitumia vibaya kutengeneza UDIKTETA wake.

Hivi alipokuwa anaua akina Ben Saanane kuna kifungu cha Biblia kilimruhusu?

Hukumu yangu ipo Wala Sina wasiswasi
 
Sasa huyo Magufuli Mingi ya miradi yake ni hasara ukiacha bwawa la umeme..mradi kama reli,mabandari ya Ziwa Tanganyika hayawezi kuleta Tija licha ya Kukamilika Kwa sababu hayana linkages..

Pilia miradi Mingi ya aliyoacha Magufuli ilikuwa chini ya 30% lakini Mwenzie Samia mbona anaikimbiza Kwa speed sana? Ndio kusema by 2025 Rais Samia atakuwa amemaliza miradi Mingi sana na akiwa Rais awamu ya pili Na uhakika uchumi Wetu utakuwa mkubwa kuliko wa Kenya Kwa sababu Kuna LNG,kwala, Bagamoyo,Eacop,Mkonga sez nk

Pili Mwendazake yeye kazi yake ilikuwa ni kuanzisha miradi bila Kuimaliza au ndio ilikuwa mbinu ya kutaka kutawala milele Kwa visingizio vya kwamba hakuna Rais atakayemaliza miradi aliyoanzisha?

Pigia msumari,Rais Samia akiendelea kuwa Rais awamu ya pili Tanzania ndio itakuwa baba wa Uchumi EAC maana by that time tutakuwa tunajitosheleza Kwa Sukari,mbolea,mafuta ya kula,nafaka zote ikiwemo ngano na pia Nchinitakuwa imefunguka sana kimiundombinu hasa ya Barabara ,maji na umeme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…