Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

wapo kimya wanaugulia maumivu...mleta mada ambaye ni loyal kawa jasiri na kuanika uovu wote wa TMT
 
Kikubwa achaneni na mambo ya kuambiwa buy or sell piga kitabu tafuta mentor sahihi mlipata elimu ambayo ni basic inatosha kujiendeleza mwenyewe.
Sikuwahi kwenda huko ingawa walinifanya nikaijua forex nikatafuta mentor now mambo ni hivi[emoji91] [emoji91]. Mentor anaerecommend broker mimi sijawahi kuwaamini aisee.
Ngoja nikatafute za weekend[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji100]
 
Mavi hayana ncha lkn ukiyakanyaga lazima uchechemee.


Naendelea kuwapa pole watu wa Forex walioliwa na TMT
 
safi sana
 
Sasa ulisema ili iweje kama unajua watu watakuita scammer unajishitukia kweli bongo tuna safari ndefu katika maisha au unaogopa watu watanufaika sana.
Na wewe nawe unakuwa wale wale wazee wa kulala sikusema hapo juu ili nipate watu au nifundishe watu au nishee nao mbinu zangu hiki kitu sitaki kabisa

Forex iko wazi kama ukijiongeza na kuzama deep sana so usianze tu kulaumu mtu wakati acces zote hizo za kufukua mbinu mujaribu .

Halafu vitabu vina mbinu kibao tatizo manataka ku generalize zote kwa pamoja kwa hili hamtafanikiwa

Chagua moja tu kati hizo za vitabu ifanyie kazi utaonaa mafanikio

Kuwa mbinu nyingi ni sawa na miluzi tu kwa mbwa

Mfano unaweza chagua kutrade kwa trendline tu kaimasta na kuwa superb takataka zongine zote ukaweka kando .

Sasa unakuta mtu anataka mambo yoote ayajue kwa wakati mmoja ndio hapo lazima aharibu

Chagua kimoja kifanye kwa uhakika sio kuchagua kumi kufanya ki averages hutofanikiwa

So pambana forex sio easy jamaani kuna shughuli pevu kweli kweli .

Na jinsi yankujimeneji kisaikolojia napo ishu nzito sana

Forex is not for everyone
 
Walikuwa wana programme ya kuwatrain vijana wa vyuo vikuu wakianzia na UDSM... Bora madogo waendelee kubet, maana Forex inataka watu kama sisi...viburi na wabishi.

jamani! Madogo watapigwa maboom yao hadi wanyambe.
Ndio tumia fursa hiyo nawe uwapige hao madogo maboom yao
 
Mlipotangaziwa kuwa Forex ni utajiri uliojificha mkaona ohooo utelezi huo umewajia! Ivi kuna biashara mabayo benki haitaki ujue afu ikawa halali kufanywa kama haijapigwa ban na serikali?n wakati mnapotangaziwa jambo musome vizuri tangazo na mjiulize.

Biashara ya Forex ni halali na ipo Kweli, ila mnapoenda kwa watu kama hawa Ontario na wengine wamejaa tele instagram kudai kuonesha mafanikio yao, hawa ni wanawageuzia nyinyi kuwa fursa, kupoteza hela kwenu ni faida kwa hawa wanaojiita mentors.

Bila shaka mmejifunza kuwa hakuna pesa ya utelezi kabisa. Kila kitu ni hard working and determination. Ulimwengu wa digitali unawatia watu shoti sana katika maisha. Kama unataka forex njoo Zanzibar kwenye wazungu wa kumwaga uje uuze na ununue dola

Unaambiwa Tanzania ndo nchi pekee unayoweza kumkuta masikini akiuza kitabu chenye mbinu 99 za kuwa tajiri lakini muuzaji wa kitabu kula hajui atapata wapi na kisha mtu ananunua 😀 😀 😀
 
Aisee,,poleni sana

Af hapo Jangid napita kila cku nkitoka kibaruan af pale ofic ya tmt naonaga km kuna watu watu hv,,bdo wapo wanaoenda au??
 
Hahaha Tanzania kuna ujinga mwingi sana
Wacha muendelee kuliwa
Halafu huyo dogo mnayesema ana dharau si mumkate makofi ?
 
Poleni ila kwanza kabisa forex hauwezi kuimaster kwa siku tano tu. Lakini pia kushindwa kujua ni vigezo gani huangaliwa kutambua broker bora ni dalili kuwa hiyo training mliyohudhuria haikuwa na ubora wa kuwasaidia nyie wanafunzi.



Nakuomba usome sana na tafuta broker mwenye spreads nyingi. Kuendelea kulalam wakati una maarifa ya forex hautafika kokote. Achana na Ontario piga kazi
 
Hizo siasa ulizozungumza nazijua aise mimi nimeshindwa kushangaa wewe umesema kuna strategy na vitabu umepitia mahali vimekusaidia sasa sijui ni tatizo gani ukashindwa kushare na wenzako hapa jamvini na wengine wapate kufanikiwa na kuijua kiundani Forex ndiyo maana yakuwa na Jamii Forum au ndiyo wale chakwako marufuku mwengine kukijua.
Mwisho vijana wakitanzania tuna safari ndefu sana katika kufikia mafanikio yetu pamoja na mapungufu yote ya Ontario ila ninampa pongezi za dhati kwakukutujuza kuhusu FOREX maana kuna watu walikua wanapiga kimya kimya na wengine ata material kushare ilikua ngumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…