Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Salaam wadau,

Tuendelee EP 04

Baada ya kuamka pasipo uwepo wa Recho, nikampigia simu. "Hello Good morning" alianza hivo kabla ya mimi kuongea. Nikajibu "morning... uko wapi..mbona hujaniamsha". Recho " Acha woga wewe, nimedamka mapema nikuandalie chai...hatahivo ipo tayari, njoo basi sitting room". Mimi "Poa am coming".

Hapo mapigo ya moyo yakarejea kwenye wastani wake wa kawaida. Nikaamka chap sitting room. Sasa bashasha lililokua usoni pa Recho hata mimi likanipa walakini, akanikaribisha chai. Niseme tu ilikua heavy breakfast, mpaka nikajisemea "kweli dawa imemuingia, sio kwa hospitality ile".


Kwa jinsi alivokua mchangamfu na bashasha nikaona kweli huyu sasa haisi ombwe la upweke tena. Hakika sikukosea ilikua hivo. Recho " Z tumelala wote Jana...nimekubali tuwe kwenye mahusiano lakini ujue kabisa, Nina mume wangu na ananipa kila kitu...najua namkose ila imeshatokea".

Akamalizia, " Ila Z unajua mapenzi wewe khah! Mwanamke gani huyo alikufundisha kut*mb*n*."
Nikabaki natabasam tu. Unajua vile unafeel pale mrejesho ukiwa chanya. Baada ya kifungua kinywa na story Chache nikasepa.


Nakumbuka Ile siku simu yangu haikukauka sms kutoka kwa Recho. Kama sio kila baada ya dakika moja basi ni tano ujumbe unaingia. Nilisifiwa sana na Mimi kurudisha salama vilevile. Sikumbuki takwimu vizuri lakini ndani ya Ile week tulikulana kana kwamba tupo honey moon Magoroto, Tanga.
Jina la Z likapoteza mvuto badala yake naitwa 'Daddy', 'Babaa' au 'my love'.


Ukisikia ndege kunasa tunduni hii sasa haukuishia kwake tu bali hata mimi nikajipata na hisia kalii sana juu yake. Ila hii haiku chagizwa na sex pekee, hapana kuna kitu cha ziada hapa alikifanya Recho. Nitasema baadae.


Mwezi wa pili sasa unaelekea kukatika toka tuanze rasmi wizi. Siku moja aliniambia hivi "unajua unanikula kiasi kwamba hata nikihesabu naona kabisa umezidi idadi ambazo Mimi na mume wangu tumefanya toka anioe." Akaendelea " Em tupunguze kidogo maana huyu akirudi atajua tu...ntashindwa kabisa kum 'act' tia!"

Mimi nikasalia kimya. Recho " unaonaje tuwe tunafanya mara mbili tu kwa week babaa...please kubali basi. Fanya hivo kunisaidia Mimi please".
Sikutaka uwe mjadala mkubwa nikamkubalia.


Ipo hivi, nilianza kwa kumtamani sana huyu dada, ukizingatia jinsi alivyojiweka na muonekano wake bila kusahau falsafa yangu dhidi ya wanawake type yake. Lakini kadri muda ulivosonga niliibua hisia kalii sana za mapenzi, nilihisi nimegraduate kutoka kumtamani na sasa nampenda.

Lile wazo lake likaanza kuniumiza kichwa tena (wivu). "Inakuaje anipangie e...au amepata mdau mwingine?" Hapa nikasahau kama mie mwenyewe ni mwizi, sasa naanza kuogopa kuibiwa mali ya wizi. Ila maadamu nilishakubali nikajisemea tutacheza na beat lakini twice a week Hapana.


Mambo hubadilika, sasa home familia ipo kwahiyo utokaji wangu sio huru sana kama hapo nyuma. Hata ratiba ya kumuona Recho ilibadilika japo sio kwa sehemu kubwa. Mara nyingi tulionana jioni. Wakati mwingine akiforce anione asubuhi basi nilifanya kwenda kwake.


Hii miezi mitatu ambayo nilikua clean bila sex nilikua kwenye mgogoro na kidemu changu cha chuo na Mimi nilikua tayari nimeridhia tuachane ukizingatia hatupo tena mkoa mmoja. Baada ya kufanikiwa kutengeneza mazingira ya kutolala home siku moja nikaenda kulala kwa Recho.

Kulivokucha saa 11 alfajiri sijui hii siku huyu dem tumuite Nailah wa chuo aliniota au vipi. Ilikua hivi:


Mimi na Recho ndani ya duvet, Boxer yangu chini, pichu ya Recho pembezoni mwa kitanda. Yaani tayari wazungu nimeshawahamisha makazi. Mlio wa sms ukasikika.
Kabla sijaendelea msomaji, mara zote tukiwa busy na ujinga wetu Mimi na Recho yule bwana mdogo kama hatakua amelala chumbani kwake basi hua anakua sitting room busy na cartoon.

Tulijitahidi kuficha uchafu wetu. Nakiri hapo tulifanikiwa. Ok tuendelee, mlio wa sms kuingia ukasikika na ni kwenye simu yangu. Kwa speed ya mwanga Recho aliiwahi simu yangu na kuniambia nitoe password. Mara nyingi nilikua nampa anakagua na hakuti kitu kwahiyo sikua na wasi. Simu yangu upande wa sms sikuset 'Hide Content'. Wakati ananipa nitoe nywila akaghairi kisha akaanza kusoma kwa Sauti. " UMEAMKAJE"?.

Nikauliza ni nani?. Akakaa kimyaa kisha akaendelea " Hii namba ninaijua, nimekalili namba za mwisho. Huyu ni demu wako".
Sasa kwa bahata mbaya au nzuri Mimi na Recho tulikua tunatumia simu aina Moja, Samsung alikua na uwezo wa kutafuta chochote kwenye simu yangu.

" Hii namba imekupigia sana japo si hivi karibuni lakini niliona ndio namba mnacheckiana sana... Haya nambie huyu ni nani na kwanini asubuhi hii anakutext."


Nikachukua simu mwenyewe nikaangalia namba, nikaona ni Nailah kweli. "Dah! Huyu Demu ananitakia Nini mimi... asubuhi yote hii sasa najiteteaje." Nikawaza kwa ukimya kisha nikamwambia. " mpenzi wangu, huyu ndio yule mwanamke nilikua nae chuo... nilishaachana nae ila hatakkubali matokeo".

Recho tena kwa Ngeli na jazba " I am the one who supposed to know umeamkaje kwasababu tumelala wote...huo ujasiri anautoa wapi kukutumia text asubuhi... Mimi sio mtoto Z !!!.
Lete mpya
 
Tuendelee EP 06

Kweli nikaweka mambo yangu sawa kisha nikaitikia wito. " Babaa nina mimba...ila sijui ina muda gani". Akaendelea " nimetoka kupima muda nakupigia simu ". Mimi "kipimo kipo wapi naomba nione". Recho " kwani hata nimeipata nguvu ya kukitunza...nilivoona majibu nikakiflash chooni kabisaa!!. Mungu wangu!?!!".

Nilipatwa na hisia mbili kwa mpigo. Moja, sasa huyu ni mke wa mtu tutafanyaje, huzini. Pili, ilikua ni hisia za furaha kwamba kumbe uwezo upo. Mpaka naweza kutia mwanamke mimba, ewaa safii.

Mimi " naomba Ile dawa tulionunua juzi". Akaieleta na nikaanza kusoma maelezo kwa mtumiaji. Kweli bhana haitakiwi kutumiwa na mjamzito. Hapo nikajiridhisha ni kweli huyu ana mimba ndio maana baada ya kutumia tu hali yake ilikua mbaya. Wakati napitia yale maelezo ya Ile dawa, Recho alisoma uso wangu na kungundua kuna kitu nilikua nawaza.

Recho " unawaza nini my love...please niambie!". Mimi " nipo sawa ila nimeona hapa ni kweli hii dawa haifai kwa mjamzito". Recho " Em nione... na kwelii maana badala ya kupata haueni kidogo nife".
Hii dawa sitaitaja jina. Ila nafikiri kwa mjamzito inaweza toa mimba na hata kusababisha kifo ingawa sina uhakika sana kuhusu kusababisha kifo.

Baada ya kujiridhisha kweli Recho kashika mimba mjadala uliofata hapo ni tutafanyaje. Ipo wazi kwamba Mimi ni jobless na yeye ni mke wa mtu. Je atoe au alee mimba?. Kwa namna yoyote' hakukua na option ya ziada zaidi ya kutoa mimba kwa maslahi yetu wote wawili , lakini yeye zaidi kulinda ndoa yake.

Nikurudishe nyumba kidogo. Nilisema hali ya kumpenda kwa dhati Recho ilianza kuibuka siku hadi siku sio kwasababu ya sex pekee. Sasa ilikua hivi.

Kama wiki moja kupita toka tuanze wizi, Recho alianza kuniulizia habari za kutafuta kazi na hata palipo hitajika support ya pesa ili kufanikisha harakati za kutembeza bahasha yule dada alijitoa kwa dhati.
Maneno kama " hujachoka kula ugali wa shikamo".." tafuta kazi babaa sikumoja uje uwasaidie wazee wako hasa mama", ni kauli ambazo zilikua zikijirudia kwenye akili yangu na kusababisha nione huyu mwanamke ana kitu".

Recho hakuishia hapo tu, alifika hatua ananiamba " kama hujatuma maombi/application yeyote leo hunikuliii". Na hapo atakomaa mpaka nimpe ushahidi, kama sio email nilizotuma basi copy za barua nilizopeleka kwa mkono. It was really funny but potential somehow. Hakika ilikua kama masihara lakini yenye faida.

Hapa vijana tuongee jambo, ni kweli unapenda mashuga mamy ya kulee ni sawa. Au wake za watu kwasababu hawana gharama kuwatunza ni sawa pia lakini amini mwisho wa mahusiano utabaini umepoteza zaidi kuliko kupata. Why?

Sugar mamy atahitaji umtimizie haja za mwili na si vinginevyo. Pesa atakupa ndio, kitu ambacho kitakulemaza au kukufanya kuwa tegemezi pasipo kuchangamka/kupambana wewe kama wewe kupata chako kitakacho dumu.

Hio ni moja lakini pili, Hilo li jimama lina watoto au familia tayari yani maanake hadaiwi kuzaa zaidi ya kula maisha. Je kwako wewe ambaye unamwaga maji ya ujanani yenye uwezo mkubwa wa kukupa watoto kila wiki una uhakika utabaki rijali hivo mpaka utakapo oa ?

Jibu rahisi ni Hapana. Uwezo lazima utashuka kwasababu ya kutumika sana. Hapo magonjwa ya zinaa nimeyaweka kando. Fikiria Hilo kisha chukua hatua.

Ok tulitoka nje ya kisa kidogo lakini ni kwa manufaa ya Adam. Turejee, kutokana na Hali ya Recho kuonesha langu lake lake langu nilijipata nampenda sana. Na ndio maana sasa baada ya Nailah kuleta shida Ile siku nikamplease kwa udhaifu mkubwa. Hivyo suala la yeye kushuka mimba yangu lilinipa furaha zaidi kuliko mawazo kitu ambacho Recho hakujua. Kweli mapenzi ni upofu.

Tukakubaliana atoe ila nimtafutie elfu hamsini tupate dawa ya kutolea. Kwa wakati ule ni kweli kuna kimchongo part time nilikipata kutokana na Ile pushing efforts zake kuhusu kazi kwahio nilimudu kupata hio pesa. Mimi " Sawa hio pesa unahitaji muda gani?". Recho " ikipatikana mapema ni sawa zaidi ili nimuagizie mtu then nitameza usiku".

Nilimpatia hio pesa majira ya mchana na nilipofika kwake nikakutana na habari nyingine mpya. Sasa hii habari ikaniondolea furaha na kuleta hisia mbaya.
Recho " me sielewi hii siku ina nini". Mimi "Kuna Nini tena mamaa, mbona sikuelewi?". Mume wangu kasema anakuja mwezi huu au ujao sijui itakuaje!?!". Hapo ndio nikaamini huyu ni mke wa mtu. Na nilishindwa kuhimili Ile taarifa nikanyongonyea mpaka dada wa watu akaogopa.

Recho " sasa mbona unakua hivo my love... kwani nimesema tutaachana?!.. hapana nimekwambia tu ili ujue". Mimi "Ooh! Sawa!" Huku nikishusha mpumzi kubwa. Nakaaga nikaondoka lakini Recho alinotice sikua sawa.

Swala la mimba likakosa mashiko badala yake huzuni yangu niliyonesha baada ya kutaarifiwa ujio wa mkuu wa kaya ukachukua nafasi zaidi kichwani kwa Recho. Tuliwasiliana mpaka saa 4 usiku na tukaagana vizuri. Sasa ni saa sita usiku Recho ananipigia tena , napatwa na hofu, je anataka kuniambia Nini....
 
Unatia kambi katika suala la kuzini
Astakfillah astakfillah wee man is not a fan of the way to the hyperspace and the way you want to do it now and I can do it now but pearl has been in the office for years and accountability to the hyperspace to get the same thing as
Hello please try to comprehend the briefing sort of an abstract of the story. Nobody is promoting infidelity nor adultery but rather uncovering the impacts against them. Learn to percieve things with a very positive sense.
 
Hello please try to comprehend the briefing sort of an abstract of the story. Nobody is promoting infidelity nor adultery but rather uncovering the impacts against them. Learn to percieve things with a very positive sense.
Mjomba mi kingereza nilichoandika hapo ni ile wanaita typing suggestions, dont take seriously mkuu...

Naona umenitemea ung'enge' huo daaah
Ndgu samahani bana mi nimetoa general tuu kuwa kuzini ni dhambi..

Kama mada yako ipo nje na ishu za kuzini mkuu basi samahani
 
Mjomba mi kingereza nilichoandika hapo ni ile wanaita typing suggestions, dont take seriously mkuu...

Naona umenitemea ung'enge' huo daaah
Ndgu samahani bana mi nimetoa general tuu kuwa kuzini ni dhambi..

Kama mada yako ipo nje na ishu za kuzini mkuu basi samahani
Hakuna shida mkuu. Hahah! Karibu sana.
 
Inapoelekea hii stori yako, lazima mtukumbuke Wazee wenu kusema "Kitanda hakizai haramu"

Ama msemo wa Vijana wa hovyo akina Poor Brain kwamba "..kwenye Ndoa zenu tuna watoto wetu..."

Kwa hoja hizi naona Kataa Ndoa wamepata ushindi wa goli 5 kama alizofungwa Kagera Sugar Jana na Simba 🙌
Alafu nilijua babu ushajilekebisha kumbe bado ngoma bila bila daaah ....

Atakaye kubadilisha wewe tabia yako inabidi awe ana PHD ya saikolojia 😄😄😄😄😄
 
Alafu nilijua babu ushajilekebisha kumbe bado ngoma bila bila daaah ....

Atakaye kubadilisha wewe tabia yako inabidi awe ana PHD ya saikolojia 😄😄😄😄😄
Hahaha.............. Kuna wakati unajikuta tunatamani tuonekane vijana wa miaka 30 lakini Mvi na kutembelea mkongojo kunatuangusha Wazee 🙌😜

Kuweni na huruma na Wazee
 
Inapoelekea hii stori yako, lazima mtukumbuke Wazee wenu kusema "Kitanda hakizai haramu"

Ama msemo wa Vijana wa hovyo akina Poor Brain kwamba "..kwenye Ndoa zenu tuna watoto wetu..."

Kwa hoja hizi naona Kataa Ndoa wamepata ushindi wa goli 5 kama alizofungwa Kagera Sugar Jana na Simba 🙌
Ni kweli. Mambo ni moto mbeleni hapo.
 
Back
Top Bottom