Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Lete mpya
 
Tuendelee EP 06

Kweli nikaweka mambo yangu sawa kisha nikaitikia wito. " Babaa nina mimba...ila sijui ina muda gani". Akaendelea " nimetoka kupima muda nakupigia simu ". Mimi "kipimo kipo wapi naomba nione". Recho " kwani hata nimeipata nguvu ya kukitunza...nilivoona majibu nikakiflash chooni kabisaa!!. Mungu wangu!?!!".

Nilipatwa na hisia mbili kwa mpigo. Moja, sasa huyu ni mke wa mtu tutafanyaje, huzini. Pili, ilikua ni hisia za furaha kwamba kumbe uwezo upo. Mpaka naweza kutia mwanamke mimba, ewaa safii.

Mimi " naomba Ile dawa tulionunua juzi". Akaieleta na nikaanza kusoma maelezo kwa mtumiaji. Kweli bhana haitakiwi kutumiwa na mjamzito. Hapo nikajiridhisha ni kweli huyu ana mimba ndio maana baada ya kutumia tu hali yake ilikua mbaya. Wakati napitia yale maelezo ya Ile dawa, Recho alisoma uso wangu na kungundua kuna kitu nilikua nawaza.

Recho " unawaza nini my love...please niambie!". Mimi " nipo sawa ila nimeona hapa ni kweli hii dawa haifai kwa mjamzito". Recho " Em nione... na kwelii maana badala ya kupata haueni kidogo nife".
Hii dawa sitaitaja jina. Ila nafikiri kwa mjamzito inaweza toa mimba na hata kusababisha kifo ingawa sina uhakika sana kuhusu kusababisha kifo.

Baada ya kujiridhisha kweli Recho kashika mimba mjadala uliofata hapo ni tutafanyaje. Ipo wazi kwamba Mimi ni jobless na yeye ni mke wa mtu. Je atoe au alee mimba?. Kwa namna yoyote' hakukua na option ya ziada zaidi ya kutoa mimba kwa maslahi yetu wote wawili , lakini yeye zaidi kulinda ndoa yake.

Nikurudishe nyumba kidogo. Nilisema hali ya kumpenda kwa dhati Recho ilianza kuibuka siku hadi siku sio kwasababu ya sex pekee. Sasa ilikua hivi.

Kama wiki moja kupita toka tuanze wizi, Recho alianza kuniulizia habari za kutafuta kazi na hata palipo hitajika support ya pesa ili kufanikisha harakati za kutembeza bahasha yule dada alijitoa kwa dhati.
Maneno kama " hujachoka kula ugali wa shikamo".." tafuta kazi babaa sikumoja uje uwasaidie wazee wako hasa mama", ni kauli ambazo zilikua zikijirudia kwenye akili yangu na kusababisha nione huyu mwanamke ana kitu".

Recho hakuishia hapo tu, alifika hatua ananiamba " kama hujatuma maombi/application yeyote leo hunikuliii". Na hapo atakomaa mpaka nimpe ushahidi, kama sio email nilizotuma basi copy za barua nilizopeleka kwa mkono. It was really funny but potential somehow. Hakika ilikua kama masihara lakini yenye faida.

Hapa vijana tuongee jambo, ni kweli unapenda mashuga mamy ya kulee ni sawa. Au wake za watu kwasababu hawana gharama kuwatunza ni sawa pia lakini amini mwisho wa mahusiano utabaini umepoteza zaidi kuliko kupata. Why?

Sugar mamy atahitaji umtimizie haja za mwili na si vinginevyo. Pesa atakupa ndio, kitu ambacho kitakulemaza au kukufanya kuwa tegemezi pasipo kuchangamka/kupambana wewe kama wewe kupata chako kitakacho dumu.

Hio ni moja lakini pili, Hilo li jimama lina watoto au familia tayari yani maanake hadaiwi kuzaa zaidi ya kula maisha. Je kwako wewe ambaye unamwaga maji ya ujanani yenye uwezo mkubwa wa kukupa watoto kila wiki una uhakika utabaki rijali hivo mpaka utakapo oa ?

Jibu rahisi ni Hapana. Uwezo lazima utashuka kwasababu ya kutumika sana. Hapo magonjwa ya zinaa nimeyaweka kando. Fikiria Hilo kisha chukua hatua.

Ok tulitoka nje ya kisa kidogo lakini ni kwa manufaa ya Adam. Turejee, kutokana na Hali ya Recho kuonesha langu lake lake langu nilijipata nampenda sana. Na ndio maana sasa baada ya Nailah kuleta shida Ile siku nikamplease kwa udhaifu mkubwa. Hivyo suala la yeye kushuka mimba yangu lilinipa furaha zaidi kuliko mawazo kitu ambacho Recho hakujua. Kweli mapenzi ni upofu.

Tukakubaliana atoe ila nimtafutie elfu hamsini tupate dawa ya kutolea. Kwa wakati ule ni kweli kuna kimchongo part time nilikipata kutokana na Ile pushing efforts zake kuhusu kazi kwahio nilimudu kupata hio pesa. Mimi " Sawa hio pesa unahitaji muda gani?". Recho " ikipatikana mapema ni sawa zaidi ili nimuagizie mtu then nitameza usiku".

Nilimpatia hio pesa majira ya mchana na nilipofika kwake nikakutana na habari nyingine mpya. Sasa hii habari ikaniondolea furaha na kuleta hisia mbaya.
Recho " me sielewi hii siku ina nini". Mimi "Kuna Nini tena mamaa, mbona sikuelewi?". Mume wangu kasema anakuja mwezi huu au ujao sijui itakuaje!?!". Hapo ndio nikaamini huyu ni mke wa mtu. Na nilishindwa kuhimili Ile taarifa nikanyongonyea mpaka dada wa watu akaogopa.

Recho " sasa mbona unakua hivo my love... kwani nimesema tutaachana?!.. hapana nimekwambia tu ili ujue". Mimi "Ooh! Sawa!" Huku nikishusha mpumzi kubwa. Nakaaga nikaondoka lakini Recho alinotice sikua sawa.

Swala la mimba likakosa mashiko badala yake huzuni yangu niliyonesha baada ya kutaarifiwa ujio wa mkuu wa kaya ukachukua nafasi zaidi kichwani kwa Recho. Tuliwasiliana mpaka saa 4 usiku na tukaagana vizuri. Sasa ni saa sita usiku Recho ananipigia tena , napatwa na hofu, je anataka kuniambia Nini....
 
Hello please try to comprehend the briefing sort of an abstract of the story. Nobody is promoting infidelity nor adultery but rather uncovering the impacts against them. Learn to percieve things with a very positive sense.
 
Hello please try to comprehend the briefing sort of an abstract of the story. Nobody is promoting infidelity nor adultery but rather uncovering the impacts against them. Learn to percieve things with a very positive sense.
Mjomba mi kingereza nilichoandika hapo ni ile wanaita typing suggestions, dont take seriously mkuu...

Naona umenitemea ung'enge' huo daaah
Ndgu samahani bana mi nimetoa general tuu kuwa kuzini ni dhambi..

Kama mada yako ipo nje na ishu za kuzini mkuu basi samahani
 
Hakuna shida mkuu. Hahah! Karibu sana.
 
Inapoelekea hii stori yako, lazima mtukumbuke Wazee wenu kusema "Kitanda hakizai haramu"

Ama msemo wa Vijana wa hovyo akina Poor Brain kwamba "..kwenye Ndoa zenu tuna watoto wetu..."

Kwa hoja hizi naona Kataa Ndoa wamepata ushindi wa goli 5 kama alizofungwa Kagera Sugar Jana na Simba πŸ™Œ
 
Alafu nilijua babu ushajilekebisha kumbe bado ngoma bila bila daaah ....

Atakaye kubadilisha wewe tabia yako inabidi awe ana PHD ya saikolojia πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Alafu nilijua babu ushajilekebisha kumbe bado ngoma bila bila daaah ....

Atakaye kubadilisha wewe tabia yako inabidi awe ana PHD ya saikolojia πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
Hahaha.............. Kuna wakati unajikuta tunatamani tuonekane vijana wa miaka 30 lakini Mvi na kutembelea mkongojo kunatuangusha Wazee πŸ™ŒπŸ˜œ

Kuweni na huruma na Wazee
 
Ni kweli. Mambo ni moto mbeleni hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…