Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja


Umesema vizuri sana mkuu, mleta mada hataki watu wahoji, anataka wakubali tu anachosema, halafu kwanini focus iwe utt tu? Au promo?
 
Mmmmh nikianza kuweka 1000 leo nikifikisha miaka 60 ntakuwa na mil.70.... Za nini? yani hapo maisha yangu yote nimekuwa maskini wa kutupwa then at 60 napata mil 70...what for?

For your kids Khantwe
 
Last edited by a moderator:
All is well but 500 books in 5 yrs!! I dont think so!!
First; Kusoma idadi hiyo ya vitabu inamaanisha kila baada ya siku tatu masaa 15 na dakika 36 kitabu kimoja kiwe kimesomwa!!!!
Naona tutafute namna bora zaidi ya kupata elimu tofauti na vitabu 500!

Second; 500 books means aloat of money!
Huyu mtu ambaye ceiling yake ya kusave ni buku(1000) anaweza vp kupata kitabu kila baada ya siku tatu! Nani atampa hicho kitabu? Maktaba ya taifa??? I dont think so!!
How much is kitabu kimoja times 500 = UNAFFORDABLE.
Au ndio unataka kufikia malengo kwa kufungua duka la vitabu kuwauzia wanaotaka kufanikiwa!!
 
wewe unayeita watu wa tz wewe ni mnan??

Duh hili ni tatizo lingine. Mkuu kama umesoma post yangu nmeandika hiv "Duh watz tuna matatizo sana". Sasa cjui swali lako lina mantiki gani maanq tayar nmesema tuna matatizo manake mm.mwnyew ni mtz. Tatizo letu lingine ni kukurupuka hatusomi vitu tukaelewa, tubadilike jamani
 
Hayo masaa mbona ujaweka na kuwa kwenye foleni na kusubiria usafiri hasa kwa walio mijini.

Ingawa mada niyacku nyingi lkn maudhui yake bado yananguvu.....Kuhusu kusoma vitabu hata kwenye Foleni au umesimama kwenye Daladala inawezekana kupanga nikuchagua....Wasi wasi wangu ni hiyo kusoma vitabu viwili kwa wk JE,,,!! utaelewa kilochoandikwa? manake issue ckumaliza Rundo la vitabu ishu nikuelewa kilichoandikwa humo....nami narudi pale uliposhauri Nilazima kusoma vitabu bila kujali idadi gani ya Vitabu na kwa muda gani kinachotakiwa ni Kusoma vitu muhimu ambavyo vitakusaidia kuboresha Shughuli.zako
 
Makaka hii niliandika tarehe 10/10/2014, mpaka leo tarehe 27/12/2014 ni siku 67 zimepita. Hii ina maana kwamba kama ulikuwa unaweka ile elfu moja moja niliyokushauri leo hii ungekuwa ja zaidi ya elfu 67, au ungekuwa unaweka zaidi ya hapo ungekuwa na fedha nyingi zaidi.
Muda unakwenda na sio rafiki kabisa, kama unasema haiwezekani chakarika kufanya kile unachojua Kansas kana. Kama unaona inawezekana changamkia kufanya hivyo. Mwisho wa siku kila mtu atapata kile alichofanyia kazi.
Nawatakia kila la kheri ja sikukuu njema.
Tupo pamoja.
www.amkamtanzania.com
 
Asnte sana kwa uchambuzi huo je kuhusu kifo itakueaje? Na ofic zenu ziko wapi?

Samahani kwani we we unajua utakufa lini?unapojenga nyumba una uhakika gani utaishi humo nyumba ikiisha?unapowekeza ktk biashara una uhakika gani utaishi mpaka uwekezaji uanze kulipa?unapozaa una uhakika gani utakuwa hai kulea watoto wako?unapoanza anza kazi tar 1 una uhakika gani utafika mwisho wa mwezi upokee mshahara wako???ukiogopa kufa utaogopa hata kupumua kwa vile utakuwa unamaliza pumzi zako.....na utakufa kwa vile umegoma kupumua!
 
Bado Sio kama hatutaki Nakubali ila mfumo wa maisha haya ni ngumu xana
 
Makirita,Uzi mzuri sana huu,mwanzoni nilipousoma niliona haiwezekani lkn inawezekana km utakua focused,kwa mtanzania maskini ambaye hamiliki mali yoyote iliyorasimishwa akisona hii itamsaidia sana,wengi wanaopinga wako sahihi,lkn pia hawako sahihi kwa sababu wanatazama mazingira yao na wanadhani kila mtz anaishi hivyo.

Na pia la kuongeza si lazima uwekeze kwa muda mrefu,unaweza wekeza kwa muda mfupi pia ukafanya yako ukipata kiasi cha kutosha,kuna watu wanaanza biashara kwa mtaji hata wa elfu 50,bwana makirita ametoa mwongozo mzuri,unaweza fuata km ulivyo au ukachagua kinachokufaa kwa mazingira yako.
 
mimi nimeisoma, nitajipa muda kutafakari na kuamua moja. maswali ambayo napenda niyafaham before joining the program, ni kwa kiasi gani inatofautia na African Life assurance? maana nao wana swaga kama hizi
 
Wabongo waliwekeza DECI pesa zote zikapotea mpaka leo.je UTT mkoje?
 
Umesema vizuri sana mkuu, mleta mada hataki watu wahoji, anataka wakubali tu anachosema, halafu kwanini focus iwe utt tu? Au promo?

Huyu ni kibaka tu... alikuja kwa kasi sana naona kashapotea
 
Nimeanza kusoma, nilipofika hapo kwenye red nikaacha. Umejifunza wapi Math?

hata mm sijaelewa hiyo formular na hiyo link siioni.
nikikumbuka hela zangu za deci sina hamu. topic nzuri imetufundisha kusave lakn habar za kwenda kusave kwa mtu sijui benk visacoss wizi mtupu. wacha nisave kwenye kibubu after five years nikivunje. hiyo 10% ni compassation tu ya kushuka kwa thaman ya hela na si faida kama ambavyo tunalishwa tango pori hapa.
 

Unajua mleta Mada anania njema sana,na pia naungana na wewe.
tatizo letu sie Vijana ni kulalamika,na kijana yoyote na walow engu ukimuambia suala la kuweka akibna kwake ni tatizo.Na hapo ndio utaona anavyoibua hoja za ajabu,mara kifo,mara uzee nk.
Na tatizo ni kwamba watu wamekariri muandikaji alivyopost badala ya kupick idea ya muandishi.
Sasa kila anaponda hoja hii unakuta kwamba ameichukua kama ilivyo.
Sie wengi tunapenda kuweka akiba sehem ambayo unaweza kuiuchukua akiba yako hata pale pasipo na sababu za msingi.
Mie ninamjomba wangu alinunua hisa Sigara miaka ya mwanzo ya 2000,leo hii wote tunamuheshim,maana yupo vizur sana na alipofarikia watoto wote walisoma vizuri na wao waka chukua nafasi ya kuendeleza hisa za mzee wao.
Tatizo ni kwamba wengi tunakaribisha matatizo tunapokuwa na pesa.Na ndio maana suala la kuweka akiba kwa muda mrefu ni janga.
 
Wether amekopi hii makala au ameitunga yeye, SURELY IT IS VERY BENEFICIAL.

Point ni nzuri sana.
Just take an idea, utagundua kitu kikubwa sana.

Vitabu 500 in 5 yrs ni utaratibu wake yeye, why dont u choose one in a year ambayo kwa upande itakusaidia?
Maana point hapa ni kuongeza
maarifa.

1000 per day ilikuwa ni illustration tu, why dont you find a suitable way for you, suitable time and suitable place to save?
Sio lazima utt... ok find any suitable place.
The idea behind is the habit of saving kwa malengo ya badaye, ukitaka hata 3 months not necessarily 30 yrs.

Mfano mi nilikuwa natumia up to 8000 for lunch, approximately 40,000/= per week, at the same time home nimeacha 10,000 ya chakula.
Lakini tangu nijifunze habit ya kusevu sasa msosi maximum buku 3, the rest nimehamishia savings ili after a certain set period nifanye kitu cha maana. Home nanunua vitu in bulk on weekly basis. Na hii ni sehemu ndogo tu ambayo nimeamua kuconvert basing on my environment. Bado maeneo kama airtime, unnecessary outings n.k

Na leo nimepata somo jipya la UTT,nilikuwaga naiona tu lakini naichukulia poa tu.

In order to change your life, you have to change something you do daily. (T. B. Joshua)

THEREFORE JUST CONVERT THE IDEA INTO YOUR PERSONAL ENVIRONMENT.
 
safi sana mchangia mada tatizo la watanzania wengi tunapenda kulalamika kuwa maisha magumu wakati chanzo cha maisha magumu ni sisi wenyewe tatizo kubwa tunapenda tuanzie juu na tunapenda sana starehe tukipata hela we angalia wangapi hapa wanaolia hawana mtaji alafu waambie kuna kasemu kakufundisha kwa mwez unalipwa laki tatu wengi watakugomea na kukutukana bila kujua kwamba kwenye kazi ndipo pana zaa kazi mtu yupo lazi alale na kula kwa mama na baba ila anaona ubishoo kushka chaki mbili vijana tunapenda sana starehe kuna watu hapa hasa vijana wapo radhi kila wikiend waende club na wanatumia laki au elfu 50 hyo hela unayoichezea ukiiweka utt kwa miaka mitatu utakuwa wap? tuache kulaumu wachawi ni sisi wenyewe.
 

point nzuri hamna kirahisi duniani uwende kwenye biashara au kilimo changamoto zipo na kingine wabongo ni wabishi mtu yupo kukatisha watu tamaa we endelea kusema haiwezekani alafu wenzako wakiwa matajiri waite FREEMASON
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…