Hivi ndoa ina umuhimu gani zama hizi za dunia ya utandawazi?

Hivi ndoa ina umuhimu gani zama hizi za dunia ya utandawazi?

Ndoa ni kama zilivyo Imani....
Hauhitaji nguvu kuanza kumshawishi mtu aone au asione umuhimu wake.

Anaeamini kuna Mungu anamuomba na mambo yake yananyooka....
Anaeamini katika matunguli anayatumia na mambo yake yanamnyookea....
Anaeamini hakuna Mungu, nae mambo yake yanamnyookea pia...

Vivyo hivyo katika ndoa kuna watu ndoa zao ni uwanja wa vita hauwezi kumuambia ndoa ni amani akaelewa.

Kuna watu ndoa zao ni amani hadi ukimuambia kugombana kupo anaweza asikuelewe watu wanagombanaje.

Haihitajiki nguvu kumshawishi mtu, na huyo mkeo/ mmeo sio wa ndoa zote kuna mwenye garasa, kuna mwenye joker n.k....
 
Kuna watu ndoa zao ni amani hadi ukimuambia kugombana kupo anaweza asikuelewe watu wanagombanaje.
Ndoa za hivi ni EXTINCT. Na hata kwenye mada yangu nimeelezea (aya ya pili).

Mimi Sexless ni kungwi ujue. Naona na kusikia mengi.
 
Mambo yamekuendea mrama kwako usidhan na wengine.
Screenshot_20210630-124212.jpg
 
Ndoa ni kama zilivyo Imani....
Hauhitaji nguvu kuanza kumshawishi mtu aone au asione umuhimu wake.

Anaeamini kuna Mungu anamuomba na mambo yake yananyooka....
Anaeamini katika matunguli anayatumia na mambo yake yanamnyookea....
Anaeamini hakuna Mungu, nae mambo yake yanamnyookea pia...

Vivyo hivyo katika ndoa kuna watu ndoa zao ni uwanja wa vita hauwezi kumuambia ndoa ni amani akaelewa.

Kuna watu ndoa zao ni amani hadi ukimuambia kugombana kupo anaweza asikuelewe watu wanagombanaje.
Haihitajiki nguvu kumshawishi mtu, na huyo mkeo/ mmeo sio wa ndoa zote kuna mwenye garasa, kuna mwenye joker n.k....
Umefunga uzi huu Mkuu.... mleta mada afuate moyo wake unamwambia nini. Achague kusuka au kunyoa...
 
Ndio kama nilivyoandika hapo ndoa kama Imani....
Mbona kama Evelyn Salt unataka kukwepa kutoa majibu halisi kwa kujificha kwenye kichaka cha Imani??

Kama ni imani, tuambie Imani hii inapatikanaje ama inajengwa vipi ili kunusuru mamilioni ya ndoa zilizo mashakani. Karibu
 
Mimi Sexless ni kungwi ujue. Naona nakusikia mengi.
Okay dada/kaka kungwi.... kwanini makungwi wengi huwa wanaachika/hawana ndoa?

Hiyo kazi ya kuhubiri mme anataka hiki anataka hiki, mme kamfanyie hiki mara ifinyie kwa ndani hakuachi, kwanini msifanye nanyie ili msiachwe?
 
Mbona kama Evelyn Salt unataka kukwepa kutoa majibu halisi kwa kujificha kwenye kichaka cha Imani??

Kama ni imani, tuambie Imani hii inapatikanaje ama inajengwa vipi ili kunusuru mamilioni ya ndoa zilizo mashakani. Karibu
Wala sikwepi wala sijifichi kwenye imani...

Ishu yangu ni hivi wewe unaona haina umuhimu ukitoa na sababu zako kama ni watoto utazaa tu, kama ni machangamsho utapata tu upo sawa kabisa wala sikupingi.

Nami kwa upande wangu naiona ina umuhimu sana na sidhani kama nahitaji kukushawishi uuone umuhimu huo nami kuiona ina umuhimu nipo sawa kabisa.
 
Unauliza then unajijibu mwenyewe baadaye unauliza tena

In very short:
  • Tunaomba usitusemee tuliopo kwenye ndoa
  • Ndoa ni zaidi ya vyote unavyoviwaza na si tu kwa ajili ya kuchakachuana
Mwisho, ukitaka kujua huwa ni kwanini tunaoa then endelea kumuomba Mungu umpate wako wa ubani, ndio utanielewa.

'True' marriage is based on 'true' love and nothing else.
 
Kwenye kuchakatana kuna mambo mengi sana ya ulimwengu mwingine hutokea, ukiona kwako kuchakata ni ishu tu kama kutema mate chini just know huna Roho Mtakatifu/uwepo wa Mungu ndani yako, yaan huna tofauti na mnyama. So ndoa ni muhimu......... Ukishindwa kabisa acha na kuchakata.
 
Hayo ni mawazo narrow sana na ya kitoto mno.
NDOA ni muhimu kwa watu wanaojielewa tu, mfano hata wewe wazazi wako wameoana, naongopa?

ndoa ipo ili ujenge familia yenye hadhi na heshima na sio kufanya mingono zembe tu kama ulivyoandka.
ndio ipo ili hata mkipata watoto muwalee pamoja kama baba na mama na sio kama malaya wasaka ngono. hii ni nature inaamua hivi ndio maana hata wanyama huwa wanatulia sehemu moja kama baba na mama.
Na ni tusi kubwa binadamu kufanananishwa alafu kuzidiwa akili na mnyama wa porini.

ndoa ipo ili kuepuka migonjwa ya ngono iliyojaa duniani.
ndoa ipo ili kujenga kizazi cha watu wanaojitambua na maadili then uache alama yako ikiendelea baada ya wewe kuondoka duniani na sio kujenga kizazi cha wafanya ngono na kufikiria ngono muda wote.
ndoa ipo ili kutulia na mtu mmoja ili utumie muda mwingine kufanya mambo mengine ambayo ni productive.
Mkuu au unadhani duniani watu wamekuja kufanya ngono tu? hii ndio sababu wazungu wametuacha mbali kimaendeleo.

mkuu alafu nimegundua kitu kingine kwenye thread yako, wewe ni mtu wa kufuata mkumbo na huna misimamo na ndio sababu ya kuandika hii thread.

kisa umeona kwamba fulani mwenye ndoa anazini hovyo basi na wewe umepata justification ya agenda yako that's childish.

na mkuu mtu mwenye mawazo ya kukataa ndoa sababu ya urahisi wa kupata ngono there's no bloody way ataweza kulea mtoto bali atakuwa analea timebomb.

Na ni mbaya zaidi kwa mwanamke kukataa ndoa sababu yeye ndio atakuwa main subject ambaye atakuwa anatumika na kila mtu just like chinese doll, actually there'll be no difference at all between that woman and the chinese doll.

Wewe hujiulizi kwanini wakati mababu na mabibi wa kipindi hicho wakati wanaishi zama zao kulikuwa hakuna migonjwa ya ngono ya ajabu'ajabu tena inayosambaa hovyo kama leo hii?
mimi nakupa jibu sababu ni ndoa.

Sasa huwezi mkuta mtu mwenye akili zake timamu na uwezo wa kufikiri uliokamilika aseme hakuna sababu ya NDOA eti sababu siku hizi ni rahisi kupata mtu wa kufanya naye uchafu wa ngono zembe. really?

Mkuu usitafute justification ya kufanya ngono zembe wewe jiamini tu na misimamo yako at your own risk.
 
Hazina umuhimu kwanza zimeleta mambo haya
1.kufa Kwa magonjwa ya zinaa
2.kuwa maskini
3.kuwa na msongo Wa mawazo
really? yaani ukikaa na mtu mmoja ukatulia then miraculously mnakufa na magonjwa ya ngono?

unapata vipi magonjwa ya ngono kama umetulia na mtu mmoja?
 
Back
Top Bottom