- Thread starter
- #61
Mkuu umeandika maandishi mengi sana lkn umeishia kuzunguka mbuyu wa mada yangu.Sasa huwezi mkuta mtu mwenye akili zake timamu na uwezo wa kufikiri uliokamilika aseme hakuna sababu ya NDOA eti sababu siku hizi ni rahisi kupata mtu wa kufanya naye uchafu wa ngono zembe. really?
Kwanza umekubali kwamba siku hizi kumpata mtu wa kuchakatana ni rahisi kama kupumua. Na ukasema ndiyo sabb magonjwa ni mengi zaidi.
Pili umetaja sabb za kubuni kuhalalisha umuhimu wa ndoa.
1. Heshima. Nani anaheshimika kwasabb ya ndoa? Au heshima unayoitaja hapa ni tofauti na ninayoifahamu? Wewe na Anna Makinda ambaye hajawahi kuolewA nani anaheshimika? Wewe na Nancy Pelos spika wa bunge la Marekani nani anaheshimika?
Kuna michepuko kibao ya mume na/au mke wa mtu. Hiyo heshima ni ipi?
2. Kulea watoto kimaadili. Umedai mtoto anayelelewa na baba au mama peke yake ni time bomu. Hapa pia hujafanya utafiti hivyo huna haki ya kuja na hitimisho hili.
Watu wengi waliofanya makubwa dunia hii ni ama yatima au walio lelewa na mzazi mmoja. Mfano Isaack Newton, Trump, Hitler, Kanumba, Diamond, Zuchu, n.k.
Rudi kajipange uje upya. Na nikutahadharishe kuwa unaongea na mtu mwenye akili nene. Hivyo njoo na sababu zenye shibe.