- Thread starter
- #81
Nadhani wote tunaongea jambo moja kwa lugha approach tofauti.Mungu Mwenyezi alishaweka utaratibu na wanadamu hatuna budi kuufuata, swala la mchepuko ni tabia zile la dhambi ya kurithi kutoka kwa Adam kukataa maagizo ya Mungu na kumtii shetani. Uchepukaji ni uchafu, uzinzi mbele za Mungu. Linabaki uutii Mungu au adui shetani?
Wewe unasisistiza watu wakatae maagizo ya Mungu ya kutokuzini. Unataka watu wamtii Mungu kwa kuoa lkn wakichepuka hilo kwako si tatizo Sana ili mradi wameoa.
Mm nasisitiza kwamba kwa kuwa watu wameshindwa kumtii Mungu kwa kutoacha dhambi ya kuzini baada ya kuoa, bora wasioe kabisaa. Kwasabb kwa kuoa na Kisha kuzini wankuwa vuguvugu. Na Mungu hapendi mtu vuguvugu.
Kuna maandiko yanasema " Ni heri mtu kuwa moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu maana nitamtapika".
Mkuu unaongea na mtu mwenye akili nene.