Hivi neno "Uchwara" ni Lissu alilianzisha?

Mzuka wana JF!

Ni matumaini yangu wote wazima wa afya na mwenyezi Mungu anaendelea kutujalia uzima, amani, nguvu, afya na faraja wakati huu mgumu wa kumpoteza ndugu yetu Bernard Kamilius Membe.

Moja kwa moja kwenye mada. Hivi hil neno la kiswahili UCHWARA mwanzilishi ni brother Tundu Lissu?

Nakumbuka wakati hule alipolitamka kwa mara ya kwanza dikteta uchwara likashika kasi sana na kuwa rasmi.

Jiwe alimaindi akakataza lisitumike.
Kabla ya hapo mimi sikuwahi sikia sehemu yoyote
 
Inaelekea wewe ni mtoto wa juzi. Hili neno uchwara ni la muda mrefu wakati wa Nyerere na asiasa za ujamaa.
Kulikuwa na mabepari......watu wenye hela sana sana especially USA and Western countries, hao walikuwa mabepari.
2. Matajiri wa nchi zilizobaki hasa Tanzania kulikuwa ma watu wenye pesa lakini huwezi kuwaita mabepari per se, bali MABEPARI UCHWARA
Kwa hiyo uchwara ni kitu ambacho sio kamili.
 
Mzuka wana JF!

Ni matumaini yangu wote wazima wa afya na mwenyezi Mungu anaendelea kutujalia uzima, amani, nguvu, afya na faraja wakati huu mgumu wa kumpoteza ndugu yetu Bernard Kamilius Membe.

Moja kwa moja kwenye mada. Hivi hil neno la kiswahili UCHWARA mwanzilishi ni brother Tundu Lissu?

Nakumbuka wakati hule alipolitamka kwa mara ya kwanza dikteta uchwara likashika kasi sana na kuwa rasmi.

Jiwe alimaindi akakataza lisitumike.
Mzuka ndiyo nini?
Screenshot_20230514-140349_Chrome.jpg
Screenshot_20230514-140328_Chrome.jpg

Mwaka huu nitahakikisha nina deal kikamilifu na nyie wachafuzi wa Lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
 
Yaani lissu aanzishe neno uchwara?
naliskia toka nimezaliwa
 
Neno uchwara lipo kitambo sana. Ni neno lenye kumaanisha kitu kisicho halisi, chenye kufanana na kitu halisi. Lissu alipenda kumuita yule bwana dikteta uchwara, yaani huyo bwana alipoanza kuonesha utawala wa kiimla alikuwa anaelekea kuwa dikteta kamili kutoka kwenye dikteta uchwara. Neno alilolianzisha Lissu ni mwendazake, tena kwa huyo huyo hasimu wake wa kisiasa baada ya kuondoka duniani. Naona wakenya nao wameanza kulitumia neno mwendazake
 
Mzuka wana JF!

Ni matumaini yangu wote wazima wa afya na mwenyezi Mungu anaendelea kutujalia uzima, amani, nguvu, afya na faraja wakati huu mgumu wa kumpoteza ndugu yetu Bernard Kamilius Membe.

Moja kwa moja kwenye mada. Hivi hil neno la kiswahili UCHWARA mwanzilishi ni brother Tundu Lissu?

Nakumbuka wakati hule alipolitamka kwa mara ya kwanza dikteta uchwara likashika kasi sana na kuwa rasmi.

Jiwe alimaindi akakataza lisitumike.
Msemo alioanzisha ni "Dikteta uchwara" ila "Uchwara" lilikuwepo.
 
Neno uchwara lipo kitambo sana. Ni neno lenye kumaanisha kitu kisicho halisi, chenye kufanana na kitu halisi. Lissu alipenda kumuita yule bwana dikteta uchwara, yaani huyo bwana alipoanza kuonesha utawala wa kiimla alikuwa anaelekea kuwa dikteta kamili kutoka kwenye dikteta uchwara. Neno alilolianzisha Lissu ni mwendazake, tena kwa huyo huyo hasimu wake wa kisiasa baada ya kuondoka duniani. Naona wakenya nao wameanza kulitumia neno mwendazake
Kwa kuweka rekodi sawa...
Samia akihutubia msibani kitaifa alilitamka sana...mwendazake je kabla Lissu alilitamka kwrli!
 
Neno Uchwara lipo kitambo sana wote tumelikuta Mfano mkwara Uchwara, utisho uchwara, lipo kitambo sana sana, ndiomana kwa umri wake lissu amelitumia kama msamiati anaoujua kitambo
 
Rostam Aziz: Najiuzulu Ubunge wa Igunga nimechoshwa na Siasa Uchwara

Hapo ndipo Umaarufu wa " Uchwara" ulianza japo ni Neno la kitambo sana
Hapana neno hili ni la Nyerere wakati wa Ujamaa. Alichukia mabepari na kwa kuwa Tanzania kulikuwa na vi-bepari ambao huwezi kuwaita mabepari, basi akawaita mabepari Uchwara.....kama alivyosema hela yetu ni hela ya madafu...kununua madafu na si vitu toka nje enzi hizo...
 
Back
Top Bottom