Hivi ni Demokrasia gani inayopiganiwa na vyama vya Upinzani? Sioni Chama cha kukipa Nchi

CCM ni Chama ambacho kina misingi na utaratibu wa namna kinavyojiendesha ndio maana utaona viongozi wanaachiana madaraka kwa taratibu hizo.

Utasikia mtu kapita kwa asilimia 100, bila kupingwa etc.. ni taaratibu zao na Wanachama wao wanazipenda.

Huku kwetu upinzani Mtu akishaanzisha Chama au Kuwa kiongozi basi yeye atakuwa kila kitu .hakuna maamuzi ya maana yatafanyika bila yeye kuwepo.

Kuna wenyeviti wana zaidi ya miaka Ishirini madarakani na bado wanaendelea kuongoza Chama ,Swali mtu kama huyu akipewa Nchi atakubali toka Madarakani?

Kuna Chama mtu kajitafutia cheo anaitwa Kiongozi Mkuu yote hiyo vyeo vingine vinavyobadilika yeye asiguswe ,swali je hawa watu ni wazalendo au anaangalia Maslahi yake tu?

Kuna vyama Nenda rudi mgombea nafasi ya Urais ni huyo kiongozi wa Chama kana kwamba hakuna mtu mwingine wa kuweza simama.

Hivi ni demokrasia ipi iko Upinzani ? Mbona miundo yao ya uongozi na mbadilishano wa madaraka haueleweki na hauwi wazi?

Mimi ni mpinzani ila naona ni bora CCM iendelee kuwepo Madarakani mbali na kwamba imetufanya Maskini wa kutupwa kwa kila siku kutujazia Mafisadi na Kukosa Maono kwa Taifa kuliko sisi Wapinzani tunao hubiri kitu ambacho hakipo kwenye vyama vyetu.
Unafuatilia uchaguzi wa Kenya?
Kuna chama hata chenye miaka mi 5 pale?
Kwa hiyo wakenya wakipiga kura ili mradi wasubir ukomavu wa kisiasa?
Miaka 60 chini ya ccm . Watu wanakunywa maji ya matope huko kusini?
Bwana kihongosi acha kujitoa nguoo
 
Mpaka tunaingia mfumo wa vyama vingi 1992 CCM ilikuwa na miaka 15 ikiongozwa na Mwalimu Nyerere ambaye ndiye aliyeianzisha baada ya kuiunganisha TANU na ASP na kuunda CCM. Na kabla ya CCM alikuwa ameiongoza TANU kwa miaka 23 hivyo ameviongoza vyama vya TANU na CCM kwa miaka 38. Sikumbuki kumuona mwanaTanu au CCM akihoji pamoja na vyama kumiliki serikali kwa muda wote huo. Leo mnavishangaa vyama vya upinzani eti havibadilishi viongozi wake, unayajua malengo ya kuanzishwa kwake?
Wanataka wafanye kama NCCR ?
WAPUUZI? WAKAFANYE KWA MREMA NA LIPUMBA KWANZA
 
Na kwa vile Nyerere alitawala nchi kwa miaka 24 na hakulalamikiwa, basi leo haina shida mtu akitawala miaka 24!!?

Uzuri wa chama unaweza kuhama kama hukubaliani na utaratibu, ama unaanzisha chama chako kabisa ili kifuate unavyotaka.
 
CCM ni Chama ambacho kina misingi na utaratibu wa namna kinavyojiendesha ndio maana utaona viongozi wanaachiana madaraka kwa taratibu hizo.

Utasikia mtu kapita kwa asilimia 100, bila kupingwa etc.. ni taaratibu zao na Wanachama wao wanazipenda.

Huku kwetu upinzani Mtu akishaanzisha Chama au Kuwa kiongozi basi yeye atakuwa kila kitu .hakuna maamuzi ya maana yatafanyika bila yeye kuwepo.

Kuna wenyeviti wana zaidi ya miaka Ishirini madarakani na bado wanaendelea kuongoza Chama ,Swali mtu kama huyu akipewa Nchi atakubali toka Madarakani?

Kuna Chama mtu kajitafutia cheo anaitwa Kiongozi Mkuu yote hiyo vyeo vingine vinavyobadilika yeye asiguswe ,swali je hawa watu ni wazalendo au anaangalia Maslahi yake tu?

Kuna vyama Nenda rudi mgombea nafasi ya Urais ni huyo kiongozi wa Chama kana kwamba hakuna mtu mwingine wa kuweza simama.

Hivi ni demokrasia ipi iko Upinzani ? Mbona miundo yao ya uongozi na mbadilishano wa madaraka haueleweki na hauwi wazi?

Mimi ni mpinzani ila naona ni bora CCM iendelee kuwepo Madarakani mbali na kwamba imetufanya Maskini wa kutupwa kwa kila siku kutujazia Mafisadi na Kukosa Maono kwa Taifa kuliko sisi Wapinzani tunao hubiri kitu ambacho hakipo kwenye vyama vyetu.

Kuna haja gani ya chama kuwa na misingi, lakini kinategemea wizi wa kura kukaa madarakani kwa shuruti? Huu ujinga kuwa kuwa eti CCM kinaendeshwa kitaasisi mmekaririshana, basi mnamwambia kila mtu mkidhani kila mmoja anaelewa hizo hisia zenu.
 
Mkuu ujue kuna viongozi wa Vyama wamefanya hivyo vyama kama vyao na familia zao tofauti na CCM
 
Umeambiwa Nyerere alitawala TANU na Ccm kwa miaka zaidi ya 30 akiwa mwenyekiti, je hivyo vyama vilikuwa vya familia yake na nani?
 
Hiyo ilikuwa kabla ya Vyama vingi ambapo tunahubiri Demokrasia
 
Kama ingekuwa kweli mnaheshimu vyama vingi leo hii CCM haikupaswa kuendelea kukaa madarakani kwa wizi wa kura. Au demokrasia ya vyama vingi ni wenyeviti wa vyama vya upinzani kutoka mapema tu madarakani?
 
Huwezi kuwapa watu Nchi ambao hawana uwezo wa kuongoza nchi hata kama wameshinda
 
CCM ni Chama ambacho kina misingi na utaratibu wa namna kinavyojiendesha ndio maana utaona viongozi wanaachiana madaraka kwa taratibu hizo.

Utasikia mtu kapita kwa asilimia 100, bila kupingwa etc.. ni taaratibu zao na Wanachama wao wanazipenda.

Huku kwetu upinzani Mtu akishaanzisha Chama au Kuwa kiongozi basi yeye atakuwa kila kitu .hakuna maamuzi ya maana yatafanyika bila yeye kuwepo.

Kuna wenyeviti wana zaidi ya miaka Ishirini madarakani na bado wanaendelea kuongoza Chama ,Swali mtu kama huyu akipewa Nchi atakubali toka Madarakani?

Kuna Chama mtu kajitafutia cheo anaitwa Kiongozi Mkuu yote hiyo vyeo vingine vinavyobadilika yeye asiguswe ,swali je hawa watu ni wazalendo au anaangalia Maslahi yake tu?

Kuna vyama Nenda rudi mgombea nafasi ya Urais ni huyo kiongozi wa Chama kana kwamba hakuna mtu mwingine wa kuweza simama.

Hivi ni demokrasia ipi iko Upinzani ? Mbona miundo yao ya uongozi na mbadilishano wa madaraka haueleweki na hauwi wazi?

Mimi ni mpinzani ila naona ni bora CCM iendelee kuwepo Madarakani mbali na kwamba imetufanya Maskini wa kutupwa kwa kila siku kutujazia Mafisadi na Kukosa Maono kwa Taifa kuliko sisi Wapinzani tunao hubiri kitu ambacho hakipo kwenye vyama vyetu.
@Zitto alipomjaribu MBOWE bila mafanikio, basi yeye akaamua kujiita Kiongozi Mkuu asiyehojika!
 
Back
Top Bottom