Hivi ni jibu gani uliwahi mpa mtu PM akakuchunia mazima?

Hivi ni jibu gani uliwahi mpa mtu PM akakuchunia mazima?

Hi guys,

Nimekumbuka hii ujinga Leo nikaishia kucheka.! Kuna wale watu huwa wanakuja PM kwa mbwembwe kibao, mrembo mrembo nyingi mara mtoto mzuri, (wanadanganyika na avatar obviously) lakini vile huja kupotea ndo wanashangaza na jukwaani unawaona unaishia tu kucheka hiiii'...!!

Huyu wa kwanza alikuja mbwembwe kibao, akauliza umri nikajibu 41, hajawahi kurudi na hata hiyo PM hakujibu, akajionea tu hii kikongwe nimetokana nayo wapi? akatoka ndukii akaniachia mpaka vumbi walaqhi'..!!

Huyu mwingine naye kaja na mbwembwe kama ngombea wa uenyekiti wa Vicoba, akataka kujua nipo wapi, nikamtajia kijiji ambacho hakipo hata kwenye ramani ya Tanzania, akajibu tu 'I thought upo dar nikutafute, nice day', akanipotezea mazima, nikaona ile namna wa mikoani hutengwa waziwazi, hahaa.!!

Huyu mwingine naye eti akaniongelesha busara siku mbili tatu,story za hapa na pale, baadaye akataka kujua nafanya kazi gani, nikamjibu mkulima, I swear mpaka Leo akanipotezea na ile PM hakujibu na huku jukwaani tunakutana zetu kiroho safi,
Hivyo kila nikionaga ID ya miminimkulimaakachekasana naishiaga tu kucheka, huwa natamani iwe 'miminimkulimaetiakanichunia'..!

Hivii huwa mnakutana nahizi sarakasi ama hizi ni kwa ajili yetu tu sisi wabarikiwa?

#nohardfeelings# tupunguze tu stress za corona,
Stay safe guys..!!
Wangejua ulivyo mrembo wangejutia hilo vumbi [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23] majibu yangu ya ndiyo hapana.. short and clear .. yalimchosha mtu yeye alikuwa anataka akiuliza swali nijielezee..khaaa!!..akanichunia mazima hadi jukwaani akanilia buyu 🤣🤣🤣🤣

yupo kama mimi ,sipendi hayo majibu, yani mwanaume mzima niandike angalau maneno 10 afu nijibiwe NDIO kama nitatuma tena texts basi hiyo siku polepole anakuwa mwenyekiti wa CCM


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema ule ukweli toka ndani ya mtima kuna kifaa hua nakielewa humu ndani dada angu[emoji23][emoji23] Ila hyo ya kukifata PM hahahaa, ndo sijawahi waza.
Hua namuombea tu kimoyomoyo siku akanyage mdudu ajikute piemuni mwangu[emoji23][emoji23]
Anaweza Kanyaga mwiba na kuishia kusonya [emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanawake wakati mwingine ni vigumu kuwaelewa, kuna siku jamaa fulani job nimempa namba ya mfanyakazi mwenzetu wa kike maana aliiomba kwa sababu ana shida ya haraka
basi jamaa akampigia huyo mwanamke akamsalimia na kumwambia “samahani naomba namba ya fulani” yule mwanamke akajibu “nani kakupa namba yangu”


Sent using Jamii Forums mobile app
Naogopa kujipendekeza au Kulazimisha mawasiliaono.
Nikishaona unajibu text kwa Maneno mawili hata kama nilikupa status gani, naanza kukuita mkuu au kiongozi😀😀
 

Attachments

  • IMG_20200410_200131.jpg
    IMG_20200410_200131.jpg
    35.1 KB · Views: 1
Siku zote naamini kama mwanamke yupo serious hata pm yake ikiwa na watu elf na ushee haitokuwa na madhara yoyote but kama ndo ile tunaita kutafuta unachokosa hapo sasa ndo itakuwa shughuli kama hizi😂😂
Hell yeah'..!!
Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee.!!.
Usichukulie hata siku moja maisha ya JF seriously.!!
 
Back
Top Bottom