Hivi ni jibu gani uliwahi mpa mtu PM akakuchunia mazima?

Hivi ni jibu gani uliwahi mpa mtu PM akakuchunia mazima?

Hi guys,

Nimekumbuka hii ujinga Leo nikaishia kucheka.! Kuna wale watu huwa wanakuja PM kwa mbwembwe kibao, mrembo mrembo nyingi mara mtoto mzuri, (wanadanganyika na avatar obviously) lakini vile huja kupotea ndo wanashangaza na jukwaani unawaona unaishia tu kucheka hiiii'...!!

Huyu wa kwanza alikuja mbwembwe kibao, akauliza umri nikajibu 41, hajawahi kurudi na hata hiyo PM hakujibu, akajionea tu hii kikongwe nimetokana nayo wapi? akatoka ndukii akaniachia mpaka vumbi walaqhi'..!!

Huyu mwingine naye kaja na mbwembwe kama ngombea wa uenyekiti wa Vicoba, akataka kujua nipo wapi, nikamtajia kijiji ambacho hakipo hata kwenye ramani ya Tanzania, akajibu tu 'I thought upo dar nikutafute, nice day', akanipotezea mazima, nikaona ile namna wa mikoani hutengwa waziwazi, hahaa.!!

Huyu mwingine naye eti akaniongelesha busara siku mbili tatu,story za hapa na pale, baadaye akataka kujua nafanya kazi gani, nikamjibu mkulima, I swear mpaka Leo akanipotezea na ile PM hakujibu na huku jukwaani tunakutana zetu kiroho safi,
Hivyo kila nikionaga ID ya miminimkulimaakachekasana naishiaga tu kucheka, huwa natamani iwe 'miminimkulimaetiakanichunia'..!

Hivii huwa mnakutana nahizi sarakasi ama hizi ni kwa ajili yetu tu sisi wabarikiwa?

#nohardfeelings# tupunguze tu stress za corona,
Stay safe guys..!!
Kama Nina Nia ya kukutongoza nakuja directly TU Kama Sina ndio hapo braa braa nyingi TU tupige story siku ziende na s kila anaekuja pm anataka akugegede wengne hupenda muunge urafiki na kushauriana

Sasa mwingne akiombwa namba anajua atatekwa au kukegedwa

kilicho akilini kitumie
 
Baada ya kupitia comments zilizotangulia,
Nimegundua sio kuwa wadada hawataki pm, bali kuna pm za watu wangewish wazipate ila hawaji, au wakija sio kama walivyotegemea, na wengine wanaoenda pm wanatumia wrong approach,
Basi wanaume wazangu tumieni approach nzuri, na ukikataliwa pm usimtukane, chill na yaishie hukohuko,
Kwa wadada wale mnaowish wawafuate pm na hawaji, basi tumieni ile ladies first
 
...WENGINE PM ZETU TUNASHARE MAVITU YA KIBAHARIA ZAIDI (LINKS) WAJAUBA WANAELEWA HAHA ILA HATUHANGAIKI NA SKETI ZA HUKU

HAHAHA YANI MKIFATWA 80% WENGI WANATAKA PAPUCHI HIVYO MKIWAPA MAJIBU TOFAUTI NA MATARAJIO YAO LAZIMA WASEPE VUMILIENI TU
 
Nilikuwa nakutafuta sana.

Waswahili wanasema kama ni sheikh basi alibadiri rangi ya kanzu watu wakampotea.

Sure nilikutafuta mno.
Mpango upo pale pale ni wewe tu mama.
Haha,
Kidizaini umeanza kunichocha, nimependa hako ka msemo ka waswahili.. Basii mwenzio nipo Jana, Leo na hata kesho.!!

Afadhali kama ka mpango bado ni endelevu.. Ngoja tu wafungue vyuo harakati zianze.!!
 
Hahahahaa. Marhabaaaa nimeipokea shikamoo yako mdogo. 🙈🙈🙈

Kama mimi tu mdogo wangu wajua vile nakupendaga pia. 😍
dada naomba kukuambia kuwa hapa nimesharinga na kunata and indeed you're the reason, kesho kama hata nitakusalimia sijui.!
 
Kama Nina Nia ya kukutongoza nakuja directly TU Kama Sina ndio hapo braa braa nyingi TU tupige story siku ziende na s kila anaekuja pm anataka akugegede wengne hupenda muunge urafiki na kushauriana

Sasa mwingne akiombwa namba anajua atatekwa au kukegedwa

kilicho akilini kitumie
Nakuelewa,
Huwa naamini hivyo pia, si kila anayekuja anakuja kwa nia ovu.! Watu wazuri wapo hivyo na wabaya pia.!!
 
Baada ya kupitia comments zilizotangulia,
Nimegundua sio kuwa wadada hawataki pm, bali kuna pm za watu wangewish wazipate ila hawaji, au wakija sio kama walivyotegemea, na wengine wanaoenda pm wanatumia wrong approach,
Basi wanaume wazangu tumieni approach nzuri, na ukikataliwa pm usimtukane, chill na yaishie hukohuko,
Kwa wadada wale mnaowish wawafuate pm na hawaji, basi tumieni ile ladies first
Absolutely,
Umeongea kweli tupu, kila siku nalia na 'approach'..!! Hakuna PM isiyojibiwa ukitumia approach nzuri.! Wafundishe hao wenzio baadhi yao hawajielewi kiukweli.!
 
...WENGINE PM ZETU TUNASHARE MAVITU YA KIBAHARIA ZAIDI (LINKS) WAJAUBA WANAELEWA HAHA ILA HATUHANGAIKI NA SKETI ZA HUKU

HAHAHA YANI MKIFATWA 80% WENGI WANATAKA PAPUCHI HIVYO MKIWAPA MAJIBU TOFAUTI NA MATARAJIO YAO LAZIMA WASEPE VUMILIENI TU
Wafike salama waendako, mwisho wa siku maisha ni lazima yaende walaqhi'.!!
 
Bila shaka hao wanakuwa ni wageni. Unaanzaje tu out of nowhere kuingia PM ya mdada humu ? Kuna stages za kuingia PM ya mdada ili usikutane na kikwazo. Kwanza anza kulike comments zake, kucomment comments zake, kubaliana na hoja zake. Taratibu tu ataanza zoea jina lako. Siku hamishia moja ya mada mlizochangia wote PM, taratibu mnageuka washikaji.
Hahaha..!
Mkuu una mbinu walaqhi'.! Naomba waige mfano wako.!!
 
Back
Top Bottom