Hivi ni kwanini hizi shule za English medium wanafunzi hawachapwi viboko?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wakuu ni kwanini hizi shule wanazojifunza kwa kutumia kiingereza huwa hamna viboko? Inamaana ukiwa unajifunza kwa kiingereza unaweza kwenda bila viboko? Nidhamu ya wanafunzi wanaosoma hizi shule ikoje?
 
Sema baadhi nyingi viboko ndivyo vinawafanya wawe na nidhamu na adabu ya kusoma.

Shule za serikali ndiko hakuna viboko na matokeo ya ufaulu huonekana wazi yako sivyo sababu toto la kiswahili elimu hukolea likitandikwa viboko.
 
sema baadhi nyingi viboko ndivyo vinawafanya wawe na nidhamu na adabu ya kusoma

Shule za serikali ndiko hakuna viboko na matokeo ya ufaulu huonekana wazi yako sivyo sababu toto la kiswahili elimu hukolea likitandikwa viboko
Yaani nachukia sana mtu anayeamini katika viboko namuona kama hayupo sawa upstairs.

Viboko anachapwa mnyama sio binadamu. Adhabu yoyote yakuumiza mwili ni adhabu ya kikatili sana.

Viboko vingekuwa vinasaidia basi taifa hili lingeongoza kwa wasomi wa hali ya juu badala yake ni kinyume.

Kwanini hatujiulizi shule ama nchi ambazo ni marufuku kutumia viboko mbona ufaulu upo vizuri mno na ukimuweka na mtoto aliyesoma kwa viboko ni tofauti kabisa.

Tuache kushabikia viboko ni unyama na mtu kama wewe siku mwanao akicharazwa viboko ikatokea akafariki au kupata ulemavu wa kudumu utakuwa wa kwanza kutaka adhabu ikomeshwe mara moja.
 
Wakuu ni kwanini hizi shule wanazojifunza kwa kutumia kiingereza huwa hamna viboko? Inamaana ukiwa unajifunza kwa kiingereza unaweza kwenda bila viboko? Nidhamu ya wanafunzi wanaosoma hizi shule ikoje?
Baadhi ya English Medium za ''uchochoroni'' wanachapa tena vibaya sana. I mean hizi za ada inayocheza around sh. milioni 2 mpaka 3. Ambazo hawachapi ni zile za bei kubwa na huko wanasoma watoto wa vigogo. Kitu ambacho naweza kukisema bila shaka yoyote ni kuwa Nchi zilizoendelea karibu zote hawachapi watoto viboko mashuleni na watoto wao wana akili sana kulinganisha na hawa wa kwetu.
 
Yaani nachukia sana mtu anayeamini katika viboko namuona kama hayupo sawa upstairs.

Viboko anachapwa mnyama sio binadamu. Adhabu yoyote yakuumiza mwili ni adhabu ya kikatili sana.

Viboko vingekuwa vinasaidia basi taifa hili lingeongoza kwa wasomi wa hali ya juu badala yake ni kinyume.

Kwanini hatujiulizi shule ama nchi ambazo ni marufuku kutumia viboko mbona ufaulu upo vizuri mno na ukimuweka na mtoto aliyesoma kwa viboko ni tofauti kabisa.

Tuache kushabikia viboko ni unyama na mtu kama wewe siku mwanao akicharazwa viboko ikatokea akafariki au kupata ulemavu wa kudumu utakuwa wa kwanza kutaka adhabu ikomeshwe mara moja.
Unawaambia hivyo watanzania watakulewa? Ni wachache sana. Mimi ni mmoja ya watu wanaolaani sana sana viboko kwa watoto iwe nyumbani au shuleni. Mbona Ulaya watoto wana akili sana na hawachapwi? Viboko vina madhara makubwa sana. Usione aina ya viongozi tulionao ufikiri ni bahati mbaya. Ni matokeo ya malezi ya utoto. Kuna rais mmoja kati ya nchi za Afrika Mashariki (jina kapuni) inaonekana malezi yake ya utoto yalikuwa mabaya sana na huenda alipigwa sana viboko. Ni mkatili, siyo mstaarabu na anaamini sana kwenye kupiga na kutumia nguvu bila akili. Imefikia mahali anamwambiwa waziri wa michezo eti timu zikifungwa fungwa tena hovyo atakiona cha moto. Hivi kweli hata mpira nao ni maguvu? Hajui kuwa wachezaji huandaliwa tangu wakiwa wadogo?
 
Tema mate chini mkubwa, Fanya utafiti halafu utupe mrejesho.
Nimefanya utafiti mkuu, nimeona hili suala. Kwanza huwezi kuta mwalimu anatembea na kiboko au anaingia darasani na viboko. Nenda hizi international school kama IST, hawa nafikiri hata kuwafokea hairuhusiwi.

Nakumbuka shule niliyosoma, mwalimu alikuwa anatuagiza twende na mianzi ya kuchapia, fimbo zingine zilionekana haziumi. Wakati nipo vidudu nilichapwa na magome ya miti, vidudu!
 
Unawaambia hivyo watanzania watakulewa? Ni wachache sana. Mimi ni mmoja ya watu wanaolaani sana sana viboko kwa watoto iwe nyumbani au shuleni. Mbona Ulaya watoto wana akili sana na hawachapwi?
Ulaya Wangekuwa na akili wangekubali ushoga,usagaji na ndoa za jinsia moja na kufundisha watoto kuanzia chekechea?
Viboko vimesaidia watoto wa kiafrika vichwa vyao kukaa sawa
 
Unadhani ni nchi zote za kiAfrika zina adhabu ya viboko? Nyie wazee wa miaka hiyo mmelishwa matango pori sana mnaamini kila mnachoambiwa.

Mbona hapa hapa Bongo kuna mashoga kibao na wamepitia vipigo huko mashuleni.
 
Hata mtoto wa Raisi Magufuli, Kikwte, au Ndalichako hawakuchapwa shuleni, lkn hawataki kuondoa viboko kwenye Shule za Umma, Ubinafsi tu, ...
Uko sahihi kabisa mkuu. Mtoto wa Magufuli Jeremiah amesoma na mpwa wangu pale Feza Primary School Kawe hakuna adhabu ya viboko wala nini zaidi ukifanya kosa unapewa warning letter tu.

Mtoto wa Kikwete hadi sasa ninapoongea yupo shule moja tena na huyu mpwa wangu hakuna adhabu ya viboko na shule hizo ndo zinaongoza kitaifa.

Sisi waAfrika sijui tuna matatizo gani wakati wakubwa wao hawataki watoto wao wachapwe sisi tunashangilia watoto wetu ndo wachapwe.
 
Unadhani ni nchi zote za kiAfrika zina adhabu ya viboko? Nyie wazee wa miaka hiyo mmelishwa matango pori sana mnaamini kila mnachoambiwa.

Mbona hapa hapa Bongo kuna mashoga kibao na wamepitia vipigo huko mashuleni.
BIBLIA imeagiza wazi kabisa viboko riksa kwa mtoto.Biblia sio kitabu cha matango pori ni maagizo ya Mungu

Mathayo 23:13 inasema Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
 
Unawaambia hivyo watanzania watakulewa? Ni wachache sana. Mimi ni mmoja ya watu wanaolaani sana sana viboko kwa watoto iwe nyumbani au shuleni. Mbona Ulaya watoto wana akili sana na hawachapwi? Viboko vina madhara makubwa sana. Usione aina ya viongozi tulionao ufikiri ni bahati mbaya. Ni matokeo ya malezi ya utoto. Kuna rais mmoja kati ya nchi za Afrika Mashariki (jina kapuni) inaonekana malezi yake ya utoto yalikuwa mabaya sana na huenda alipigwa sana viboko. Ni mkatili, siyo mstaarabu na anaamini sana kwenye kupiga na kutumia nguvu bila akili. Imefikia mahali anamwambiwa waziri wa michezo eti timu zikifungwa fungwa tena hovyo atakiona cha moto. Hivi kweli hata mpira nao ni maguvu? Hajui kuwa wachezaji huandaliwa tangu wakiwa wadogo?
Huo ndo ukweli mkuu. Hata hawa hapa wanaoamini katika viboko sio kwamba ni akili zao bali ni athari za kisaikolojia hivyo imewaingia akilini kwamba bila viboko hakuna elimu.

Viboko vinawaathiri sana watoto kisaikolojia.
 
Uko sahihi kabisa mkuu. Mtoto wa Magufuli Jeremiah amesoma na mpwa wangu pale Feza Primary School Kawe hakuna adhabu ya viboko wala nini zaidi ukifanya kosa unapewa warning letter tu.

Mtoto wa Kikwete hadi sasa ninapoongea yupo shule moja tena na huyu mpwa wangu hakuna adhabu ya viboko na shule hizo ndo zinaongoza kitaifa.

Sisi waAfrika sijui tuna matatizo gani wakati wakubwa wao hawataki watoto wao wachapwe sisi tunashangilia watoto wetu ndo wachapwe.

Ni ubinafsi na uchoyo, angalia yule Mkuu wa Mkoa au sijui Wilaya sikumbuki sawa sawa Mkoani Mbeya alivyowapiga watoto wa wenzie na Magufuli akamsifia, lkn mtoto wake Magufuli kaficha private school, na Magufuli anapinga kuondolewa kwa adhabu ya viboko kwa watoto wa wengine, kuna kipindi Serikali ilitaka kuondoa Magufuli na wakubwa wenzake wakapinga, lkn watoto wao hawaguswi, watoto wa wengine wanapigwa kama wanyama wengine mpaka wanapoteza maisha kama kule Mara nafikiri.

Dunia nzima imeshaachana na huu ukatili hata hapo Kenya nafikiri na Uganda pia hawapigi tena watoto kama sisi, Tanzania watu ni sadists, mtu anapiga mtoto mpaka anavunja mkono au hata kumuua kabisa, ...
 
Back
Top Bottom