Hivi ni kwanini mzazi yupo radhi akusomeshe mpaka PhD lakini asikupe mtaji wa kufanya biashara?

Hivi ni kwanini mzazi yupo radhi akusomeshe mpaka PhD lakini asikupe mtaji wa kufanya biashara?

berylyn

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2021
Posts
877
Reaction score
2,618
Unakuta mzazi anakwambia, "Mimi nitakusomesha mpaka pale utakaposema basi" lakini kukupa mtaji heh utasubiri sana.

Mzazi atajitutumua hata Kama ada ni kubwa atailipa hivyo hivyo. Unaweza mwambia mzee, hiyo pesa badala ya kunipeleka Feza Schools, unaonaje upatie nifungue biashara? Atagoma, atakwambia mimi kazi yangu ni kukusomesha.

Siri ni nini? Kwa nini ipo hivyo? Kwanini huwa wanagoma?
 
Serikali inayokupa boom na kukopesha ada. Je ukimaliza chuo inakupa startup package?

Ukiwa na mawazo aina hii maana yake ulienda shule lakini haukuelimika
 
Primitive..

Enzi Zao Mwenye Elimu Anaheshimiwa Zaidi Ya Mwenye Pesa..
Hawajui Dunia Imebadilika..
Hapa nakuelewa mkuu, kumbe ndo maana wanang'ang'ania kusomesha watoto , loh. Sikuhizi wenye pesa ndo wanasikilizwa[emoji3]. Siyo wenye elimu. Ndo maana ukiwa una degree lako afu huna pesa hamna mtu anakusikiliza. Ndo maana mtu akimaliza chuo afu asiwe na pesa anaona nyumbani siyo mahala salama, anadharaulika na elimu yake.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Wazazi wengi hali za maisha ni kawaida
Akupe labda 20mil ufilisike anapatawapi nyingine kukuboost urudi kwenye mstari
Hivyo anaona bora upate elimu unaweza ajiriwa ukapata na mtaji kupitia ajira
 
Uaminifu,wazazi wachache sana wanawaamini watoto wao. Tangu primary hadi chuo unakuta kijana hajawahi pewa pesa cash akalipe ada either shule au bank[emoji23][emoji23][emoji23]sembuse kukupa pesa mtaji wa biashara ngumu sana
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom