Hivi ni kwanini mzazi yupo radhi akusomeshe mpaka PhD lakini asikupe mtaji wa kufanya biashara?

Hivi ni kwanini mzazi yupo radhi akusomeshe mpaka PhD lakini asikupe mtaji wa kufanya biashara?

Biashara inahitaji elimu pia mkuu ni Bora usome upate maarifa hata ukipewa mtaji uwe na uwezo wa kuumanage
Hiyo elimu sio hii ya darasani ingekuwa ndio hii basi wasomi wote wangetoboa kwenye biashara.
 
Unakuta mzazi anakwambia, "Mimi nitakusomesha mpaka pale utakaposema basi" lakini kukupa mtaji heh utasubiri sana.

Mzazi atajitutumua hata Kama ada ni kubwa atailipa hivyo hivyo. Unaweza mwambia mzee, hiyo pesa badala ya kunipeleka Feza Schools, unaonaje upatie nifungue biashara? Atagoma, atakwambia mimi kazi yangu ni kukusomesha.

Siri ni nini? Kwa nini ipo hivyo? Kwanini huwa wanagoma?

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Hii ni mada ya msingi sana umeianzisha Berylyn ambayo inabidi itutafakarishe wote.

Elimu ni muhimu sana kwa kweli, ila tofauti na zamani elimu pekee haitoshi miaka ya sasa. Mzazi inabidi awe na connection ili mtoto wake anayemsomesha akimaliza amconnect na kama hana, amuandalie maisha baada ya kumaliza elimu yake.

Ipo haja ya wazazi kutambua hilo kwa sasa kwamba mtoto akisoma sio guarantee ya mafanikio kwenye maisha. Kwa hiyo asije akatumia resources zake zote alizonazo kwa ajili ya kumsomesha mtoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sorry,hivi ulifanikiwa kupata mtu wa kukushika mkono@berlyn ?
 
Back
Top Bottom