Hivi ni kwanini mzazi yupo radhi akusomeshe mpaka PhD lakini asikupe mtaji wa kufanya biashara?

Unakuta mzazi anakwambia, "Mimi nitakusomesha mpaka pale utakaposema basi" lakini kukupa mtaji heh utasubiri sana.

Mzazi atajitutumua hata Kama ada ni kubwa atailipa hivyo hivyo. Unaweza mwambia mzee, hiyo pesa badala ya kunipeleka Feza Schools, unaonaje upatie nifungue biashara? Atagoma, atakwambia mimi kazi yangu ni kukusomesha.

Siri ni nini? Kwa nini ipo hivyo? Kwanini huwa wanagoma?

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Unapewa Elimu kubwa na Bora,Bado unataka upewe na pesa!!watoto wa siku Hz Mbona vichwa maji!!tumia Elimu yako kutafuta pesa,wewe unataka samaki,mzazi kakufundisha kuvua samaki!hauna shukrani,unataka avue samaki wengi na akupe wewe kiasi wa kuuza!!!?!
 
Mimi huwa nawafikiria wazazi ambao wanasomesha mtoto nursery kwa gharama ya milioni moja na nusu kwa mwaka bado kuna gharama za usafiri na uniform! Halafu mwenyewe anakula wali tembele ili huyu mtoto wa miaka mitatu mpaka mitano asome huko. Kisha hushindwa kumpa milioni 3 kijana wake ili ajitegemee.
 
Madelu kasema tuwasaidie kujiajiri, kwa hiyo mkimaliza hizo PhD kuna mashamba yanawasubiri huku...
 
Biashara inahitaji elimu pia mkuu ni Bora usome upate maarifa hata ukipewa mtaji uwe na uwezo wa kuumanage
Nakataa syo kweli nenda kwa wahindi waarabu na wasomali alafu unambie hcho usemacho mtoto anapelekwa shule ili afaham lugha,na hesabu basi wewe sas unafundishwa mar vishazi huru mara maarifa cjui GS
 
Unakuta mzazi anakwambia, "Mimi nitakusomesha mpaka pale utakaposema basi" lakini kukupa mtaji heh utasubiri sana.

Mzazi atajitutumua hata Kama ada ni kubwa atailipa hivyo hivyo. Unaweza mwambia mzee, hiyo pesa badala ya kunipeleka Feza Schools, unaonaje upatie nifungue biashara? Atagoma, atakwambia mimi kazi yangu ni kukusomesha.

Siri ni nini? Kwa nini ipo hivyo? Kwanini huwa wanagoma?

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Sababu wao siyo wafanyabiashara. au kama ni wanyabiashara wanajua umuhimu wa elimu kwenye biashara.ndiyo maana wanakupeleka shule.ili baadaye ndiyo wakupe mtaji.au wameshajua kwamba dishi lako halikamati vizuri signal kwenye biashara,wanaona bora wafute lawama kwa kukupeleka shule ushindwe wewe
 
1. Biashara inahitaji elimu, ukiona toto linakataa shule ili lifanye biashara ujue haliko serious. Soma kwanza, then utafanya biashara kwani unakimbilia wapi? ili iweje?
2. Elimu inaweza kukupa mtaji.
3. Biashara ni ngumu kusimama especially kwa mtu anaye anza. Kuacha shule na kwenda kuanza biashara ni ukosefu wa akili. Fanya kazi kwanza ndo uanze biashara.

Kama unataka kuanzisha genge tafuta mtu mwenye genge lililofanikiwa omba kazi kwake. Fanya kazi hata bure upajlte kujifunza.

Ku conclude jibu la swali lako, mtoto mwenye umri wa kwenda shule, au chuo..akija na kukwambia kuwa hataki kusoma ila anataka mtaji kuna vitu kama vinne vinakujia haraka haraka ambavyo si vizuri katika maisha yake.

1. Ni uvivu...huyu mtoto ni mvivu hivyo hata biashara hataweza.
2. Ana tamaa na pesa za haraka haraka. Hivyo hata ukimpa mtaji atapoteza tu kwa tamaa.

3. Anapenda starehe, anataka pesa za kwenda kutanua.

4. Kuna mtu amemdanganya anataka kumtapeli.

So kumsaidia huyu mtoto ni kuto mpa mtaji na kumlazimisha asome au aingine mtaani apigike, akili ikimujia atakuja na mawazo mengine mazuri
 
Unakuta mzazi anakwambia, "Mimi nitakusomesha mpaka pale utakaposema basi" lakini kukupa mtaji heh utasubiri sana.

Mzazi atajitutumua hata Kama ada ni kubwa atailipa hivyo hivyo. Unaweza mwambia mzee, hiyo pesa badala ya kunipeleka Feza Schools, unaonaje upatie nifungue biashara? Atagoma, atakwambia mimi kazi yangu ni kukusomesha.

Siri ni nini? Kwa nini ipo hivyo? Kwanini huwa wanagoma?

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Ni kwa sababu ya aina ya thinking pattern zao, ambazo husukumwa na priorities hasa security inayotokana na ajira. Wengi wao huamini kwenye kusoma Sana, ufaulu mzuri kisha kazi yenye mshahara mnono,huku wakiamini kuwa biashara ni dude moja hatarishi yenye kupoteza pesa na kwa kukosa maarifa hizo pesa zao huwapa wenye biashara za shule ili watoto wao wapewe risiti zinazoitwa vyeti.
 
Nashukuru sijawahi kula Hela ya ada since Niko secondary napewa naenda kulipa mwenyewe kwa muhasibu enzi zile shule za serikali.

Nafika shule na Hela nyingi sana ila kabla siku haijaisha fasta sana nishamuona muhasibu.

Maana wezi walikuwa wengi
 
Tunavyojitahidi kujinyima ili nyinyi mupate elimu halafu ndiyo fadhila zenu hizi!

Ati tuwapatie mtaji badala ya elimu, hiyo mumesikia wapi? Halafu mutakuja kutusema hatukuwasomesha tumewawacha maisha yamewaharibikia.

Hamuna kheri kabisa nyinyi vijana. Mtaji tafuteni wenyewe mujiendeleze
Mi unaweza Kusema kusomesha mtoto shule ya gharama kubwa wakati uwezo wako mdogo ni upumbavu!
Elimu ya sasa inapaswa imwandae kijana kuwa na financial knowledge na creativity bila hill hata akipata kazi hizi na mishahara ya kibongo na nidhamu ya fedha hana atabakia kuwa maskini na hata kuwa na impact yeyote!
Umeona ndugu zetu wana Kagera walio wengi wameengemea sana kwenye elimu na kushindwa kuwa wafanyabiashara,wakulima au wafugaji wazuri mwisho wa siku mkoa wao unakuwa nyumba kwa kila jambo!
Saizi kusomesha ukitegemea kuja kupata ajira tu haitoshi utabaikia kuwa mtumwa na utashangaa wapambanaji kitaa unawakopa daily!
 
Unakuta mzazi anakwambia, "Mimi nitakusomesha mpaka pale utakaposema basi" lakini kukupa mtaji heh utasubiri sana.

Mzazi atajitutumua hata Kama ada ni kubwa atailipa hivyo hivyo. Unaweza mwambia mzee, hiyo pesa badala ya kunipeleka Feza Schools, unaonaje upatie nifungue biashara? Atagoma, atakwambia mimi kazi yangu ni kukusomesha.

Siri ni nini? Kwa nini ipo hivyo? Kwanini huwa wanagoma?

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Sasa ukisha pata elimu hayo mengine si utafanya mwenyewe

Ila sio kesi wewe mwanao usimsomeshe mpe mtaji
 
Mzazi ambaye ni muoga wa Biashara na ambaye sio Business minded lazima apinge tu.
 
Unakuta mzazi anakwambia, "Mimi nitakusomesha mpaka pale utakaposema basi" lakini kukupa mtaji heh utasubiri sana.

Mzazi atajitutumua hata Kama ada ni kubwa atailipa hivyo hivyo. Unaweza mwambia mzee, hiyo pesa badala ya kunipeleka Feza Schools, unaonaje upatie nifungue biashara? Atagoma, atakwambia mimi kazi yangu ni kukusomesha.

Siri ni nini? Kwa nini ipo hivyo? Kwanini huwa wanagoma?

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Vijana wakipewa pesa watanywea na kuhonga bora elimu huwezi kunywea wala kuhonga
 
Unakuta mzazi anakwambia, "Mimi nitakusomesha mpaka pale utakaposema basi" lakini kukupa mtaji heh utasubiri sana.

Mzazi atajitutumua hata Kama ada ni kubwa atailipa hivyo hivyo. Unaweza mwambia mzee, hiyo pesa badala ya kunipeleka Feza Schools, unaonaje upatie nifungue biashara? Atagoma, atakwambia mimi kazi yangu ni kukusomesha.

Siri ni nini? Kwa nini ipo hivyo? Kwanini huwa wanagoma?

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Our African parents,
 
Jiulize pia kwa nini serikali inatoa mkopo wa moja kwa moja kwa ajili ya masomo vyuoni lakini haitoi mkopo wa mtaji kwa biashara ?
 
Sijuwi ni kwanini kumpa mtu cash ni vigumu kuliko kumsaidia huduma anayotaka indirectly. Hii hata wanaokunywa pombe, ukimuomba kiasi cha shs 5000/= , hakupi, lakini atakununulia bia za shs 10000/=. Hapa kuna siri gani?! Mzee wa mada ya walevi na wanywa pombe, kuna nini hapa?
 
Ni akili za kikoloni za kurithi. Sio mbaya kusomesha ila sasa ni vema na kutazama nyakati maana zimebadilika.

Unasomesha mtoto kwa zaidi ya milioni 15 halafu anakuja kufukuzia kazi kwa miaka 5 ambayo akiipata analipwa laki 5 kama mshahara.

Ila hiyo pesa kama mzazi angemuandaa kwenye biashara pengine angemaliza tu form 4 na kuanza biashara na kutengeneza kipato cha zaidi ya milioni 3 kwa mwezi na kukuza mtaji na hata kujiendeleza kielimu akiwa na biashara yake.
 
Back
Top Bottom