macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Ustaarabu husaidia kuondoa tabia za kishenzi na kuzaa tabia za kiungwana. Kadiri muda unavyokwenda ndio binadaam wanazidi kustaarabika na kutumia njia nyingine kutatua matatizo yao badala ya kupigana. Hata ukienda nchi zilizoendelea utakuta kiwango cha kupigana kiko chini kulinganisha na nchi zinazoendelea.Nakumbuka miaka ya 80-90 ilikuwa jambo la kawaida kukuta jamaa wanapigana mitaani halafu watu wanashangilia sana.
Yaani ukiwa mtemi au gangwe basi unaonekana wa maana sana. Hata baadhi ya disco ilikuwa lazima ziishe kwa ngumi.
Kwa wale wa Iringa mtawakumbuka kina cool 9, shedadi, Ray nk