Hivi ni kwanini siku hizi watu hawapigani mitaani kama miaka ya 1980s?

Hivi ni kwanini siku hizi watu hawapigani mitaani kama miaka ya 1980s?

Ukitaka kujua wakongwe huwa kwa fix wako fiti soma uzi huu, hutaona hata mmoja atasema kama aliwahi kupigwa hapa, Kila mmoja alikuwa mtemi tu, sasa sijui nani alikuwa anapigwa, Yale yale ya shule Kila mtihan wa kwanza tu sijui nani alikuwa wa mwisho, kweli fix na watu wa zamani kama stoo na vumbi
 
Mimi kiukweli enzi zangu nimeumiza sana wenzangu kwa kuwarushia mawe kila inapotokea tumepigana. Sikuwa mtaalamu sana wa ngumi lakini nilikuwa nina shabaha sana ninaposhika jiwe kupambana na adui zangu. Ni mara chache sana jiwe nililokuwa narusha lisimpate mgomvi wangu na mara nyingi jiwe lilikuwa linaangukia eneo la kichwa.

Ugomvi na hiyo shabaha ya kuwarushia mawe wenzangu vilikuja kunigharimu sana katika masomo yangu kwa kupata suspension za mara kwa mara. Hata hivyo namshukuru sana Mungu kwa vile pamoja na suspension hizo kwenye mitihani nilikuwa nafaulu vizuri na pia sikusababisha vifo japo niliokuwa nawaumiza ambao walikuwa ni wanafunzi wenzangu walikuwa wakikaa majumbani hata mwezi mzima bila kwenda shule wakiuguza vidonda.

Hata hivyo ugomvi wangu miaka yote ulitokana na kujitetea au kutetea haki zangu baada ya uvumilivu wa muda mrefu na hata wanafunzi wenzangu walijua hilo. Ndiyo maana nimejikuta nikiupenda sana wimbo wa Coward of the County wa Kenny Rogers.
 
~~~>>Umenikumbusha miaka kadhaa nyuma..

Siku moja nilijifanya mtata... Nikamchokoza jamaa mmoja hivi..Alikuwa na kidemu chake nikawa natafuta Ujiko...


Jamaa akanipiga ngumi moja ya pua... Sijakaa sawa akanipa moja ya Sikio.. Hapo nikiangalia mbele sioni


Jamaa anaendelea kutupia ngumi.... Nikaona Izrael ananisogelea.. Nikataka kukimbia wapambe wananizuia... Wanashangilia ninavyokula ngumi


Jamaa akanifumua ngumi moja Juu ya Sikio..... Hapo damu zikaanza kutoka... Akili zika kaa sawa

Nikaona hapa nakufa....Nikajikaza... Nikaelekeza nguvu zote kichwani.... Nilimtandika kichwa kimoja cha Kujitoa mhanga.... Jamaa akapepesuka nikapata Upenyo wa kukimbia

Nilitoka Speed ambayo hata wangenikimbiza na Piki piki wasingenikamata


NB:
Ila jamaa alinifumua.
 
Mleta mada unanikumbusha mbali sana 1981 ama 1982 kama sijakosea kuna dogo flan aliingia anga zangu kijijin huko mbarali kwa kumtongoza mchepuko wangu. Nilitembeza vitasa kijiji kizima kwa madogo wote wenye umri kama wake. Maumiv makal sana niliwakabiz kwa kosa la mtu mmoja. Yan nilikuwa na bwaka nikiibuka 10 ardhin nikizama nikichomoza 20 wengine chali. Nikamchukua dogo mwengine mwembamba hiv nikamtumia kama fimbo kwa kuwacharaza. Ila kwasasa nimejikita zaid kusaka hela uzee nao ndio huo. Ila miaka iyo ya themanini nilikuwa mtemi sana
Mkuu acha kutizama sana Filamu za kihindi.
 
We pigana kwa mabavu.

Kuna wenzio wanapigana ki bantu. Shaur lako mjini hapa.

(Sio kama najisifia ila ni True Talk)

Mi nilikua na body la kawaida tu in my teenage years (19 - 23) and kind of fat. Sikua mgomvi au mpenda shari na mtu but if u wanna take it further im cool.

Nilikua na masela kibao high school people who u used to respect me much...cz nilikua mtu flan very cool nd ukiwa na urafiki na mimi lazma kuna kitu valuable uta earn.

Sasa kuna boya mmoja high skul kaenda hewa design alijaribu pick a fight with me after i asking him to repay my money niliyomkopesha. Jamaa akawa na anani push, matusi na dharau nyingi. Mi sikubishana nae....nikapiga story mbili tatu na wanangu in my crew nikawaeleza mchezo mzima.

Tukapanga jamaa tumfanyizie after tumetoka prepo.....kurudi dome. Nikawa na wanangu wengine kama 6 hivi tume nyuti sehem kimyaa....msela ile anapita tu tukamuita chemba...akaja. Tukamtia kibano cha haja na wanangu piga sanaa kibano jamaa kavimba uso mzima...piga sanaa mimbata, mateke....na tukampa week hela irudi.

Inshort yule jamaa mpaka tunamaliza shule alitokea kuniogopa mnooo cz kuna ushenzi wana walitaka kufanya kama sio mm angepotea yule.
 
~~~>>Umenikumbusha miaka kadhaa nyuma..

Siku moja nilijifanya mtata... Nikamchokoza jamaa mmoja hivi..Alikuwa na kidemu chake nikawa natafuta Ujiko...


Jamaa akanipiga ngumi moja ya pua... Sijakaa sawa akanipa moja ya Sikio.. Hapo nikiangalia mbele sioni


Jamaa anaendelea kutupia ngumi.... Nikaona Izrael ananisogelea.. Nikataka kukimbia wapambe wananizuia... Wanashangilia ninavyokula ngumi


Jamaa akanifumua ngumi moja Juu ya Sikio..... Hapo damu zikaanza kutoka... Akili zika kaa sawa

Nikaona hapa nakufa....Nikajikaza... Nikaelekeza nguvu zote kichwani.... Nilimtandika kichwa kimoja cha Kujitoa mhanga.... Jamaa akapepesuka nikapata Upenyo wa kukimbia

Nilitoka Speed ambayo hata wangenikimbiza na Piki piki wasingenikamata


NB:
Ila jamaa alinifumua.
😀😀😀😀😀
 
Hela zenyewe ziko wapi hadi tupigane hovyo?
Siku hizi mbabe pesa, anatubaka na tunaambulia maumivu tu.
Mshahara wa mwaka mmoja unatolewa kwa muamala mmoja tu wa ATM
 
Dunia ya leo asilimia kubwa wenye miili ndo waathirika. Unamrushia ngumi moja tu ananyooka unaishia gerezani. Na hizi gym zilivyokuwa fashion unaona mtu kifua nyumba kumbe bwabwa unamchapa anaanza kutoa kamasi. Mambo ya ngumi yashapitwa na wakati ukijumlisha na wanaotakata ngozi kwa kunywa maji kutembea na bastola si utaishia kuzimu tu ukianzisha vagi.
 
Mimi nakumbukia siku hzi nikipiga bia napigana sana. lkn zaman nilikuwa Na ngvu sana.
zimeisha

siku hizi watu wamestaarabika, lkn watoto hawana adab kabisa. cheki mtoto wa 1990 Hana adabu, unakuta mna share dem. mm nahonga kwa ajil ya kushikwa urobo, dogo anasmamia vidole binti hubaki njia panda.

Nguvu hatuna tena
 
Ustaarabu husaidia kuondoa tabia za kishenzi na kuzaa tabia za kiungwana. Kadiri muda unavyokwenda ndio binadaam wanazidi kustaarabika na kutumia njia nyingine kutatua matatizo yao badala ya kupigana. Hata ukienda nchi zilizoendelea utakuta kiwango cha kupigana kiko chini kulinganisha na nchi zinazoendelea.
Hivi hata mashuleni siku hizi madogo hawagombani "ngumi" kama miaka ya 80s to 90s ?
 
Mr Hero bora wewe umeliona hilo yaan hakuna anayesema alikuwa anapigwa bora mimi nlipigwa kichwa kimoja chini na sikuendelea na pambano
 
Wachangiaji wengi mmejibu kua siku hizi watu wamestaarabika na wanashughulika kutafuta pesa zaidi, lakini ukichunguza hata zile ngumi za watoto wenye umri chini ya miaka 16 hakuna tena siku hizikama ilivyokua zamani 80s to 90s...!! na watoto wa umri huo kimewapata nini nao siku hizi hawapigani mitaani?
 
Tena kulikuwa na watemi Wa mtaa, kijiji mji darasa. Shule nzima we acha tu. Nikiwa sumbawanga 1980s kulikuwa na vuguvugu sana la makarateka. Kuna jamaa akiitwa Mchemwa alikuwa anafanyia mazoezi pale jangwani primary school jamaa alikuwa fiti balaa
 
Back
Top Bottom