Haa mambo ya ugomvi.. Nakumbuka shule mitaa ya BK, tuko form three, tunasubiri kuingia fomu four. Four washamaliza mitihani, sasa form three ndio wababe na wakuu. Basi akaja mbabe mmoja , alikuwa form one anaingia fomu two, alikuwa nyantuzu Fulani limepanda, halafu haliheshimu form two , form three wala nini. Yaani kila mtu akiliona anasepa usiingie kwenye anga zake. Basi siku, tukagombea mapera , kuna mshikaji wangu amepanda anachuma ananishuria mimi naokota kama saa saba mchana. tumemaliza mitihani tunazagaa zagaa.
Basi yule mbabe akaja kuninyang'anya yale mapera aliyokuwa anarusha mshikaji wangu. Duh shule nzima wanaangalia. Nikasema huyu mshenzi , nikamlisha ngumi. Kwanza hakuamini kama mtu anaweza kuthubutu kumrushia ngumi, basi akaja kwa nguvu amalize mchezo.
Mimi nikamrukia mateke na vichwa , nikamfletisha chali.. Shule nzima wakaja kunibeba na kushangilia nilivyomuadhiri yule mbabe. Wakisema kumbe hana nguvu.
Basi si maticha wakaona hiyo movie, wananidabua kwenda staff room, kwamba nisingeweza kumpiga yule mbabe kama sio mafunzo ya kung fu, tuliyokuwa tunafundishwa na jamaa mmoja aliyekuwa anagombea udiwani hapo BK.
Nikapata viboko na ikawa ndio mwisho wa mafunzo ya kung- fu, kimoyoni vile viboko sikujali sana kwani watu walikuwa waniangalia kwa jicho jingine.
Ugomvi si mchezo.