Hivi ni kwanini siku hizi watu hawapigani mitaani kama miaka ya 1980s?

Hivi ni kwanini siku hizi watu hawapigani mitaani kama miaka ya 1980s?

Mleta mada unanikumbusha mbali sana 1981 ama 1982 kama sijakosea kuna dogo flan aliingia anga zangu kijijin huko mbarali kwa kumtongoza mchepuko wangu. Nilitembeza vitasa kijiji kizima kwa madogo wote wenye umri kama wake. Maumiv makal sana niliwakabiz kwa kosa la mtu mmoja. Yan nilikuwa na bwaka nikiibuka 10 ardhin nikizama nikichomoza 20 wengine chali. Nikamchukua dogo mwengine mwembamba hiv nikamtumia kama fimbo kwa kuwacharaza. Ila kwasasa nimejikita zaid kusaka hela uzee nao ndio huo. Ila miaka iyo ya themanini nilikuwa mtemi sana
Jirani ulitishaa, manake sio kwa mkong'oto huo uliotembeza
 
ha ha haaaa, kiongozi umenikumbusha mbali sana, kiukweli sifurahii watu wakipigana lakini zamani bhana tulikuwa tunapigana. ukichokozwa kidogo tuu unaenda kutafuta watu mnaamsha ngumi mwitu ballaa, mkono mkono. sijui chips yai zisizo kauka zimechangia au maendeleo kwa ujumla yamepiga hatua na kuongezeka kwa ustaarabu katika jamii.
 
BINAFSI SINAGA MUDA WAKUSHADADIA NGUMI COZ NIKO NA STRESS ZANGU HALAF TENA KUNA UWEZEKANO WA KIPIGO KUHAMIA KWAKO MPITA NJIA
 
Nakumbuka miaka ya 80-90 ilikuwa jambo la kawaida kukuta jamaa wanapigana mitaani halafu watu wanashangilia sana.

Yaani ukiwa mtemi au gangwe basi unaonekana wa maana sana. Hata baadhi ya disco ilikuwa lazima ziishe kwa ngumi.

Kwa wale wa Iringa mtawakumbuka kina cool 9, shedadi, Ray nk

Nimecheka sana
 
Hasa mingumi ya wanandoa tumeimiss sana, miaka ile siku haipiti salama bila songombingo mtaani - midundiko pia imepotea kabisa.
 
msinikumbushe enzi za watemi wa wazamani.akina double difu(rip) na kidume (rip).hao wote walikuwa ni mabaunsa ktk kumbi mbalimbali za starehe hapa town dsm.

walikuwa wanafanya kazi ya ziada sana maana zama hizo disko likuwa haliishi bila watu kupigina.Mara nyingi chanzo nilikuwa ni mwanamke.


Siku hizi watu wanapigana na maisha.ugumu wa maisha na harakati za utafutaji ni kipigo tosha
 
sikuhizi kupigana hela...

yaani hata bifu zinaingiza hela sio kama zamani
 
kama unataka kesi za mauaji uishi na hiyo mentality miaka hii.
watu wengi wagonjwa bila kujijua. zamani mtu kufariki kizembe ilikuwa sio kawaida.

siku nimemuona mtu anatembea mwenyew akaanguka kama kuku mwenye mdondo kilicho mpnya ni watu walikuwa karibu tukampa first aid akapata hwa angekuwa mwenyew kifo kile. maisha ngumi tosha.
 
Kupigana na mtu ni kupotezeana Muda WA Kutafuta pesa pia siku hizi watu wameshakufa wanasubiri kuzikwa tuuu, Ngumi moja mtu chali
Watu wanapigana na maisha
Watu wanatembea kumbe ndani mabua wameliwa na mchwa. Ukipiga kidogo mtu anapukutika. Lakini pia siku hizi watu wamestaarabika.
 
Back
Top Bottom