macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Ustaarabu husaidia kuondoa tabia za kishenzi na kuzaa tabia za kiungwana. Kadiri muda unavyokwenda ndio binadaam wanazidi kustaarabika na kutumia njia nyingine kutatua matatizo yao badala ya kupigana. Hata ukienda nchi zilizoendelea utakuta kiwango cha kupigana kiko chini kulinganisha na nchi zinazoendelea.Nakumbuka miaka ya 80-90 ilikuwa jambo la kawaida kukuta jamaa wanapigana mitaani halafu watu wanashangilia sana.
Yaani ukiwa mtemi au gangwe basi unaonekana wa maana sana. Hata baadhi ya disco ilikuwa lazima ziishe kwa ngumi.
Kwa wale wa Iringa mtawakumbuka kina cool 9, shedadi, Ray nk
Hahahaa...ini lishakatika...!
Hahaaa...unasikia watu kaua..kaua...lazima akili iruke!Linaning'inia.........
Acha fix wewe...eti nilimtumia dogo mwembamba kama fimbo...Mleta mada unanikumbusha mbali sana 1981 ama 1982 kama sijakosea kuna dogo flan aliingia anga zangu kijijin huko mbarali kwa kumtongoza mchepuko wangu. Nilitembeza vitasa kijiji kizima kwa madogo wote wenye umri kama wake. Maumiv makal sana niliwakabiz kwa kosa la mtu mmoja. Yan nilikuwa na bwaka nikiibuka 10 ardhin nikizama nikichomoza 20 wengine chali. Nikamchukua dogo mwengine mwembamba hiv nikamtumia kama fimbo kwa kuwacharaza. Ila kwasasa nimejikita zaid kusaka hela uzee nao ndio huo. Ila miaka iyo ya themanini nilikuwa mtemi sana
Mbolea toka vyoo vya watu hasa wa Mbezi beach wanaokula chips mayai utapata nini?Mayai ya kuku wa kisasa, chipsi za mafuta ya trans .. foma vyakula mchicha, mahindi, mpunga nk kulimwa kwa kutegemea mbolea za viwandani nk, hapo kupigana ni kujipa tiketi ya kwenda ahera.
Upige mtu kumbe ini lishakatika linasubiri kumalizika ndio utafurahi........
Mi nshasema sipigi mtu.......