Kwa watu wa CCM mliopo humu ambao at least nawaonaga mna akili kidogo ni wewe na Johnthebabtist.
Nirudi kwenye mada yako! Jibu la hayo yote uliyoandika hapo ni Sera mbovu za Chama chako na kukosa kwa akili kwa watu wa Chama chako ambao wamekuwa wakiiongoza hii nchi miaka nenda rudi kulikosababisha haya yote.
Nashukuru Mungu nimetembea nchi nyingi na nimefanya research ya kutosha. Tanzania kwa kifupi ni takataka kwenye suala la kupangilia makazi na miji yetu.
Mara nyingine huwa nafikiria kuwa ni bora mzungu angetutawala muda mrefu at least angetupangia miji yetu na maeneo yetu na kutuacha tukiishi kistaarabu.
Hata ukipita masaki saivi ni uchafu mtupu. Majengo yanajengwa hovyo bila mpangilio. Sehemu za makazi zinakuwa za biashara alafu ni biashara kichaa cha pubs za restaurants. Hakuna tena ile decency ya zamani ya oysterbay na masaki.
Maeneo mengine ndo uchafu mtupu. Makazi yanejengwa hovyo na wala hatajapangwa. Kila mtu anajiamulia ajenge anavyoona yeye sawa. Kila nyumba kuna fremu, barabarani ni vibanda vya machinga kila kona, huyu anauza mahindi, huyu nguo , huyu kaweka vyombo barabarani.
Tanzania kwa kifupi imeoza, mfano dar tu, maeneo yaliyokuwa yamependezeshwa vizuri saivi yamejaa vibanda vya hovyo hovyo na hayatamaniki tena. Mpaka Mlimani City saivi kwa nje kuna uchafu wa vibanda vya wamachinga, nenda njia ya cocacola ambayo miaka ya nyuma ilikuwa inapendeza saivi ni vibanda kila kona na uchafu mtupu.
Nchi nyingi za Africa zimeanzisha projects za satellite cities. Rwanda wanajenga kama mbili na Kagame keshafungua moja juzijuzi. Senegal wanajenga yao kubwa balaa na ya kisasa kupindukia, Kenya pia wanajenga zao mbili na ziko vizuri na Madagascar pia.
Sie huku kazi yetu ni kusifu na kuabudu upuuzi tu. Hakuna lolote la maana tunalofanya. Hatuna project yeyote ile. Mtu kiongozi anasimama anasema Eti machinga ruksa kufanya biashara sehemu yeyote ile. Ndo mana Tanzania karibu kila sehemu ni takataka.
Kuanzia Songwe, Mbeya, Iringa, Morogoro,Pwani, Dar , Mwanza , Arusha,Dodoma, kigoma , Tabora na sehemu zingine zote ni uchafu tu.
Nilikuwa nakipenda sana na kukissuport Chama cha Mapinduzi hapo awali ila nilivyozidi kupata exposure nimekuja ku gundua kuwa tumefanya makosa sana kuwaacha waendelee kututawala. Wameifanya nchi hii na maisha ya watu wa nchi hii kuwa ya hovyo sana.
Jambo linaloniuma ni kuwa kwa CCM kushindwa kusimamia vizuri suala la makazi, imepelekea watanzania wengi hadi kuona kuwa wao kuishi vizuri sehemu zilizopangwa vizuri na kujengwa vizuri ni anasa.
Shame!!!